PreGE2025 Mbeto : INEC , ZEC Tume huru za Uchaguzi zenye uwazi na haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
9,722
Reaction score
15,117
Mbeto : INEC , ZEC Tume huru za Uchaguzi zenye uwazi na haki

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeutaka Upinzani kutozibeza Tume za Uchaguzi , INEC na ZEC na kudai si huru wakati Chadema na ACT Wazalendo , vimekuwa vikiongeza idadi vya Viti vya Udiwani ,Uwakilishi, Ubunge na kupata kura nyingi za urais .

CCM kimesema Tume hizo ziko huru na kutenda haki zikiongozwa na binadamu na kwamba Tume yoyote itakayoundwa kwa mfumo wowote , zitaendelea kuongozwa na binadamu si Malaika .

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zazibar Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis , aliyesema madai ya upinzani kuhusu Tume za Uchaguzi hayana mantiki , mashiko na kukosa nguvu ya hoja.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mbeto alisema grafu ya idadi ya Viti vilivyokwenda upinzani , kuanzia Mwaka 1995 hadi 2020, imekuwa ikipanda katika Uchaguzi za Serikali za Mitaa, Udiwani, Uwakilishi ,Ubunge na kuongezeka kura za Urais.

Alisema katika Uchaguzi Mkuu wa Kwanza Mwaka 1995 , NCCR-MAGEUZI na CUF , vilipata Viti kwa uchaguzi wa Tanzania Zanzibar , ambapo CCM mwaka huo ilipata Viti 24 na CUF 23 vya Ubunge na Uwakilishi.

"Nafikiri maana ya uwazi na demokrasia kwa upinzani hadi itangazwe CCM kimeshindwa kura za urais. Uchaguzi ni mchakato wa kukubalika kwa chama cha siasa na wananchi . CCM kina Mizizi mirefu , Nyenzo, Rasimali Fedha na watu kuliko Upinzani " Alisema Mbeto

Hivyo basi, Mwenezi huyo katika maelezo yake ,alisema, haiwezekani vyama vilichosajiliwa Mwaka 1993 na kuendelea , kama Chadema NCCR-MAGEUZI , CUF , ACT au CHAMA viwe na ubavu wa kukiangusha CCM .

"CCM ni jiti kubwa lenye Matawi mapana na Mizizi mirefu .Gogo na shina la mti wake halikatiki kirahisi . Kuchuana na CCM katika Uchaguzi kunahitajika upinzani wenye mbavu nene za kisiasa " Alisisitiza Mbeto

Aidha Katibu huyo Mwenezi akitoa mfano, alisema uchaguzi wa Mwaka 2015, Chadema kilipata Viti vya Ubunge maeneo ya Mijini na kukosa Vijijini , kutokana na uchanga wake kisiasa.

Mbeto alitaja kuna Wabunge wa Chadema wamekuwa bungeni kwa zaidi ya vipindi viwili ,ushindi wao umetangazwa na Tume ambazo leo wanaibeza na kudai si huru.

'Kina Tundu Lissu, John Heche, John Mnyika, Godbless Lema, Halima Mdee ,Ester Bulaya, Boniface Jackob ,Peter Msigwa, Said Kubenea na joseoh Mbilinyi wote wametangazwa washindi na Tume ya uchaguzu iliopo sasa " Alieleza Mwenezi huyo

Akizungumzia Katiba ya Tanzania na Zanzibar , Mbeto alisema Katiba hizo , zimeongoza nchi kwa miaka 61 bila misukosuko ya aina yoyote, kila katika wakati mgumu Katiba hizo zilitoa majibu na kuelekeza.

'Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliunda Tume iliokusanya maoni ya wananchi ilioongozwa na Joseph Warioba. Likaundwa Bunge Maalum la Katiba. Ilipoandikwa Katiba inayopendekezwa. Chadema na CUF wakawatoa wabunge wao kabla ya Bunge Maalum la katiba hakijafikia tamati " Alisema

Mbeto alieleza kuwa leo unapoisoma Katiba iliopendekezwa kwa utuo , utulivu na umakini, utaona ilivyozingatia changamoto na kutekeleza ushauri na maoni yaliotolewa na watanzania kwa ustadi na mazingatio .
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.

Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.

Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
 
Mbeto : INEC , ZEC Tume huru za Uchaguzi zenye uwazi na haki

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeutaka Upinzani kutozibeza Tume za Uchaguzi , INEC na ZEC na kudai si huru wakati Chadema na ACT Wazalendo , vimekuwa vikiongeza idadi vya Viti vya Udiwani ,Uwakilishi, Ubunge na kupata kura nyingi za urais .

CCM kimesema Tume hizo ziko huru na kutenda haki zikiongozwa na binadamu na kwamba Tume yoyote itakayoundwa kwa mfumo wowote , zitaendelea kuongozwa na binadamu si Malaika .

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zazibar Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis , aliyesema madai ya upinzani kuhusu Tume za Uchaguzi hayana mantiki , mashiko na kukosa nguvu ya hoja.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mbeto alisema grafu ya idadi ya Viti vilivyokwenda upinzani , kuanzia Mwaka 1995 hadi 2020, imekuwa ikipanda katika Uchaguzi za Serikali za Mitaa, Udiwani, Uwakilishi ,Ubunge na kuongezeka kura za Urais.

Alisema katika Uchaguzi Mkuu wa Kwanza Mwaka 1995 , NCCR-MAGEUZI na CUF , vilipata Viti kwa uchaguzi wa Tanzania Zanzibar , ambapo CCM mwaka huo ilipata Viti 24 na CUF 23 vya Ubunge na Uwakilishi.

"Nafikiri maana ya uwazi na demokrasia kwa upinzani hadi itangazwe CCM kimeshindwa kura za urais. Uchaguzi ni mchakato wa kukubalika kwa chama cha siasa na wananchi . CCM kina Mizizi mirefu , Nyenzo, Rasimali Fedha na watu kuliko Upinzani " Alisema Mbeto

Hivyo basi, Mwenezi huyo katika maelezo yake ,alisema, haiwezekani vyama vilichosajiliwa Mwaka 1993 na kuendelea , kama Chadema NCCR-MAGEUZI , CUF , ACT au CHAMA viwe na ubavu wa kukiangusha CCM .

"CCM ni jiti kubwa lenye Matawi mapana na Mizizi mirefu .Gogo na shina la mti wake halikatiki kirahisi . Kuchuana na CCM katika Uchaguzi kunahitajika upinzani wenye mbavu nene za kisiasa " Alisisitiza Mbeto

Aidha Katibu huyo Mwenezi akitoa mfano, alisema uchaguzi wa Mwaka 2015, Chadema kilipata Viti vya Ubunge maeneo ya Mijini na kukosa Vijijini , kutokana na uchanga wake kisiasa.

Mbeto alitaja kuna Wabunge wa Chadema wamekuwa bungeni kwa zaidi ya vipindi viwili ,ushindi wao umetangazwa na Tume ambazo leo wanaibeza na kudai si huru.

'Kina Tundu Lissu, John Heche, John Mnyika, Godbless Lema, Halima Mdee ,Ester Bulaya, Boniface Jackob ,Peter Msigwa, Said Kubenea na joseoh Mbilinyi wote wametangazwa washindi na Tume ya uchaguzu iliopo sasa " Alieleza Mwenezi huyo

Akizungumzia Katiba ya Tanzania na Zanzibar , Mbeto alisema Katiba hizo , zimeongoza nchi kwa miaka 61 bila misukosuko ya aina yoyote, kila katika wakati mgumu Katiba hizo zilitoa majibu na kuelekeza.

'Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliunda Tume iliokusanya maoni ya wananchi ilioongozwa na Joseph Warioba. Likaundwa Bunge Maalum la Katiba. Ilipoandikwa Katiba inayopendekezwa. Chadema na CUF wakawatoa wabunge wao kabla ya Bunge Maalum la katiba hakijafikia tamati " Alisema

Mbeto alieleza kuwa leo unapoisoma Katiba iliopendekezwa kwa utuo , utulivu na umakini, utaona ilivyozingatia changamoto na kutekeleza ushauri na maoni yaliotolewa na watanzania kwa ustadi na mazingatio .
La haulla! Wala hamuonagi haya! Mkt aunde tume ya kusimamia uchaguzi unaomhusu! Kwamba kw kua huko nyuma wapinzani walipata uwakilishi mkubwa uwe kigezo cha kuhalalisha kuendlea kw refa na ma linesmen alowachagua yeye wa mashindano yanayomhusu! What kinda thinking is this!! Naamini waTanganyika tumevuka kiwango hiki ktk kuchanganua mambo ...duh!
 
Back
Top Bottom