Mazungumzo ya Mfanyabiashara Rostam Aziz aliyoyafanya na UTV

Mazungumzo ya Mfanyabiashara Rostam Aziz aliyoyafanya na UTV

MdengestanfromCuba

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
667
Reaction score
743
Naam wakuu

=========================
Mfanya biashara na mwanasiasa maarufu ndugu Rostam Aziz anahojiwa katika kipindi kinachoruka muda huu kupitia channel ya UTV Azam Tv, lakini kipindi sio live, mahojiano yanaendeshwa na nguli wa habari nchini, Tido Mhando


View: https://www.youtube.com/watch?v=twTNb51Vu0A

Updates====================
"Pia mtandao unaweza kubadilika kulingana na muda na hata mazingira. Hivyo mtandao wa mwaka 1995, hata mwaka 2005 hatukuwa wote. Wengine walifariki na wengine kubadilika" amesema RA

Amesema kuwa mwaka 2015 mtandao wao haukushinda kwani Kikwete hakumuunga Hayati ENL hivyo mtandao wa Magufuli ukaweweza kushinda.

Rostam amesema wanamtandao wanabadilika kulingana na wakati na mazingira. Amesema siyo kweli kuwa mtandao wa 1995 mpaka Leo upo. Amesema mtandao wa Mkapa ulishindwa 2005 kwa hiyo huwezi kusema bado upo, amesema mtandao wao na Kikwete ulikufa 2015 na ukaingia mtandao wa JPM kwa hiyo si rahisi mtandao wa wao wao wa 2015 kuendelea kuwepo kwa kuwa mazingira na wakati vinabadilika.

Mimi nilikuwa mfanyabiashara wa kwanza kuingia bungeni, wakati huo fomu za bunge za kugombea ubunge zinabox mbili awe mkulima au mfanyakazi mimi nilikrozi zote mbili nikaandika mfanyabiashara, kwahiyo nilizua kasheshe kwenye kamati kuu ya chama wanabishana sasa huyu tunafanyaje kwa sababu si mfanyakazi wala mkulima. Siku wakabishana na hatimaye wakakubali sekta binfasi, biashara ndio tunako kwenda kwahiyo nivuziri kupata wawakilishi, Amesema Rostam Aziz
 
IMG_20250905_210224_8.jpg
 
Back
Top Bottom