Maziwa ni sumu mwilini

Maziwa ni sumu mwilini

According to the Centers for Disease Control and Prevention (CDC), from 1993 through 2012,

Whose centre is it ??----- to which country does it belong??!!.

Above all Tanzanians are not milk drinking persons. Kwao kunywa maziwa ni anasa.
 
dharau hizi kabisa mimi najua tu "Please may i go to toilet" alafu analeta maandishi marefu namna hii
Hahaaa nimekumbuka tulivokua tunapata tabu hapo jamani, mwisho inabidi ujikaze mpaka kipindi cha English kipite ndo upate upenyo wa kwenda huko toi
 
Wanakutisha tu, tungeshakuzika kitambo. Napenda lile ganda/ utando wa juu kwenye maziwa mgando, tukiwa wadogo unalilia timing unalila kipande kidogo unamrushia paka kumuuzia kesi.

Sie wakati huo maziwa yanakamuliwa kwa ng'ombe bado ya moto unayapiga kwenye kipeyu bado yanatoa ule moshi
Halafu Yale matamu kinyama .. huyu jamaa mchawi tu..🤣
 
Mwana jamvi, pengine unahisi nimekosea. hapana sijakosea iko hivi, wengi tunatambua maziwa kama agent wa kuua sumu mwilini, hasa pale mtu anapozamilia kujitoa uhai akanywa sumu tunamuwahi kwa maziwa. Hiyo ni faida ndogo sana ukilinganisha madhara u anayoyapata kwa kutumia maziwa mara kwa mara.
Nawasilisha.

Umekosea maana hujatoa maelezo ya kutosha ambayo yatatufanya tuondoe unywaji wa maziwa dunia nzima.
 
Hata sielewi mmetoka kwenye chanjo ya COVID eti siyo salama sasa mmeamua kusema na maziwa ni sumu,, wakati huko vijijini maziwa wanakunywa bila kuchemsha toka kitambo,,
Kwani ww ni dokta, tumekunya maziwa ambayo hayachemshwa huko vijijini wakati tunachunga ng'ombe,,
Unayajua yale maziwa wanyakyusa wanaita MASULU ww
Umenikumbuka masulu ni matamu hayo ila ni kama mchuzi mepesii hamna matuli hata kidogo😂
 
Weupe wa maziwa usikufanye ukahisi yapo salama hivyo. Yanaweza yawe safi lakini si salama, hapa nazungumzia uwepo wa vimelea vya magonjwa, kama bacteria na virus kwa maziwa hayo.
Kuanzia uvunaji wa maziwa, uhifadhi na hata wavunaji wenyewe huweza kuleta vimelea humo. Hapa sija zungumzia magonjwa na vimelea vinavyobebwa na ng'ombe mwenyewe kutoka katika chakula, malazi , magonjwa n.k.
Hata kupata kifua kikuu inawezekana, maana vimelea vya TB vinaweza patikana ata katika maziwa, kama ng'ombe au mbuzi anaumwa tb. Pia kuhara kwa sababu maziwa huvutia bacteria wengi kuishi ndani yake, so sio poa kunywa bila kuchemsha hata kiasi maana bacteria wengi hufa kwa joto la kawaida na ukiyachemsha hakuna vitamini itapotea kwa hayo maziwa.
Hivi kuna watu wanakunywa maziwa ambayo hayajachemshwa. Duh!
 
Kweli maziwa ni sumu serikali ihamasishe watu waanze kutumia kilimanjaro lager wakubwa na watoto akizaliwa tu waanze kupewa serengeti light ili tuepuke sumu mbaya ya maziwa
 
Weupe wa maziwa usikufanye ukahisi yapo salama hivyo. Yanaweza yawe safi lakini si salama, hapa nazungumzia uwepo wa vimelea vya magonjwa, kama bacteria na virus kwa maziwa hayo.
Kuanzia uvunaji wa maziwa, uhifadhi na hata wavunaji wenyewe huweza kuleta vimelea humo. Hapa sija zungumzia magonjwa na vimelea vinavyobebwa na ng'ombe mwenyewe kutoka katika chakula, malazi , magonjwa n.k.
Hata kupata kifua kikuu inawezekana, maana vimelea vya TB vinaweza patikana ata katika maziwa, kama ng'ombe au mbuzi anaumwa tb. Pia kuhara kwa sababu maziwa huvutia bacteria wengi kuishi ndani yake, so sio poa kunywa bila kuchemsha hata kiasi maana bacteria wengi hufa kwa joto la kawaida na ukiyachemsha hakuna vitamini itapotea kwa hayo maziwa.
Mkuu kwa maziwa ya mama je mtoto anaponyonya kwa nini asiyachemshe maziwa ya mama kuepuka maradhi ?
 
Mkuu kwa maziwa ya mama je mtoto anaponyonya kwa nini asiyachemshe maziwa ya mama kuepuka maradhi ?
Maziwa ya mama hayana shida sababu yanatoka kwa binadamu na kuingia kwa binadamu mwingine, system ni moja na yana faida kibao kushinda ya ng'ombe. Lakini pia, wamama wanapewa limit ya kumnyonyesha mtoto sana sana kwa miezi sita tu (nafkiri, naeza kosolewa) na pia wanaagizwa kuwa makini na diet yao during hio period ya kunyonyesha na pia wakati wanaponyonyesha wakinge titi dhidi ya vumbi ndio maziwa yasipate uchafu mtoto anaponyonya. Tena wakina mama wanapewa kisomo ya madawa ambayo hawafai kuwa wanatumia mpaka washauriane na daktari katika kipindi hicho sababu dawa hizo hupitia kwenye mishipa na kusambaa hadi kwa titi na mtoto hufyoza maziwa yaliona dawa, so hawafai kutumia vileo au dawa strong zozote. Kila kitu kina limitation zake mkuu

Ndo maana ya ng'ombe tunayachemsha coz yule ni mnyama, digestive system yake ni tofauti na yetu, kuanzia vyakula hadi madawa mbalimbali nk., tangu akiwa mdogo hadi anakuwa.
 
Kwendraaa!.

Nimekunywa maziwa tangu nikiwa mdogo mpaka sasa. Sina tatizo lolote la kiafya.

Tena mimi nakamulia mdomoni, nayanywa moja kwa moja yakiwa ya moto. Ni matamu balaa.

Maziwa ambayo sinywi kabla ya kuchemshwa ni ya mbuzi tu. Tena sababu ya harufu tu.

Maziwa ya ng'ombe nakamulia kwenye kibuyu nashushia. Burudaani!.

Kama maziwa yangekuwa sumu, ningelikwishakufa siku mingi.
 
Back
Top Bottom