Weupe wa maziwa usikufanye ukahisi yapo salama hivyo. Yanaweza yawe safi lakini si salama, hapa nazungumzia uwepo wa vimelea vya magonjwa, kama bacteria na virus kwa maziwa hayo.
Kuanzia uvunaji wa maziwa, uhifadhi na hata wavunaji wenyewe huweza kuleta vimelea humo. Hapa sija zungumzia magonjwa na vimelea vinavyobebwa na ng'ombe mwenyewe kutoka katika chakula, malazi , magonjwa n.k.
Hata kupata kifua kikuu inawezekana, maana vimelea vya TB vinaweza patikana ata katika maziwa, kama ng'ombe au mbuzi anaumwa tb. Pia kuhara kwa sababu maziwa huvutia bacteria wengi kuishi ndani yake, so sio poa kunywa bila kuchemsha hata kiasi maana bacteria wengi hufa kwa joto la kawaida na ukiyachemsha hakuna vitamini itapotea kwa hayo maziwa.