Mbegu za kisasa ni ajenda ya kishetani na kiiluminati

Mbegu za kisasa ni ajenda ya kishetani na kiiluminati

Africa [emoji288] ni bala Giza sana
Unamkwepaje mzungu na wakati unatumia vitu ambavyo akitaka kukuua anatumia ivyo vitu
1. Dawa za HIV
2. Dawa za kifua kikuu
3. Dawa za kuzuia mimba
4. Dawa za malaria
5. Matumizi ya simu
6. Matumizi ya internet
7. Matumizi ya malipo
8. Matumizi ya kuku wa nyama
9. Matumizi ya kuku wa mayai
10. Matumizi ya vyakula vya makopo kutoka ulaya na Asia (Lactojen)
11. Dawa za kuzuia mimba isitoke kwa wamama wajawazito wenye matatizo ya kutoka kwa mimba
12. Madawa yote tunawategemea wao
13. Dawa za malaria


Apo unakuja na mawazo ya kipuuzi eti mbegu izo zinaua vizazi vya mbegu zetu, mkae mkijua awo wazungu wakija wanakutana na wataaramu wetu wa kukopi na kupest na wanapewa maelekezo jinsi ya kufanya.

Mzungu aepukikiki hata kidogo

Kila kitu unawategemea wao, mpaka misaaada ya Bajeti ya nchi, tunawategemea wao

Mzungu aepukikiki acheni mawazo ya kibange bangi.
Well said mkuu. Sisi tunawategemea wazungu. Je wao wanamtegemea nani?
 
Kwa hiyo mtu akufanyie research and development ya billions of dollars ili wewe uje uvune mazao kocho kocho bila gharama yoyote. Ingia deep kidogo utafute source ya motivation yao.You will be surprised.
Mkuu mbona unatumia gari, na ndege kwa usafiri badala ya miguu. Huwezi kukataa maendeleo ya sayansi na tekenolojia ya wazungu kwa kuhoji motivation behind. Mzungu mara zote anatumia akili ili kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii.

Sasa kama unadhani tatuzi za matatizo zina madhara haina budi uachane nazo.

Hata hivyo nashangaa baadhi ya watu kukataa pembe jeo za kilimo (GMO) kwa kukomenti hapa kwa kutumia smartphones za wazungu.

Kweli Africa tuna kazi
 
nakumbuka enzi zile mbegu za asili za mahindi kama kilima,kagili,ilonga na n.k!siku hiz hazipo kabisa!!!
 
Huwezi kuingia JF ukatoka mtupu. Moyo unauma kuona wakulima wetu hawajui madhara ya mbegu hizi. Hiv ikitokea siku mbegu asili zote zimetoweka na hawa mabwana wakagoma kutoa mbegu itakuaje? Si tutawasujudia? Kinachokera zaidi mbegu za GMO hazina ladha nzuri. Tunakulaga tu. Acheni mzaha jamani!!! Michele wa asili mtamu. Miaka ya nyuma ukipikwa wali mtaa mzima hoi kwa harufu maridhawa.
Mkuu siyo kwamba hawajui, ila hawajapewa taarifa, inaweza kuwa makusudi au kwa baht mbaya
 
Kwanza wewe mwenyewe ni mtu mzungu hapo kwahiyo usitake kutubadilishia mkanda hapa......tuache hivyo hivyo na conspiracy theory zetu.....

SONY Xperia Z5 Premium
Mkuu ukweli umeongea kitu safi kabisa watanzania wengi ni wajinga mno kitendo cha kuumiza kichwa kufikiria jambo anaona ni ujinga bora akaangalie bongo movie au wasafi festival ya kina diamond kijana kama huyo ambae pengine ana familia yake anaita hizo ni conspiracy ni jambo la kusikitisha sana na ndio maana mipango yao hawa wakuuu inafanikiwa sana kwa sababu ya watu wajinga wa hii aina na kwa mtindo huu tutakufa tu
 
Kweli tupu kabisa!

Bahati mbaya wanadamu ambao ndio walengwa wa hizo mbinu hizo, ndio wa kwanza kupinga, kubeza uchambuzi huu na badala yake kuzishangilia na kuzifurahia mbinu za kuwamaliza kama Haki za Wanawake, za Watoto, Chanjo, Mbegu za kisasa nk. Binadamu amefanywa kama broiler atalishwa kidogo na baadae kuchinjwa
 
Nakubaliana na wewe. Na hapa Tanzania kampuni zinazoleta hizi sumu hapa nchini ni pamoja na Syngenta, Bayer, Bolton na agent wao wapo na baadhi ya maprofesor wa vyuo vyetu vya kilimo nchini wanapokea kifunga mdomo wafumbie macho na kutokuishauri serikali vizuri.

Kwa kweli mbegu zao zote pamoja na mbolea kama Yara na mbegu zote za Dekalb zitokazo South Africa zinatakiwa zichunguzwe na kuhakikiwa na serikali. Takukuru ihusike. Tumsome Mwana harakati Vandana Shiva tutaipata Somo zuri.
 
Mimi huwa najiuliza kwa Nini mbegu za mazao zitokanazo na mazao ya mbegu zao hazioti? Yaani ukitaka kupanda lazima uende ukanunue mbegu zao..Inawezekana hata mazao ya mbegu zao ni ugonjwa mtupu, ndio maana vyakula vinaleta maradhi,,vimelea vya ushoga na kuharibu ardhi yetu.

Mimi huwa naiogopa Sana fate ya gmo maana ukiacha mazao hata wanyama nao wamewaharibu ng'ombe,,mbuzi, kuku.Unakuta maziwa tunakunywa ya kisasa , mayai ya kisasa, nyama ya kisasa na nafaka ndio usiseme.Sasa mutation iliofanyika kwenye Gene za hivyo vitu unakuta inahamia mpaka kwenye miili yetu.

Ndio maana tunashuhudia maajabu yasioelezeka.
 
Ukiachilia mbali kunyang’anywa aridhi, kuachilia mbali madhara mbegu hizi zinazotuachia kwenye miili yetu baada ya kutumia nafaka zake, mbegu hizi pia zinaweza kuifanya ardhi kuwa ni tasa katika uzalishaji kwa miaka 10. Na ikiwa kwa miaka 10 aridhi yako haitaweza kutoa kitu, jiulize mkulima atapatia wapi fedha za kuweza kulipa mikopo yake, hapo ndipo jamaa wanapokuja na kuichukua ardhi yako.

Nchi za Ulaya bado kwa kiasi kikubwa zinaitegemea Afrika kwa malighafi, tunajua walizibeba kwa wingi sana wakati wa ukoloni na hata baada ya uhuru waliendelea kufanya hivyo kwa kupitia viongozi ambao wengi walikuwa ni vibaraka wao, ambao waliwapatia nchi hizi baada ya uhuru, na wale ambao waliwapinga na kukataa kuwa vibaraka waliuwawa kwa namna mbalimbali, sote tunajua hili, walio bakizwa madarakani ni wale waliokubali kwenda sambamba na sera zao, na wao wakazifikisha nchi zetu hapa zilipo.

Hivyo nchi nyingi za Ulaya na Marekani si kwamba tu zinatizama bara hili la Afrika kama sehemu ya kuchota rasilimali mbalimbali, lakini pia kama shamba ambalo watakuja kupanda mazao yao mbalimbali na kuyasafirisha kwenda katika nchi zao. Ndiyo maana Green Revolution inafanya kazi nzuri ya kuwapokonya wakulima wadogowadogo aridhi zao.

Katika vita hivi vya kutunyang’anya aridhi zetu, Gate Foundation, nyuma ya Bill Gate anayetoa mabilioni ya dola zake huku akitabasamu ili aonekane ni malaika na binaadam mzuri kushinda wote mwenye moyo wa pekee katika kuisaidia Afrika, huyu ndiye askari mwenye bunduki iliyo jaa risasi za mbegu za kisasa kwa ajili ya kutuangamiza ili aweze kuchakua aridhi zetu juu ya miili yetu iliyo lala kwenye aridhi yetu ikiwa imekauka kwa njaa kutokana na aridhi yetu kufanywa tasa na risasi za mbegu za kisasa kutoka kwenye bunduki ya Bill Gate na wenzake.

Asilimia 55 ya aridhi yote Afrika leo hii haifai kwa kilimo baada ya kulimwa kwa miaka mingi aina moja ya mazao kwa ajili ya watu wa Ulaya na Marekani. Aridhi hiyo imekuwa ni tasa na Mwafrika bado anavaa suruali yenye viraka matakoni, wakati Bill Gate na wenzake wanatembelea ‘Private Jet’.

Wakati wa kuwa wabinafsi na aridhi zetu umefika. Sema hapana kwenye ‘Uchukuaji Huru’ wao wanaita uwekezaji, mpaka sera zake zibadilishwe.
Batanzanie waione hii
 
Mimi huwa najiuliza kwa Nini mbegu za mazao zitokanazo na mazao ya mbegu zao hazioti? Yaani ukitaka kupanda lazima uende ukanunue mbegu zao..Inawezekana hata mazao ya mbegu zao ni ugonjwa mtupu, ndio maana vyakula vinaleta maradhi,,vimelea vya ushoga na kuharibu ardhi yetu.

Mimi huwa naiogopa Sana fate ya gmo maana ukiacha mazao hata wanyama nao wamewaharibu ng'ombe,,mbuzi, kuku.Unakuta maziwa tunakunywa ya kisasa , mayai ya kisasa, nyama ya kisasa na nafaka ndio usiseme.Sasa mutation iliofanyika kwenye Gene za hivyo vitu unakuta inahamia mpaka kwenye miili yetu.

Ndio maana tunashuhudia maajabu yasioelezeka.

Baambie
 
Nakubaliana na wewe. Na hapa Tanzania kampuni zinazoleta hizi sumu hapa nchini ni pamoja na Syngenta, Bayer, Bolton na agent wao wapo na baadhi ya maprofesor wa vyuo vyetu vya kilimo nchini wanapokea kifunga mdomo wafumbie macho na kutokuishauri serikali vizuri.

Kwa kweli mbegu zao zote pamoja na mbolea kama Yara na mbegu zote za Dekalb zitokazo South Africa zinatakiwa zichunguzwe na kuhakikiwa na serikali. Takukuru ihusike. Tumsome Mwana harakati Vandana Shiva tutaipata Somo zuri.
Somo zuri sana
 
Watu wachache kabisa na wamiliki wa kampuni chache tu, lakini kampuni kubwa mno duniani, watu hao nyuma ya kampuni hizi wanafanya kila wawezalo usiku na mchana kumiliki kila punje ya mbegu iliyopo kwenye uso wa dunia.

Msukumo wa mbegu za kisasa dhidi ya zile za asili ni mkubwa mno katika dunia ya leo kupitia matangazo ya biashara na taasisi za kiserikali. Kiasi kwamba inaonekana tegemeo la dunia ijayo kwenye chakula lipo kwenye mbegu za kisasa pekee.

Hitajio la viwanda na uroho, ulafi wa watu wachache kutaka kumiliki uzalishaji wa mbegu zote duniani kupitia makampuni yao ya kimasonia. Ili kamapuni hizo kujihakikishia umiliki wa mbegu zote duniani ndipo walipo kuja na wazo la GMO (GENETIC MODIFIED seeds, crops, animals etc) Mbegu hizi za kisasa zinawazuia wakulima kuotesha mbegu zao wenyewe, kila msimu wa kilimo lazima ukanunue mbegu mpya.

Moja ya matatizo makubwa kwenye uso wa dunia ya leo ni njaa, ambayo imeenea katika kila kona ya dunia, na nchi ambazo zipo kwenye umasikini wa kutupwa pamoja na njaa kwa wananchi wake ndizo nchi zinazo ongoza kwa kusafirisha chakula nje ya mipaka yake.

GMO nazo siyo suluhisho kwenye tatizo ambalo tunalo, bali ni mafuta kwenye moto unao waka.

Dhana kuwa utapiamlo unasababishwa na vyakula ambavyo havina ‘ubora’ kutokana na kutumiwa kwa mbegu ambazo si za kisasa ni uwongo na ni siasa mbaya mno kuiingiza kwenye chakula, kwani sote tunajua kinacho sababisha utapiamlo ni kutopatikana kwa vyakula vyenye virutubisho mbalimbali kwa mlaji na hata kidogo siyo suala la kutokutumia mbegu za GMO.

Wanacho hitaji wakulima wetu siyo mbegu za GMO, bali ni aridhi ya rutuba na nguvu ya kiuchumi, ilikuweza kuifanya kazi yao katika ubora wa hali ya juu. Kuwagawia wakulima mbegu za GMO, hata kidogo zoezi hilo haliwezi kuwa ndiyo suluhisho la njaa duniani, wala mbegu hizo haziwezi kuilisha dunia, hivyo sababu hiyo haiwezi kutumika kama uchochoro wa kujinadi kuwa mbegu hizi zitawalisha watu masikini.

Kilimo hichi kinacho tegemea mbegu za GMO ni mfumo ambao unawanyonya wakulima wadogo na wakubwa na kujinenepesha wenyewe, kujilisha wenyewe badala ya mfumo kuwanenepesha wakulima wadogo na kuwalisha watu wa nchi zinazo endelea. Hii ni aina nyingine ya unyonyaji ambayo muda si mrefu wakulima wetu watajikuta ana kwa ana wakipambana na jinamizi hili kukomba aridhi zao.

Bill Gate anasema kuwa malengo makubwa ya Gate Foundation ni kupambana na njaa duniani kote, na silaha aliyoichagua kwenye vita hivyo siyo nyingine bali ni mbegu za GMO.

Mwaka 2010 GATE alinunua Share 500,000 kwenye kampuni ambayo inahusika na kutengeneza na kusambaza mbegu hizi za GMO kote duniani, na kwa kupitia ‘wanasayansi’ ambao tayari wapo kwenye mfuko wa suruali ya Gate, akatangaza kuwa ‘wanasayansi’ 900 wamethibitisha kuwa mbegu hizo zinafaa kupambana na baa la njaa kote duniani.

Lakini ukweli ni mwingine kabisa, mwaka 2008 wanasayani hao hao walitangaza kuwa mbegu hizo siyo suluhisho la tatizo la njaa duniani, na Bill Gate kama mdau mkubwa kwenye hilo alikuwa akifahamu ukweli huo, lakini waziwazi mwaka 2010 akaja na kauli tofauti ya wanasayansi hao na kuudanganya uma, kwa nini Bill?

Lakini si hivyo tu, Gate alishafahamu KUPITIA KWA WANASAYANSI HAO kuwa GMO zinayo madhara kwenye viungo vya mwili, viungo vya ndani ya mwili kama ini, figo na vingine, GMO zinayo madhara kiafya, lakini Gate akapigia kimya yote hayo.... na juu ya yote akasema uwongo na kuwasingizia wanasayansi 900 ... Duh.

Lakini tukija kwenye mazingira halisi, dunia ni tofauti kabisa. Maelfu ya wakulima WAMEJIUWA kutokana na gharama kubwa kupitiliza walizo shindwa kuzimudu kupitia kilimo cha mbegu za kisasa za GMO na ambazo zilishindwa pia kuzalisha kiwango cha mazao kilicho takiwa.

Kupitia World Bank na United Nations, wakatoa mafungu ya kutosha na kutengeneza taasisi waliyoiita International Assessment of Agricultural Knowledge, Science and Technology for Development (IAASTD). Taasisi hii ikawa ndani yake inajumuisha wanasayansi takribani 900, ambao walipewa jukumu zito la kusimamia na kutizama suala zima la njaa duniani na ni vipi litaweza kutokomezwa, ingawa kazi waliyo pewa ni nzito, hata kidogo majibu yao hayakuwa mazito katika kutoa suluhu ya janga lenyewe.

Juu ya yote majibu yao yakaja kugeuzwa kichwa chini miguu juu na bilionea Bill Gate.

Umoja wa Ulaya nao wamekuja na sheria nyingine yenye mkanganyiko, sheria hiyo inazikusanya mbegu zote za asili walizo nazo wakulima na kuwapatia mbegu mpya za viwandani, sheria hiyo inawataka ni lazima watumie mbegu za viwandani na siyo asilia. Suala hili liko wazi katika nchi zetu zinazoendelea, tumeambiwa kuwa ili bidhaa zetu ziwe na ubora na ili ziweze kushindana katika soko la kimataifa basi hatuna budi kutumia aina fulani ya mbegu, aina fulani ya dawa za kilimo na aina fulani ya mfumo wa kilimo, lakini vyote hivyo vimejaa sumu kuliko virutubisho, cha ajabu pamoja na kufuata maelekezo yote hayo bado ni sehemu ndogo tu ya bidhaa hizo tunayouza nje nyingine inabaki hapa, hapa tunaitumia wenyewe, Freemasons wanahakikisha tunajimaliza wenyewe kwa sumu walizo tupatia.

Oktoba 15, 2009, Bill Gates mwenyekiti mwenza wa Gates Foundation alitangaza mchango wa dola za Marekani milioni 120 katika kusaidia kile kinacho fahamika kama ‘Green Revolution in Africa’. Kitu hichi Green Revolution in Africa; kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere alivyo danganywa na Freemasons wa Asia na Ulaya na kuunga mkono sera za Ujamaa na Kujitegemea, ambazo zimeipatia taifa la Tanzania mpaka hivi leo kilema cha uchumi, vifo vya viwanda na kudumaa kwa sekta binafsi na kuwafanya wananchi wake kula ugali wa njano, sera ambazo Ethiopia iliishia kusababisha vifo visivyo na idadi kwa wananchi wake kutokana na njaa.

Leo hii Tanzania bado tukiwa na majeraha yale, yale ya uchumi, kidonda bado hakija kauka, viwanda bado havina matumaini ya kunyanyuka na sekta binafsi zikijaribu kujikongoja, watu wale, wale, Freemasons wakiwa na ajenda ile, ile lakini katika sura tofauti, wametuletea ‘Green Revolution for Africa’. Kwa sababu ya mizigo ya madeni tuliyo shindwa kuilipa na wananchi tukadanganywa kuwa eti madeni hayo yamesamehewa, nchi kama Tanzania na nyinginezo tunakuwa tayari tupo kwenye mazingira ambayo hatuwezi kukwepa chochote kinacholetwa na bwana hawa wakubwa.

Unamkumbuka ‘Economic Hit Man?’ Haya ndiyo madhara yake, Kwa hiyo leo kwa kupitia ‘Green Revolution,’ Tanzania tumepewa ‘Kilimo Kwanza’. Jina zuri eeeh, kama vile la ‘Ujamaa na Kujitegemea’ au siyo. Subirini muda tu punde tutaona mahali ambapo ‘Kilimo Kwanza’ kitakapo topelekea, ni kubaya zaidi kushinda pale tulipo achwa na ‘Sera za Ujamaa na Kujitegemea’.

Kumbuka sera hizi siyo za viongozi wetu. ‘Ujamaa na Kujitegemea’ hazikuwa sera za Mwalimu Nyerere, wala Azimio la Arusha hazikuwa sera zake, lakini kwa ajili ya kujifaragua kwa wananchi wake, akidhani ni sera bora zitakazo muimarisha kisiasa, alizifuta na kuzichukua kama za kwake.

Lakini ukweli ni kuwa sera hizo alimegewa na mabwana wakubwa wenye malengo tofauti na jina la sera zao. Sera za ‘Kilimo Kwanza’ siyo za Jakaya Kikwete, naye kapewa kama alivyo megewa Mwalimu Nyerere, lakini zote lengo la sera hizo ni moja, na mpishi wa sera hizo ni mmoja, Freemasons.

Green Revolution imeasisiwa na Gate Foundation mwaka 2006, kwa ajili ya kumbukumbu tu, Bill Gates ni Freemasons wa daraja la 33. Green Revolution ilitengenezwa kwa malengo ya kuhakikisha wakulima wadogo, wadogo wanapata mitaji ya kuwawezesha kujilisha wenyewe na watu wao. Unalionaje lengo hilo, zuri eeeh. Kwa sababu hapa Afrika inapata mitaji ambayo ilikuwa ikiihitaji kwa muda mrefu. Lakini kama zilivyo ajenda zote za hawa jamaa, lazima maneno mazuri hayo, au picha nzuri hiyo, nyuma yake, chini yake, kunayo jinamizi lilifichwa na sura nzuri za jamaa hawa.

Gate Foundation ni mpiganaji namba moja anaye hakikisha kuwa mbegu za kisasa, kutoka viwandani, mbegu zisizo za asili kabisa yaani ‘Genetically Modified Seed’ (GMS) zinapatikana dunia nzima, mbegu hizi zinayo madhara maradufu kuliko faida.

Gates wametajwa kutoa dola bilioni 1.4 kusaidia nchi masikini katika kilimo cha Green Revolution. Sura nyingine zilizomo katika mstari wa mbele wa kuhakikisha tunapata mbegu za kisasa, na misaada mbayo mbeleni itageuka ni kitanzi cha kutunyongea na kamba ya kutuburuta kokote wanapo pataka ni Rockefeller Foundation, Monsanto Foundation na Syngenta Foundation pamoja na serikali ya Norway. Unaonaje, sura ni zile, zile utakazo kuta kwenye sera ya uzazi wa mpango, ni zilezile utakazokuta kwenye haki za watoto, ni zilezile utakazozikuta kwenye haki za wanawake, haki za mashoga na kwengineko, jamani hatushtukii ndugu zangu wa kiafrikaaaaaa!!!!!

Inauma sana jamani.
Serikali ya Norway ni moja ya wachangiaji wakubwa katika kile kinacho fahamika kama Svalbard Global Seed Vault inayo patikana kwenye milima ya Icy, Norway.

Mradi huu ulikamika mnamo mwaka 2008, ambapo chini ya aridhi wamejenga ghala kubwa mno linalotumika kuhifadhia mbegu za kila aina ya nafaka na mimea. Wakulima na taasisi mbalimbali kote duniani wamekuwa wakishiriki katika kupeleka mbegu za asili katika hazina hiyo.

Eti wanasem pale ambapo mazingira yatabadilika na kusababisha madhara makubwa kwenye uoto wa asili basi mbegu hizo zitatufaa, mbona basi wasiziweke kwenye hazina hiyo hizo mbegu za kisasa kama kweli ni nzuri?

Dunia nzima itakapo kuwa inaegemea bidhaa hizi za viwandani, hasa hizi mbegu tunazo danganywa ni za kisasa, ambazo madhara yake ni makubwa zaidi, hawa mabwana wakubwa, watatumia mbegu za asili kwa faida yao wenyewe, hawa mabwana wakubwa watakapo zidi kuiharibu aridhi mpaka ishindwe kuzalisha tena mbegu za asili kwa namna yoyote wanayo fahamu, bado wao watakuwa salama, kwakuwa sehemu fulani kwenye uso wa dunia wana benki yao iliyo kusanya mbegu zote za asili kutoka duniani kote.

India mwaka 2008. Oktoba mpaka Disemba mwaka huo dunia ilishuhudia maelfu ya wakulima wa India wakijiua wenyewe . Ni baada ya kutumia mbegu hizi za bilgate na kilimo kikafeli mwisho wakanyang'anywa mashamba

Nitarudi kuendelea
kwa hisani ya salimmsangi
Kila nikisoma hili bandiko, nasema haya ni mafunuo ya kweli ya kiroho na yasiyo ya kibinadamu. Muda utaongea. Asante.
 
Back
Top Bottom