Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si umeona wahanga ni wengi mkuu? Ungeitoa tu hiyo dawa hapa maana watu wanakwambia wamepaka Sulphur mpaka wakanuka ila mba umo tu!
Dawa ya mba kichwani Ndimu au limau: Kabla kwendaHabari wapendwa....naulizia yeyote anayejua dawa au mafuta mazuri yanayomaliza mba kichwani.Nywele zinawasha mtu unajikuna hadi vidonda vinaanza kutokea kichwani.Mba huo ata kama ukipakwa mafuta kama,radiant...kuza hauishi kabisa.Ni muda mrefu sasa zaidi ya miaka miwili mba hauishi kichwani.msaada wenu JF doctors na wengineo wenye ujuzi.
Duh asante kwa ufafanuzi mzuri, changamoto mimi binafsi nina nywele fupi aka size ya Brash lakini bado MBA wapo. Msisitizo nina oga daily na kusafisha kichwa, ninafuta maji yote kichwani ila sipaki mafuta ya aina yoyote kichwani
pole sana mamaa.... Jaribu maji ya battery ya gari itaweza kukusaidia...
Mpendwa hicho kinachoitwa mba si kila mara kinabeba maana halisi ya mba.Kwa maana halisi ya mba kama zile unazoona kifuani,shingoni au kwenye mashavu..zile kila mtu anakuwa nazo kama sehemu ya vimelea vya kawaida kwenye ngozi ambavyo kuonekana kwake kunategemea mabadiliko fulani ktk ngozi..Kwa mfano wakati kuna hali ya hewa ya unyevu unyevu au wakati wa ujauzito au ukitumia kemikali(inaweza kuwa sabuni,cream nk.) ambazo zinapunguza kinga ya mwili/ngozi nk..nk..nk..Unaweza kutumia dawa ya kawaida ya fangasi zikapotea..ila zinaweza kujitokeza tena ikiwa hali ile ya mwanzo itajitokeza tena(maana kumbuka vimelea vyake vipo tu wakati wote)..Aina hii inatumalizia sana hela ktk kununua dawa..tunaibiana sana ktk hilo lakini kiukweli hakuna uwezekano wa kuzimaliza kabisa kutokana na sababu niliyotoa hapo mwanzo..
Hizi za kichwani ndipo panapohitaji unifuatilie vizuri..
Tumia mfano huu:
Naelewa unatumia taulo hapo nyumbani..taulo huwa linachafuka,siyo? Ulishawahi kuiuliza linachafuka vipi wakati unalitumia uikiwa umeoga..mwili msafi? Unajua pia ni kwa nini tunapauka ikiwa hatujajipaka mafuta hata kama tumeoga?
Majibu:
Kila wakati ngozi yetu inajitengeneza upya..kwa maana kwamba chembechembe(cells) mpya za ngozi zinazaliwa huku zile za zamani zikipukutika..cells zinazaliwa kutokea ndani ya ngozi kuja juu..kama ambavyo mti unavyotengeneza maganda;kwamba ganda la nje linakuwa kavu/limekufa..kwa hiyo basi cells za juu/nje ya ngozi zinakaa kwa muda mfupi,zinakufa kisha zinapukutika..sasa hizo cells zinazopukutika ndizo kimsingi zinamaanisha ule mpauko au huchangia kuchafua taulo..ukipata mchubuko kidogo kwenye ngozi utaona kijiganda kidogo mfano wa nailoni..kile kimetengenezwa na hizi cells ninazozungumzia hapa.
Kwa upande mwingine,baada ya kuoga vizuri kisha ukakauka bila kupaka mafuta,kutakuwa na kipindi fulani ambapo ngozi itapauka..hii inatokana na kuonekana kwa sehemu ya juu iliyokufa ya hicho kinailoni nilichosema hapo juu..maana yake inakuwa inapukutika ili kuachia cells/kinailoni kipya kukaa pale juu! Lakini huu mpauko baada ya muda huanza kupotea taratibu na ngozi kuonekana ktk hali ya kawaida..hii hutokana na ngozi kujitengenezea mafuta fulani kutoka ndani yanyosukumwa kuja kunawirisha sehemu ya juu ya ngozi..
Sasa tatizo lako nini?
Kama nilivyoelezea ukuaji wa ngozi hapo juu..ninamaanisha ni pamoja na ngozi ya kichwa.Mchakato huo wote unafanyika pia kwenye ngozi ya kichwa sawa sawa kabisa na sehemu nyingine za mwili..Tunapokuwa tunaoga tunaondoa ile sehemu ya ngozi iliyokufa pamoja na uchafu mwingine ktk ngozi yetu..Sasa ktk sehemu nyingine za mwili ni rahisi kuondoa kila uchafu na kisha kujifuta vizuri ili kuacha ngozi ikiwa safi..Lakini hii ni tofauti na ngozi ya kichwa.Kule kuna nywele hivyo si rahisi kuondoa na kufuta uchafu wote(hapa namaanisha zile cells zilizokufa pamoja na uchafu mwingine)..Kushindwa kuondoa uchafu huo kunapelekea kuzidi kuongezeka kwa hizo cells zilizokufa na matokeo yake kunakuwa kama vumbi fulani hivi jeupe..ni rahisi kuliona wakati unachana nywele..Ule muwasho ni matokeo ya huo uchafu..Sasa hapa ndipo watu wanapokosea kuita MBA..kiuhalisia si mba za kawaida ila ni mchakato wa kawaida wa ukuaji wa ngozi!
Sasa mtu mwingine anaweza uliza mbona watu wengine hawana tatizo hilo? Jibu ni kwamba,si kweli kwamba hawana..maana hiyo itakuwa ni kusema kwamba,ukuwaji wa ngozi yao ni tofauti na watu wengine..hapana..kuwezakuwa ukuaji wa wa ngozi taratibu sana..au muda mwingi ngozi ya kichwa chake inakuwa na unyevu au mafuta mafuta(kumbuka nadharia ya kupauka)..lakini hii haimaanishi kwamba cells zake hazifi na kutengeneza uchafu..Lakini pia inawezekana watu wengi tunalo hilo tatizo ila hatusemi hadharani!
Tatizo hili ni kubwa kwa watu wenye nywele ndefu..na ni hakina kabisa kwamba kwa watu wasiofuga nywele kwao si tatizo kabisa..Niseme mapema kwamba si kweli kwamba kuwa na tatizo hili kunamaanisha mtu haogi vizuri..hapana.. Kwa jinsi ngozi ya kichwa ilivyo na nywele inafanya uwepo ugumu wa wa namna bora ya kusafisha ile ngozi.
Mimi mtu angeniuliza afanye nini ili kuondokana na tatizo hili..jibu langu lingekuwa fupi tu..USIRUHUSU NYWELE KUWA NDEFU!! Najua hii si habari njema kwa akina dada na akina mama..lakini huo ndio ukweli wenyewe.
Kwa hiyo @Anne deo kusema una mba sugu mimi nitasema sio..

Tumia dawa inaitwa Ketoconazole ipo cream kwenye tube na shampoo kwenye chupa. Nunua zote elfu 15 kwa elfu 20 halafu anza kuoshea nywele hiyo shampoo na ukimaliza paka hiyo cream. Wallah baada ya wiki utaona kwisha. Mimi yamenitokea kwa wanangu yalikuwa sugu mno miaka kama miwili.
Dawa ya mba kichwani Ndimu au limau: Kabla kwenda
kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya
kukoga yaani yawe ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji
yaliyo safi.
Au Dawa ya pili ya Mba tumia hii hapa Fenugreek kwa kiswahili inaitwa Uwatu . Hii unachukua
vijiko 2 vya chai vya fenugreek unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika,
halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa
moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu
yoyote.Tumie kisha uje unipa Feedback Chanzo .MziziMkavu
![]()
Kiingereza Fenugreek Seed Lugha ya Kibantu Kiswahili (Uwatu) Lugha ya kiarabu Dawa hii inaitwa Hilba.
Mrimi naomba unisaidie mimi sasa hadi usoni hizo cells zinapukutika tena nakuwa kama nababuka uson lkn kwa somo lako nimeelewa vizur sasa naomba unisaidie kwa hili maana kuna dhalura za kutokupaka mafuta siku nyingine yaan nisipopaka tu napauka ajabu!
Mkuu pole sana.
Maelezo yangu hapo juu nimejaribu kueleza jinsi hicho kinachoitwa mba kinavyotokea..Lakini pamoja na hayo maelezo,sikatai kwamba inawezekani kukawepo na mba kichwani..hapana..inawezekana ngozi ya kichwa ikawa na mba(kwa maana ya mba za ukweli) ila kama nilivyosema hapo juu,vimelea vinavyosababisha mba ni sehemu ya vimelea vya kawaida kwenye ngozi..kwa hiyo unaweza kutumia daya ya kawaida ya fangasi(ketakonazole,whitefield,pamoja na hata za kienyeji,nk..nk.) zikapotea ukadhani umepona,lakini kiukweli kutokana na asili ya vile vimelea,baada ya muda(wiki au hata miezi) zinarudi kama mwanzo,tena kwa kasi na nguvu zaidi.
Mkuu tukirudi kwenye swala lako,binafsi sioni kama ni tatizo..ikiwa ukijipaka mafuta hali hiyo inapotea,basi hizo dharura (unazosema) si hoja..maana hata mimi na wengine tukioga na kukaa bila kupaka mafuta tunapauka..hatuwezi kusema huo ni ugonjwa..kwa kawaida sehemu za mwili zilizo wazi(exposed to sun) kama usoni zinapauka zaidi kulinganisha na zile zilizojificha..
Kuna vitu watu wanakosea sana..na tunadanganyana sana na kuibiana sana..vitu vingi tunavyotumia vina madara makubwa ktk ngozi zetu.Kwa kawaida ngozi yetu ni sehemu muhimu katika kuukinga mwili wetu dhidi ya maradhi.Na kwenye ngozi kuna mafuta mafuta na vimelea vya aina mbalimbali vinyotusaidia kupigana na vimelea hatari vyenye madhara kwenye ngozi..kwa hiyo tunatakiwa kujitahidi kuiweka ngozi ktk hali inayoruhusu kukuwa kwa vimelea hiyo vya ulinzi pamoja na kuruhusu hayo mafuta mafuta kutengezwa na kudumu ktk ngozi..sasa hizi kemikali tunazotumia ikiwa ni pamoja na sabuni na vipodozi mbalimbali tunavyotumia vinatupunguzia hiyo kinga ya asili..
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba,hata hizi sabuni za dawa tunazouziwa tunaambiwa ni nzuri kwa ngozi..madhara yake ni makubwa kuliko faida zake kwenye ngozi..Siko hapa kuharibu biashara za watu ila nafanya tu kuema ukweli ambao watu hawapendi usemwe..Kiukweli,kule kuharibu tu balance ya asili ya ngozi,ndio mwanzo wa matatizo ya ngozi yako..Tena,hata kuoga mara nyingi kwa siku kuna madhara mengi kuliko faida zake kwenye ngozi!! Utakuwa salama tu ikiwa hutatumia sabuni! Sisemi watu wasioge..hapana.. ninasema ukioga mara mbili kwa siku kwa kutumia sabuni ni salama zaidi kuliko kuonga mara 7 kwa siku kwa kutumia sabuni! Of course,unaweza kuoga asubuhi kwa sabuni lkn hapo katikati mchana unaweza kuoga mara nyingi uwezavyo ila cha msingi tu usitumie sabuni,halafu usiku ukatumia sabuni.
Of course hili linaweza kuwa somo ambalo halijazoeleka kwa watu ila nasisitiza..matatizo mengi ya ngozi yetu yanatokana na tabia zetu za kujiweka safi kupita kiasi!! Kwa hiyo ndugu yangu,hebu jichunguze..usoni unajisafisha mara ngapi na unatumia sabuni gani..
Mimi ningeulizwa nitoe mapendekezo,ningeshauri tuachane na hizi sabuni zenye kemikali nyingi..ningeshauri watu watumie sabuni za kawaida za vipande..na tena nigeenda mbali zaidi kwa kushauri watu wasioge kwa sabuni zaidi ya mara mbili kwa siku..Of course,kutokana na maumbile yetu unaweza kutumia sabuni sehemu kadhaa za mwilli kama kwapa nk..nk. Lakini isiwe ile mtu anajipanga kuingia bafuni utadhani anakwenda vitani..anabeba vikorokoro viiingi..unawezasema kesho haogi tena!!
Kwa hiyo mkuu,nimalizie kusema,wewe jichunguze,unasafisha uso mara ngapi na unatumia sabuni gani..na hata wakati mwingine mafuta tunayotumia yanakuwa na madhara vile vile..maana kumbuka,ngozi yenyewe ina mfumo wa asili wa kujitengenizea mafuta yake..sasa tukitumia chemikali yoyote inayopungunzia ngozi uwezo wake wa kujitunza ndipo tunapopata madhara kama haya..
Asanteni.
Hamna madhara yoyote usipomtoa hizo nywele za utotoni. Ila Mtoto huyo hana mba kichwani bali ni uchafu wa ukoko ambao mtoto huja nao wakati ulipotoka kujifungua.
Mpakaze mafuta mengi ya mgando hapo kichwani na utosini, na usiache kichwa kikawa kikavu. Kama ana nywele nyingi mpunguze kidogo, halafu baada ya kumuacha na hayo mafuta muda mrefu jaribu kama kumchana huku ukikwangua huo uchafu taratibu sana. Kumbuka huyo ni mtoto mdogo hivyo usifanye kwa nguvu. @IvyAngel Nakutakia malezi mema ya mtoto huyo.