Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwarekodi video za utupu watu wawili wanaodaiwa kufumaniwa na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Singiba Buchadi (42) ambaye ni fundi umeme na mfanyabiashara Dephina Buchadi (42).
Kamanda Muliro amewataja wengine kuwa ni Doratea Mathayo (39), Wilbard Teobard (55), Albert Buchadi (30), Valenzi Silvester (40).
Amesema kuwa watuhumiwa hao wote ni wakazi wa Kongowe Wilaya ya Mkuranga.
“Vitendo vya kikatili walivyovifanya watuhumiwa hawa ni pamoja na kutoa adhabu wakati wao si mahakimu wala majaji, vitendo hivi havikubaliki kisheria katika nchi inayofuata mfumo wa utawala wa sheria na kwa sababu hizo watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo,”alisema Muliro.