Mbagala, Dar: Polisi yawanyakua watu 27 Walioiba Saruji kwenye ajali

Mbagala, Dar: Polisi yawanyakua watu 27 Walioiba Saruji kwenye ajali

Huu msemo unakuwa vice vesa kwamba tajiri kuona ufalume wa binguni Ni ngumu....hapaa naona maskini kuona ufalume wa mbinguni ndo mtihani
 
Kuna mtu namjua ni mpigaji aliibiwaga mizigo
Yake sasa ilibd aingie front aende huko kutemesha,nlimsindikiza nlicheka sana
Mpigaji kpigwa😂😂😂
Tuliingia kijiji kimoja watu wote watu wa deal wezi

Ova
Nami hufurahishwa sana na matukio kama hayo: jambazi kuvamiwa na kuporwa ama kuuawa akiporwa, mwizi kuvunjiwa na kuibiwa, mbabe kupigwa, mzinzi kuchukuliwa mke nk nk.

Tukija kwenye "animal planet" sasa, simba akizingirwa na kuliwa na fisi ama mamba, fisi kukamatwa na kuliwa na simba, nyoka kumeza mjusi na nyoka kumezwa na kenge, kenge kumezwa na mamba huku akilalamika!

Nikiangalia matukio ya namna hiyo hujisikia burudani nikifarijika kuona kwambakumbe dunia haina mbabe hii, bali ni timing tu.
 
Ile clip ya lile tukio niliiona.
Mimi nilidhani Ni wananchi wenye Nia njema wanaokoa Mali na kwenda kuihifadhi sehemu salama.
 
Nao wakiibiwa wanaumia 😂😂😂

Ova
 
Ile clip ya lile tukio niliiona.
Mimi nilidhani Ni wananchi wenye Nia njema wanaokoa Mali na kwenda kuihifadhi sehemu salama.
Wananchi wote wale ni wezi tu
Wanaume,wanawake,wazee,vibibi

Ova
 
Ile clip ya lile tukio niliiona.
Mimi nilidhani Ni wananchi wenye Nia njema wanaokoa Mali na kwenda kuihifadhi sehemu salama.
Wananchi wote wale ni wezi tu
Wanaume,wanawake,wazee,vibibi

Ova
 
KUKAMATWA WATU 27 KWA TUHUMA ZA KUIBA MIFUKO YA SARUJI BAADA YA AJALI YA MALORI MBAGALA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu 27 kwa tuhuma za kuiba mifuko ya saruji baada ya ajali ya malori mawili eneo la Mbagala Mission.

Mnamo tarehe 04/10/2021 saa 04:30 asubuhi eneo la Mbagala Mission, Lori lenye namba za usajili T 164 DKC aina ya Horse na tela lake namba za usajili T 342 DJZ likiwa limebeba mifuko ya saruji lilipata ajali na kutumbukia kwenye mtaro kutokana na tairi kupasuka.
Baada ya ajali hiyo kutokea zaidi ya watu 50 walijitokeza na kuiba mifuko ya saruji.

Aidha, tarehe 05/10/2021 majira ya saa 06:40 usiku eneo la Mbagala Mission, Lori lingine lenye namba za usajili T 705 AUE lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 911 ATR likiendeshwa na MUHIDINI HUSSEIN (39),mkazi wa Morogoro, likitokea Mbagala kuelekea mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji nalo lilipata ajali.

Polisi walifika mapema eneo la tukio na kuwakuta watu 27, wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye Pikipiki na Bajaji. wote walikamatwa na jumla ya mifuko 368 iliokolewa ikiwemo 10 iliyokutwa kwenye nyumba za watu.

Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Onyo;-
Jeshi la Polisi halitasita kushughulika kikamilifu kwa mujibu wa sheria na watu wote wenye tabia ya kukimbilia kwenye matukio ya ajali badala ya kuokoa watu na mali, wao wanageuka kuwa wahalifu/wezi.

MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

Pia soma;

Thread 'Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji' Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji
This is all about poverty!
 
Back
Top Bottom