Mbagala, Dar: Polisi yawanyakua watu 27 Walioiba Saruji kwenye ajali

Mbagala, Dar: Polisi yawanyakua watu 27 Walioiba Saruji kwenye ajali

KUKAMATWA WATU 27 KWA TUHUMA ZA KUIBA MIFUKO YA SARUJI BAADA YA AJALI YA MALORI MBAGALA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu 27 kwa tuhuma za kuiba mifuko ya saruji baada ya ajali ya malori mawili eneo la Mbagala Mission.

Mnamo tarehe 04/10/2021 saa 04:30 asubuhi eneo la Mbagala Mission, Lori lenye namba za usajili T 164 DKC aina ya Horse na tela lake namba za usajili T 342 DJZ likiwa limebeba mifuko ya saruji lilipata ajali na kutumbukia kwenye mtaro kutokana na tairi kupasuka.
Baada ya ajali hiyo kutokea zaidi ya watu 50 walijitokeza na kuiba mifuko ya saruji.

Aidha, tarehe 05/10/2021 majira ya saa 06:40 usiku eneo la Mbagala Mission, Lori lingine lenye namba za usajili T 705 AUE lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 911 ATR likiendeshwa na MUHIDINI HUSSEIN (39),mkazi wa Morogoro, likitokea Mbagala kuelekea mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji nalo lilipata ajali.

Polisi walifika mapema eneo la tukio na kuwakuta watu 27, wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye Pikipiki na Bajaji. wote walikamatwa na jumla ya mifuko 368 iliokolewa ikiwemo 10 iliyokutwa kwenye nyumba za watu.

Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Onyo;-
Jeshi la Polisi halitasita kushughulika kikamilifu kwa mujibu wa sheria na watu wote wenye tabia ya kukimbilia kwenye matukio ya ajali badala ya kuokoa watu na mali, wao wanageuka kuwa wahalifu/wezi.

MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

Pia soma;

Thread 'Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji' Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Umasikini hupelekea roho mbaya siku zote!!usitegemee upate matatizo kwenye maeneo ya watu masikini na wahuni utapata msaada!!
FB_IMG_1597733863117.jpg
 
Hapo kwenye idadi ni UONGO.
hakuna gari ya cement inayobeba mifuko 700.
tani 30 ni mifuko 600.kama gari ilibeba mifuko 700.
Kiwanda kilifanya makosa.
 
Cpati picha lori hilo lingepata ajari maeneo ya arusha/kilimanjaro 😁
 
Ajali zimekuwa nying Sana barabaran kumekuwa kwamoto Yan kila siku Ajali kulikon kamanda wa usalama barabaran au traffic wamepungua au traffic siku hiz kaz yao n kupiga touch na kukusanya mapato na s elimu ya barabaran
 
Safi,
Watu 27 kwa mifuko 700,
Ni sawa na laki 4 hvi @ mmoja.
Na za polisi, Milion moja moja
 
Walikua wanajiokotea.

Ila wanaume wa Dar nao wazembe, watu 27 mnakamatwa na polisi usikute polisi 6.
Walikua wanajiokotea.

Ila wanaume wa Dar nao wazembe, watu 27 mnakamatwa na polisi usikute polisi 6.
Wabongo hatujazoea milio ya risasi bana. Ikipigwa moja hewani tu: paa!! hata aliyekuwa anaharisha chooni atatoka ndukiii!!!
 
KUKAMATWA WATU 27 KWA TUHUMA ZA KUIBA MIFUKO YA SARUJI BAADA YA AJALI YA MALORI MBAGALA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu 27 kwa tuhuma za kuiba mifuko ya saruji baada ya ajali ya malori mawili eneo la Mbagala Mission.

Mnamo tarehe 04/10/2021 saa 04:30 asubuhi eneo la Mbagala Mission, Lori lenye namba za usajili T 164 DKC aina ya Horse na tela lake namba za usajili T 342 DJZ likiwa limebeba mifuko ya saruji lilipata ajali na kutumbukia kwenye mtaro kutokana na tairi kupasuka.
Baada ya ajali hiyo kutokea zaidi ya watu 50 walijitokeza na kuiba mifuko ya saruji.

Aidha, tarehe 05/10/2021 majira ya saa 06:40 usiku eneo la Mbagala Mission, Lori lingine lenye namba za usajili T 705 AUE lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 911 ATR likiendeshwa na MUHIDINI HUSSEIN (39),mkazi wa Morogoro, likitokea Mbagala kuelekea mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji nalo lilipata ajali.

Polisi walifika mapema eneo la tukio na kuwakuta watu 27, wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye Pikipiki na Bajaji. wote walikamatwa na jumla ya mifuko 368 iliokolewa ikiwemo 10 iliyokutwa kwenye nyumba za watu.

Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Onyo;-
Jeshi la Polisi halitasita kushughulika kikamilifu kwa mujibu wa sheria na watu wote wenye tabia ya kukimbilia kwenye matukio ya ajali badala ya kuokoa watu na mali, wao wanageuka kuwa wahalifu/wezi.

MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

Pia soma;

Thread 'Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji' Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji
Niliona taarifa ya habari ITV ila nilijiuliza wezi hawa wamekamtwa, wezi wale wa mafuta Morogoro tuliaminishwa ni mashujaa na pesa wakapewa, ni nini tofauti yao, kwanini na hawa wasiwe mashujaa mbele ya serikali ileile? Wezi wa Morogoro tupo tuliowaita ni wezi na wangestahili adhabu, badala yake tukaonekana wabaya!
 
Hata hivyo polisi walizembea Sana tena Sana. Yaani watu mpaka wanaiba wao walikuepo wapi
Mawazo ya kijijga sana! Kwani kazi ya polisi ni kufukuza wezi, ni kukamata wezi
 
likitokea Mbagala kuelekea mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji nalo lilipata ajali.

Polisi walifika mapema eneo la tukio na kuwakuta watu 27, wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye Pikipiki na Bajaji. wote walikamatwa na jumla ya mifuko 368
Nusu ya mzigo umeibiwa halafu unasema so and so walifika mapema!!! Kama walifika mapema si wangeokoa yote usingeibiwa hata mfuko mmoja!!!
 
Nimewaza kama wewe mkuu.

Yawezekana vipi malori mawili kwa wakati tofauti ndani ya masaa 12 yapate ajali eneo lile lile. Na malori yamebeba bidhaa ile ile?

Coincidence? Sidhani.

Ila hao wapuuzi acha washikishwe adabu maana watanzania tumekuwa wapuuzi sana.
Akili za hao madereva sawa na wale "...ndugu yangu aliyepotea miaka mingi amepatikana kwa juhudi za mganga Jumwa Huswen, kwakweli huyu mganga kiboko..."

Ukifuatilia vizuri utakuta hao madereva wanahusiana
 
Back
Top Bottom