Mkuu inaonekana una grudges nyingi sana na CHADEMA sifahamu walikukosea nini.
Lakini ukiamua ku move on basi unayaacha yaliyopita otherwise ni ngumu kutuaminisha waliobaki sio wapinzani ilihali wanapigwa marisasi mara watekwe n.k yaani kwanini aumie hivo wakati akirudi CCM anapewa post nzuri?
Mie naamini katika wakati ambapo wapinzani wa kweli wanajionyesha hadharani ni sasa. Maana sio kwa hustle wanazopitia, so wanahitaji support kuliko kejeli zisizo za msingi.
Naomba unielewe vizuri, mimi ninaufahamu upinzani na najua kila mahala penye jumuia yeyote ile ambayo ina watu wengi lazima upinzani uwepo.
Lakini kuna makosa ya organisation yaliyopo upinzani hayawezi kutufikisha kule tunako kutaka tufike. Kuwepo kwa wapinzani wa kweli hakufanyi mnayo yapanga yakatokea, lazima pawepo na hatua za lazima na makusudi ambazo lazima zifuatwe ndio mtapata matokeo mnayoyataka.
1) Mmejipanga vipi kabla ya kwenda kufanya tukio? kupanga vizuri kwa unachotaka kukifanya unakuwa umekwisha tenda 40% ya tukio.
2)Usidharau ubora wa mshindani wako, ukidharau ubora wake unaweza ukatumia silaha hafifu kuliko unazotakiwa kuzitumia kushinda vita.
3) Wapiga kura ni Watanzania, na sio Chadema inawapiga kura wake na vituo vyake, ni pamoja na wapinzani wa Chadema ni wapiga kura wetu, woooote.
4) Kusimamia kila mnacho kifanya, tulipata matatizo kwa ujazaji form wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, jee tunashindwa kitu gani kuwahimiza wagombeaji waende kwa wanasheria tulio watayarishaa kuwasaidia kama chama na wagombeaji wengi wanauwezo wa kulipia hata kama 50,000/=.
5) Tunaingia uchaguzi bila kampeni materials, kwani tulikuwa hatujui uchaguzi utakuwa lini?
6) Jee tuliendesha hata semina kuwatayarisha wagombea kwenda kwenye uchaguzi huu, hasa wanaoingia kenye uchaguzi huu kwa mara ya kwanza?.
7) Kwa nini utafiti au ushauri hasa wa maandishi haufanyiwi kazi na unatolewa bure ?.
Hali yetu haikuwa nzuri hata 2015, lakini aibu ilifichika baada ya Mzee Lowasa kuokoa jahazi.
8) Kama chama chochote kile ukiona watu wenye ufahamu hawapewi nafasi au wanabezwa lazima ujiulize? kunani? Kila mwaka wa uchaguzi kundi linalo ondoka ni educated Elites kwa nini?
9) Tunaogopa ushindani ndani ya chama? siwezi kueleza sana hichi sio sahihi kuweka mengi wazi ni kipindi cha uchaguzi, lazima niwe na kaba ya roho, Chadema imekwisha pigika ndani na njee tukiendeleza kidogo tutakimaliza.
Na mapungufu yote yanaweza kufanyiwa kazi, Chadema lazima kihakikishwe kinabaki kwa kuweza kupigana vita nzuri na yenye ufundi 2025.