Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi naelewa wabunge wanakatwa kodi kutoka kwenye mishahara yao kumbe siyo, kama kweli hawakatwi kodi basi ni tatizo kubwa sana na ni ngumu sana kuhamasisha watu walipe kodi wakati kuna tabaka la watu hawalipi kodi kabisa.Unalipa kodi halafu unasikia wabunge walopitisha ulipe kodi wao hawalipi, mara waziri wa fedha anayetuambia tulipe kodi tena kwa dharau yeye anakwepa kodi, hujakaa sawa unasikia wizara ya fedha wamejilipa mamilioni kipuuzi puuzi tu. Halafu mtu aniambie nidai risiti, nehiiii.
Tatizo wala sio kwa walipa kodi, bali ni wakusanya hizo kodi, wanazitumia kwa manufaa ambayo huyo mlipa kodi anayaona?!!mfano mdogo kwenye mambo ya ushuru kwenye masoko, kuna ushuru wa uzoaji taka, kila siku mfanyabiashara anatozwa 300!!lakini takataka hazizolewi kwa wakati hadi waanze tena kupiga kelele, kesho huyo atakuwa na moyo wa kulipia hiyo huduma, sana sana atasikia pesa fulani zimeliwa!!huko kwingine utasikia mabilioni yameliwa, waliyo yala wala hakuna hatua wanayochukuliwa, zaidi utasikia tu kuwa tumeunda tume, ndio limekwisha hilo!!viongozi wakubwa ambao wana vipato vikubwa hawakatwi kodi, kwa ufupi mtu anaona hata akilipa kodi haoni tofauti na asipolipa, jiulize mbona wazungu hawana tabia hizo?!!Kwema Wakuu!
Kama nilivyoeleza kwenye heading hapo, suala la ulipaji Kodi Kwa sisi Watanzania ni kipengele. Watanzania wengi wetu Kama sio wote hatupendi kulipa Kodi.
Hata wanaolipa Kodi ni kutokana na hawana jinsi mazingira yanawabana tu.
Ila Kama wangeambiwa kwa hiyari yao nakuhakikishia watu wasingelipa kodi.
Watumishi wa Umma kama sio kukatwa juu kwa juu kwenye mishahara Yao na waajiriwa wa sekta binafsi zile kubwa, wangekuwa wanalipwa mikononi mwao kisha wao wenyewe ndio wakalipe Kodi, na kuhakikishia kodi isingelipwa.
Siku ya jana nilikuwa naongea na Mbunge mmoja ambaye ni rafiki yangu sana, akanichekesha mno. Nilipomgusia suala la kukatwa Kodi kwenye mishahara yao, alionyesha kukasirishwa Sana na mpango huo. Hataki kabisa Mshahara wake uguswe, yaani alikuwa mkali Kama mbogo ungedhani Mimi ndiye ninayemkata😃😃😃.
Usishangae Rais halipi Kodi,
Usishangae Mawaziri na wabunge hawalipi Kodi,
Kodi kulipa Kwa Watanzania ni kipengele.
Hata hivyo nafahamu kuna indirect Tax ambazo watu hulipa Kodi, lakini hapa nazungumzia Direct Tax.
Maeneo niliyowahi kuishi, Wafanyabiashara wakisikia TRA au Manispaa wanakuja, utashindwa kushangaa, watu watafunga MADUKA, ofisi na kukaa pembeni wakijifanya sio wakazi wa eneo hilo😃😃😃
Haya ninayoyazungumza wote tunayajua, hakuna asiyejua kuwa Watanzania wengi ni mabingwa waliobobea Kwa kukimbia kulipa Kodi.
Wanaoomba joto ya jiwe ni Wafanyabiashara WA mjini, katikati ya Mji au jiji hawa mazingira hatawaruhusu kuwakimbia TRA Ila vinginevyo, wangekuwa nao wanakimbia tuu.
Kama Watanzania wengi tungekuwa tunapenda kulipa Kodi, nakuhakikishia nchi hii ingekuwa moja ya nchi zilizoendelea.
Kama Watanzania wengi tungekuwa tunapenda kulipa Kodi, nakuhakikishia Wafanyakazi WA TRA wangekuwa na maisha ya kawaida Sana, kwani mishahara yao sio mikubwa kihivyo lakini Rushwa ndio inawafanya watambe hapa mjini.
Ukitaka kuwabana Watanzania wengi yaani wengi walipe Kodi basi hakikisha unawabana kwenye Maeneo yanayotumiwa na wengi na walipe indirect way.
Kwa mfano, kwenye MIAMALA ya simu, vocha Kama serikali ilivyofanya,
Sema serikali iangalie kwenye Kodi zenyewe wazikatazo waweke walau nafuu sio haya makato nyonyaji,
Masuala ya Luku waongeze, Masuala ya Bill ya maji waongeze,
Lengo sio kuwakomoa Watanzania Bali kuwafanya walipe Kodi, maana Kwa njia ya kawaida serikali imethibitisha haiwezi kulipisha Watanzania Kodi.
Na Watanzania wengi tumethibitisha hatuwezi kulipa Kodi Kwa hiyari yetu pasipo nguvu.
Nawasilisha, mwenye hoja karibu, na wenye povu pia Ruksa
Taikon wa Fasihi
Ruaha, Iringa
Halafu linasimama li kiongozi eti KODI NI UZALENDO!!!wakati wao hawalipi , haya yote ni kutokana na UPIMBI WETU WANANCHI.Kama ni kweli mawaziri na wabunge hawakatwi kodi kwenye mishahara yao basi inashangaza sana na ni tatizo kubwa sana maana wao wanatakiwa wawe mfano kwa raia wengine. Tunaomba sana wabunge na viongozi wote wa serikali waanze kukatwa kodi kwenye mishahara na marupurupu yao yote wanayoyapata ili wawe mfano kwa wananchi.
Tatizo wala sio kwa walipa kodi, bali ni wakusanya hizo kodi, wanazitumia kwa manufaa ambayo huyo mlipa kodi anayaona?!!mfano mdogo kwenye mambo ya ushuru kwenye masoko, kuna ushuru wa uzoaji taka, kila siku mfanyabiashara anatozwa 300!!lakini takataka hazizolewi kwa wakati hadi waanze tena kupiga kelele, kesho huyo atakuwa na moyo wa kulipia hiyo huduma, sana sana atasikia pesa fulani zimeliwa!!huko kwingine utasikia mabilioni yameliwa, waliyo yala wala hakuna hatua wanayochukuliwa, zaidi utasikia tu kuwa tumeunda tume, ndio limekwisha hilo!!viongozi wakubwa ambao wana vipato vikubwa hawakatwi kodi, kwa ufupi mtu anaona hata akilipa kodi haoni tofauti na asipolipa, jiulize mbona wazungu hawana tabia hizo?!!
Ugumu wenyewe unakuja kama na hawa waze wa kazi nao wangekuwa wepesi kuilipa hiyo kodi yenyewe kutoka ktk mishahara yao kma palr mjengoni mtu anakula m12 kwa mwezi tungeanzia apa kwenda mbele!
Kama ni kweli mawaziri na wabunge hawakatwi kodi kwenye mishahara yao basi inashangaza sana na ni tatizo kubwa sana maana wao wanatakiwa wawe mfano kwa raia wengine. Tunaomba sana wabunge na viongozi wote wa serikali waanze kukatwa kodi kwenye mishahara na marupurupu yao yote wanayoyapata ili wawe mfano kwa wananchi.
Elimu ya kulipa kodi inatakiwa itolewe tokea ukiwa mdogo ili ukifika ukubwani uilipe kwa hiari bila shuruti...
Sio kwamba watanzania ni wagumu kulipa Kodi hapana ugumu unakuja pale Kodi hizo zikitumiwa vibaya na viongozi kwa mfano leo hii haijulikan makao makuu ya nchi ni wapi dar au Dodoma rais na mawaziri wanapishana barabarani na angani Kama daladala (dar-dodoma),(dodoma-dar) gharama zote hizi zinakwenda kwa walala hoi ambao serikali imewapa jina la wanyonge.
Mtu anaye sisitiza ulipaji wa Kodi yeye halipi Kodi kuanzia rais,mawaziri , wabunge nk hivi unategemea nani atakuwa na moyo wa kulipa kwa hali hii mkuu?
Watu kuto wajibishwa Mara kadhaa ripoti ya CAG imekuwa ikiibua ufisadi na matumizi mabaya ya pesa za Umma mwisho mafisadi na wezi husimamishwa tu kazi au kubadilishwa kitengo mambo ya ukoo wa panya ndani ya CCM badala kupelekwa mahakamani kwa hali Nani atakuwa na moyo wa kulipa Kodi ambazo zinakwenda kwenye matumbo ya watu wachache.
Nani atakuwa na moyo wa kulipa Kodi ambazo zinakwenda kuwajengea watu nyumba za kifahari na kuwanunulia magari ya kifahari uku nchi ikiwa na matatizo kibao Kwenye maji,elimu,umeme,ajira nk.
Nani atakuwa na moyo wa kulipa Kodi ambazo zinakwenda kuhudumia mashirika yanayo jiendesha kwa hasara Kama ATCL.
Kwema Wakuu!
Kama nilivyoeleza kwenye heading hapo, suala la ulipaji Kodi Kwa sisi Watanzania ni kipengele. Watanzania wengi wetu Kama sio wote hatupendi kulipa Kodi.
Hata wanaolipa Kodi ni kutokana na hawana jinsi mazingira yanawabana tu.
Ila Kama wangeambiwa kwa hiyari yao nakuhakikishia watu wasingelipa kodi.
Watumishi wa Umma kama sio kukatwa juu kwa juu kwenye mishahara Yao na waajiriwa wa sekta binafsi zile kubwa, wangekuwa wanalipwa mikononi mwao kisha wao wenyewe ndio wakalipe Kodi, na kuhakikishia kodi isingelipwa.
Siku ya jana nilikuwa naongea na Mbunge mmoja ambaye ni rafiki yangu sana, akanichekesha mno. Nilipomgusia suala la kukatwa Kodi kwenye mishahara yao, alionyesha kukasirishwa Sana na mpango huo. Hataki kabisa Mshahara wake uguswe, yaani alikuwa mkali Kama mbogo ungedhani Mimi ndiye ninayemkata[emoji2][emoji2][emoji2].
Usishangae Rais halipi Kodi,
Usishangae Mawaziri na wabunge hawalipi Kodi,
Kodi kulipa Kwa Watanzania ni kipengele.
Hata hivyo nafahamu kuna indirect Tax ambazo watu hulipa Kodi, lakini hapa nazungumzia Direct Tax.
Maeneo niliyowahi kuishi, Wafanyabiashara wakisikia TRA au Manispaa wanakuja, utashindwa kushangaa, watu watafunga MADUKA, ofisi na kukaa pembeni wakijifanya sio wakazi wa eneo hilo[emoji2][emoji2][emoji2]
Haya ninayoyazungumza wote tunayajua, hakuna asiyejua kuwa Watanzania wengi ni mabingwa waliobobea Kwa kukimbia kulipa Kodi.
Wanaoomba joto ya jiwe ni Wafanyabiashara WA mjini, katikati ya Mji au jiji hawa mazingira hatawaruhusu kuwakimbia TRA Ila vinginevyo, wangekuwa nao wanakimbia tuu.
Kama Watanzania wengi tungekuwa tunapenda kulipa Kodi, nakuhakikishia nchi hii ingekuwa moja ya nchi zilizoendelea.
Kama Watanzania wengi tungekuwa tunapenda kulipa Kodi, nakuhakikishia Wafanyakazi WA TRA wangekuwa na maisha ya kawaida Sana, kwani mishahara yao sio mikubwa kihivyo lakini Rushwa ndio inawafanya watambe hapa mjini.
Ukitaka kuwabana Watanzania wengi yaani wengi walipe Kodi basi hakikisha unawabana kwenye Maeneo yanayotumiwa na wengi na walipe indirect way.
Kwa mfano, kwenye MIAMALA ya simu, vocha Kama serikali ilivyofanya,
Sema serikali iangalie kwenye Kodi zenyewe wazikatazo waweke walau nafuu sio haya makato nyonyaji,
Masuala ya Luku waongeze, Masuala ya Bill ya maji waongeze,
Lengo sio kuwakomoa Watanzania Bali kuwafanya walipe Kodi, maana Kwa njia ya kawaida serikali imethibitisha haiwezi kulipisha Watanzania Kodi.
Na Watanzania wengi tumethibitisha hatuwezi kulipa Kodi Kwa hiyari yetu pasipo nguvu.
Nawasilisha, mwenye hoja karibu, na wenye povu pia Ruksa
Taikon wa Fasihi
Ruaha, Iringa
Ni vyema ila wao wawe mfano pia, sio kupuyanga tu kisha wanataka sie ndio tulipishwe mikodi kandamizi😂😂😂
Wao wagongwe spana pia maana wana maisha ya kifahari sana! Wao wakishalipa kodi itatupa moyo na sisi
Duniani kote watu ni wagumu kulipa kodi. Hata enzi za Yesu suala la kodi ni mshikemshike. Sababu zipo nyingi lakini kubwa zaidi ni jinsi gani kodi inayokusanywa inavyotumika.
Kama unafikiri Watanzania ni wagumu zaidi ya mataifa mengine tafuta sababu za ziada za huo ugumu.
Hivi nikuulize, hapo Ruaha ulipo, kuna nyumba ngapi za kupangisha? Dar zipo ngapi? Hivi kwa nini mpaka sasa hakuna kodi ya wenye nyumba? Na ninaamini kama wangewekewa kodi, hakuna ambaye angelalamika. Ni kodi itatozwa kwenye mapato yao. Siyo hii ya miamala ambayo inatozwa kwenye huduma, siyo mapato.
Zipo kodi zinazoumiza. Na hii ya miamala ni mfano. Tayari kuna tozo, tunatozwa tozo juu ya tozo. Huku wanaacha fursa tele za kutoza kodi ambazo zisingeumiza watanzania. Hiyo ndiyo hoja. Kusema tu kwamba watanzania hawapendi kulipa kodi, hujawatendea haki. Hizo ni kauli za kibwanyenye.
Sababu kuu ni kutokana walipa Kodi directly ni wachache, hivyo lazima wachache waumie mno.
Ila Kama Kila mtu angelipa Kodi kulingana na Uchumi wake, Kodi ingepungua
Tatizo la kusoma na kutoelewa ni kubwa Tanzania. Je umeelewa nilichoandika? Kwangu mimi kodi ni muhimu sana kwani bila kodi basi hakuna nchi. Soma tena: nimesisitiza kodi itozwe na itumike vizuri ili watu watoe kwa wingi!!!SERIKALI ya Tanzania inaongozwa na Watanzania wachache waliopata bahati ya kuwa Viongozi.
Imagine wewe unakimbia Kodi sasa hivi na sio kiongozi, Inategemea ukiwa kiongozi utatoa Kodi?
Ndio maana mimi nasema ningekuwa govt siwezi kamwe kushusha tozo au kodi zozote kwenye jamii ya wakwepa kodi kama Tzn japo ndio asili ya Binadamu.
Tanzania tunakosa nini hadi tuanze kukamuana hiki ambacho hata hakikidhi Mahitaji? Kuendesha Serikali inamaana Utalii,Madini,Gas na Mengineyo alotujaalia ALLAH haviwezi kugeuka hela kwa Serikali?Kama Serikalini ni Wavivu wa kufanya kazi na kuvigeuza hivyo kuwa hela ya kununua Mafuta ya V8 huku nani boya sasaa.
Tatizo la kusoma na kutoelewa ni kubwa Tanzania. Je umeelewa nilichoandika? Kwangu mimi kodi ni muhimu sana kwani bila kodi basi hakuna nchi. Soma tena: nimesisitiza kodi itozwe na itumike vizuri ili watu watoe kwa wingi!!!