Mbele ya CHADEMA Kuna Uzima na Mauti, wapiga kura kazi kwenu

Mbele ya CHADEMA Kuna Uzima na Mauti, wapiga kura kazi kwenu

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
253
Reaction score
360
Ukiangalia mtifuano uliopo Katika Kinyang'anyiro Cha Uwenyekiti Taifa ndani ya Chama Kikuu Cha Upinzani CHADEMA, utagundua kwamba Kuna Uzima na Mauti kwenye hicho Chama.

Mauti ya Chadema iko hapa: Tuhuma za miaka yote kuihusu Chadema kama taasisi zimekuwa zikipuuzwa sana huku wanasiasa maarufu na wakutegemewa na Chama wakihama mara kwa mara na kutoa tuhuma zilezile.

Tuhuma hizo ndani ya Chadema ni pamoja na Ukanda, Ukabila, Matumizi yasiyokuwa ya wazi ya Fedha za Chama, Matumizi mabaya ya madaraka pamoja na Upendeleo wa Kikanda na Kikabila.

Kwa miaka mingi sana Chadema imekuwa ikisakamwa na tuhuma hizi huku wengine wakizielekeza Moja Kwa moja kwa Mwenyekiti Taifa Mh. Freeman Aikael Mbowe.

Na wengi waliokuwa wanajaribu kuleta mageuzi kwa kutaka mawazo mapya na misimamo mipya ikalie Nafasi ya juu kabisa ya Chama walikuwa na option mbili, wakae kimya au waondoke Chamani. Wengi tumewashuhudia waliondoka. Vitendo hivi vimekuwa vikileta maswali mengi sana kwa wanachama na wasio wananchama.

Uzima wa Chadema uko hapa: Kutokana na hayo yote, ili CHADEMA ijihuishe yaani ipate kuchangamka na kupata natumaini mapya na Safari yenye ari, Chaguo ni moja tu kwamba Mwenyekiti Mh. Freeman Mbowe anapaswa kuachia nafasi hiyo ya juu ili kufuta tuhuma zote hizo.

Lakini kama ataamua Kugombea na kulazimisha matokeo akashinda hicho ndicho Kitakuwa KIFO RASMI KWA CHADEMA. Tuhuma zote za miaka yote zitakuwa ZIMETHIBITISHWA/Confirmed kwamba ni Kweli.

Watakaobaki kwenye Chama ni wale wanufaika wa moja Kwa moja tu! Lakini sio wenye nia ya dhati ya kuja kuliongoza Taifa hili. Na hapo ndipo Watakuwa Wameturahisishia kazi sisi Wana CCM kuendelea kushika hatamu mpaka tutakapochoka wenyewe. Na Dua na Sala Zetu Wana CCM tunaomba apite Mh. Freeman Aikael Mbowe.

Uchaguzi huu wa CHADEMA ndio Utaamua CHADEMA iendelee kuwa hai au ife. Ama iendelee kuwa Chama Kikuu Cha Upinzani au iwe kama Chauma, TLP, PDP au Jahazi na vingine.
 
Back
Top Bottom