Mbali na kuikosoa serikali kuhusu Makato; lakini kiukweli Watanzania kwenye kulipa Kodi tuwagumu sana

Elimu ya kulipa kodi inatakiwa itolewe tokea ukiwa mdogo ili ukifika ukubwani uilipe kwa hiari bila shuruti...
 
Kama ni kweli mawaziri na wabunge hawakatwi kodi kwenye mishahara yao basi inashangaza sana na ni tatizo kubwa sana maana wao wanatakiwa wawe mfano kwa raia wengine. Tunaomba sana wabunge na viongozi wote wa serikali waanze kukatwa kodi kwenye mishahara na marupurupu yao yote wanayoyapata ili wawe mfano kwa wananchi.
 
Mimi naelewa wabunge wanakatwa kodi kutoka kwenye mishahara yao kumbe siyo, kama kweli hawakatwi kodi basi ni tatizo kubwa sana na ni ngumu sana kuhamasisha watu walipe kodi wakati kuna tabaka la watu hawalipi kodi kabisa.
 
Tatizo wala sio kwa walipa kodi, bali ni wakusanya hizo kodi, wanazitumia kwa manufaa ambayo huyo mlipa kodi anayaona?!!mfano mdogo kwenye mambo ya ushuru kwenye masoko, kuna ushuru wa uzoaji taka, kila siku mfanyabiashara anatozwa 300!!lakini takataka hazizolewi kwa wakati hadi waanze tena kupiga kelele, kesho huyo atakuwa na moyo wa kulipia hiyo huduma, sana sana atasikia pesa fulani zimeliwa!!huko kwingine utasikia mabilioni yameliwa, waliyo yala wala hakuna hatua wanayochukuliwa, zaidi utasikia tu kuwa tumeunda tume, ndio limekwisha hilo!!viongozi wakubwa ambao wana vipato vikubwa hawakatwi kodi, kwa ufupi mtu anaona hata akilipa kodi haoni tofauti na asipolipa, jiulize mbona wazungu hawana tabia hizo?!!
 
Halafu linasimama li kiongozi eti KODI NI UZALENDO!!!wakati wao hawalipi , haya yote ni kutokana na UPIMBI WETU WANANCHI.
 
Ugumu wenyewe unakuja kama na hawa waze wa kazi nao wangekuwa wepesi kuilipa hiyo kodi yenyewe kutoka ktk mishahara yao kma palr mjengoni mtu anakula m12 kwa mwezi tungeanzia apa kwenda mbele!
 


Umesema kweli Mkuu
 
Ugumu wenyewe unakuja kama na hawa waze wa kazi nao wangekuwa wepesi kuilipa hiyo kodi yenyewe kutoka ktk mishahara yao kma palr mjengoni mtu anakula m12 kwa mwezi tungeanzia apa kwenda mbele!


Viongozi wanatoka kwenye jamii yetu, hatuwakodishi au kuwatoa mbinguni
 


Mbona bado hujashangaa Mkuu
 
Elimu ya kulipa kodi inatakiwa itolewe tokea ukiwa mdogo ili ukifika ukubwani uilipe kwa hiari bila shuruti...


Hata wapewe Elimu, hulka ya binadamu imekaa hivyo

Namna Bora ni kutengeneza mifumo ambayo mlipa kodi hawezi kukimbia.

Watu hawatoi Zaka na Sadaka sembuse Kodi
 

Umenena Kwa uchungu Sana Mkuu
 
Duniani kote watu ni wagumu kulipa kodi. Hata enzi za Yesu suala la kodi ni mshikemshike. Sababu zipo nyingi lakini kubwa zaidi ni jinsi gani kodi inayokusanywa inavyotumika.
Kama unafikiri Watanzania ni wagumu zaidi ya mataifa mengine tafuta sababu za ziada za huo ugumu.
 
Ni vyema ila wao wawe mfano pia, sio kupuyanga tu kisha wanataka sie ndio tulipishwe mikodi kandamiziπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Wao wagongwe spana pia maana wana maisha ya kifahari sana! Wao wakishalipa kodi itatupa moyo na sisi


Wao ni Kwa sababu Wana namna ya kukimbia,
Sisi wa kina Katope hatuna njia ya kukimbia πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 

Nakubaliana na wewe kabisa.

Ila Case study Kwa Uzi huu ni Tanzania Mkuu
 


Mkuu umetoa ushauri mzuri Sana.
 
Achana na hayo mambo ya directly.
Serikali ifanye wanaolipa kodi kuwa wengi. Na njia pekee ni kukuza uchumi kwa kuondoa vikwazo vinavyokwamisha biashara na uwekezaji.
Sababu kuu ni kutokana walipa Kodi directly ni wachache, hivyo lazima wachache waumie mno.

Ila Kama Kila mtu angelipa Kodi kulingana na Uchumi wake, Kodi ingepungua
 
SERIKALI ya Tanzania inaongozwa na Watanzania wachache waliopata bahati ya kuwa Viongozi.

Imagine wewe unakimbia Kodi sasa hivi na sio kiongozi, Inategemea ukiwa kiongozi utatoa Kodi?
Tatizo la kusoma na kutoelewa ni kubwa Tanzania. Je umeelewa nilichoandika? Kwangu mimi kodi ni muhimu sana kwani bila kodi basi hakuna nchi. Soma tena: nimesisitiza kodi itozwe na itumike vizuri ili watu watoe kwa wingi!!!
 


πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Mkuu hayo yote yalikuwepo tangu kuumbwa Kwa dunia, lakini bado hatatusaidii na huenda yasitusaidie kabisa
 
Tatizo la kusoma na kutoelewa ni kubwa Tanzania. Je umeelewa nilichoandika? Kwangu mimi kodi ni muhimu sana kwani bila kodi basi hakuna nchi. Soma tena: nimesisitiza kodi itozwe na itumike vizuri ili watu watoe kwa wingi!!!


Hakuna asiyejua umuhimu wa Kodi,
Kama vile hakuna asiyejua umuhimu wa Zaka na Sadaka lakini binadamu ndio tupo hivyo.

Nimekusoma na nimekuelewa sema wewe ndio huangalii uhalisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…