Mbagala (Dar): Baadhi ya maeneo ya barabara yaliyokuwa yanazibwa na 'machinga' yaanza kuwa wazi

Mbagala (Dar): Baadhi ya maeneo ya barabara yaliyokuwa yanazibwa na 'machinga' yaanza kuwa wazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2026-03-03_16-41-06.jpg
Baadhi ya wafanyabiashara wa biashara ndogondogo (machinga) waliokuwa wakifanyia shughuli zao katika maeneo yasiyo rafiki, hususan barabarani na kwenye njia za watembea kwa miguu, wameanza kupisha na kuondoka katika maeneo hayo.

Tukumbuke kuna mdau aliwahi kuleta andiko hapa jukwaani akieleza kuwa wafanyabiashara wanaopanga mbao na kupanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara walikuwa wakisababisha foleni, hali iliyofanya magari kuchukua muda mrefu kupita katika eneo la Mbagala Rangi Tatu.

Hata hivyo, katika eneo hilo bado kuna changamoto, ikiwemo baadhi ya watu kutotumia daraja la kuvuka barabara. Hali hii inachangia msongamano wa watu wanaokatiza barabarani ovyo na kusababisha foleni kubwa, hasa nyakati za jioni.

Ni jambo jema ikiwa mamlaka zimechukua hatua kushughulikia tatizo hili. Hata hivyo, natoa wito kwa mamlaka kuhakikisha wafanyabiashara hao wanatengewa maeneo rafiki ya kufanyia shughuli zao ili waweze kuendelea kujipatia kipato bila matumizi muhimu ya barabara.

Aidha, natoa wito kwa mamlaka kuchukua hatua zaidi kwa kuweka uzio wa vyuma katika barabara ya Mbagala Rangi Tatu, kama ilivyofanyika katika Barabara ya Morogoro kuanzia kwenye daraja la kuvusha watembea kwa miguu kuelekea Stendi ya Magufuli. Uwekaji wa uzio huo utasaidia kupunguza uvukaji holela wa barabara, kupunguza msongamano, na kurahisisha upitaji wa magari, pamoja na kupunguza ajali ikizingatiwa uwepo wa mwendokasi.

Pia soma ~ Foleni Mbagala inakera sana, ‘Trafiki’ wapo bize na Daladala tu
 
Hao ndo wapiga kura wao sio rahisi kuwaondoa zaidi ya kutoa matamko tu juu yao.

Ila ni sababu kubwa ya foleni maeneo mengi yenye watu wengi.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
hapo wameondoa tu yale mabanda , wameleta hizo meza nyepesi
 
Back
Top Bottom