Mbeya: Askari wa JWTZ amuua Baba yake kikatili akimtuhumu ushirikina

Mbeya: Askari wa JWTZ amuua Baba yake kikatili akimtuhumu ushirikina

Poleni wafiwa. Hii inashangaza sana. Tumezoea kusikia haya ya imani za kichawi katika familia masikini na watu ambao hawakwenda shule. Hii familia inaonekana ilikwenda shule kwa kiasi cha kutosha tu! Au kukosa hofu ya Mungu?

Ukikosa hofu ya Mungu, unaweza chapisha makaratasi ya kura na kujipigia wewe nyumbani na kuzipeleka kwenye vituo vya kupigia kura chini ya ulinzi wa polisi!!
 
Kanda ya ziwa huko hamna madhara, nyie furaha pekee mliyochagua kuwa nayo duniani ni kusonga ugali mkubwa, mkipata ugali mkubwa tu hayo ni mafanikio makubwa sana kwenu Sasa kwenye vita ya ktafuta mafanikio/mali nani atawazungumzia vibaya?
Kaskazini inatafutwa pesa asee had nchi nzima Hadi mihimili ya nchi inashiriki kuweka chuki, maana ukiona huna adui ujue hauna mafanikio.
We jamaa umeongea upumbavu mtupu kwa akili yako unadhani kanda ya ziwa yote unawazidi kwa utajiri? Au unawalisha kiasi kwamba useme hawatafuti pesa,kitu ambacho wakaskasini wanapigwa na wengi ni ule utafutaji wa dhuluma kwa watu wengi wa kasikazini.
 
We jamaa umeongea upumbavu mtupu kwa akili yako unadhani kanda ya ziwa yote unawazidi kwa utajiri? Au unawalisha kiasi kwamba useme hawatafuti pesa,kitu ambacho wakaskasini wanapigwa na wengi ni ule utafutaji wa dhuluma kwa watu wengi wa kasikazini.
Kanda ya ziwa ndo kanda ambayo mara kwa mara inatoa mikoa na wilaya zinazoshika nafasi za juu juu kwa umasikini Tz japo dhahabu inapatikana huko kilicho kosekana ni akili ya maendeleo tu , akija mtu akipiga kampeni kwa kisukuma anajizolea kura za kutosha miaka nenda miaka Rudi huku umasikini ukiendelea kuwa wa kiwango Cha lami.

Mikoa ya shinyanga imefanywa kama shamba vile inavunwa dhahabu alafu inaachwa ikiwa imechakaa na wananchi hawashituki wala nini Yani.
Huwezi kulinganisha na kaskazini shughuli kubwa ni utalii na kilimo lakin miundombinu na maendeleo ya mtu mmoja mmoja ni makubwa
 
Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea mauaji ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Edward Ndonde anayedaiwa kuuawa kikatili kwa kuchomwa visu na mtoto wake, Mussa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT.

Mussa anadaiwa kufanya mauaji hayo leo Jumatano Januari 12, 2022 nyumbani kwa baba yake mtaa wa Lumbira Kata ya Iwambi jijini Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Christina Musyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa chanzo ni kutuhumiana kwa mambo ya kishirikina.

Amesema mtuhumiwa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT amekamatwa baada ya kufanya mauaji hayo na kwamba uchunguzi unaendelea ili hatua za kisheria ziweze kushika mkondo wake.

"Ni kweli tukio lipo na limetokea leo, ambapo pia marehemu alikuwa mwalimu msitaafu, chanzo kinadaiwa kuwa mambo ya kishirikina, ambapo mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu baba yake kuwa ni mchawi na Jeshi la Polisi limemshikiria kwa uchunguzi zaidi" amesema Christina.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Alhaji Saad Kusilawe amesema marehemu aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa ambapo alikitumikia kwa muda wote kwa uadirifu na kwamba wanasubiri maelekezo kwa ajili ya taratibu za mazishi.

"Tumepoteza hazina ya kiongozi, kwani katika utumishi wake aliweza kumaliza vyema hadi anastaafu, ni pigo kubwa na ni masikitiko makubwa" amesema Kusilawe.

Naye Balozi wa mtaa huo, Hezron Thobias amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alianza kutamka maneno kuwa amemaliza kazi yake aliyoitiwa na baba yake ya kuchinja kuku, jambo lililowashtua na kwenda kuangalia waliposikia kelele zikitoka ndani.

"Alionekana kama ana ugoro na amelewa, akawa anatamka maneno kuwa amemaliza kuchinja kuku, tukamuona mama yake analia anasema njooni muone mtoto alichofanya akiwa anatokwa machozi, ile tunaingia ndani tukakuta amemuua, damu zimemwagika" amesema Thobias.

Mwananchi imefika nyumbani kwa marehemu huyo na kukuta vilio na simanzi vikitawala huku majirani na waombolezaji wakiendelea na taratibu msiba.

Chanzo: Mwananchi, 12 January 2022
Atakua mchaga huyo,
 
Watoto na wazazi
Watt kipindi hiki wamevurugwa hofu ya mungu hakuna
Mambo hayaend mzz akizingua nae anamzingua
 
Juzi ilitokea kaskazini ikatafsiriwa kama tabia ya kabila fulani, Leo imetokea kwingine haya mambo hayafai kutafsiriwa kwa picha ya ukabila maana hasira,chuki,tamaa,ugomvi na wivu havina ukabila vinaweza kuwa katika moyo wa yeyote na ikasababisha madhara kama haya ya mauaji.
Uovu hauna kabila wala rangi ni wajinga wachache wenye chuki na makabila ya wengine Sasa na huyu wa mbeya naye ni mchaga?
Uhalifu na ushetani hauna kabila wala rangi
 
jamani kuna nini kati ya wazazi na watoto!!!!!
Malezi siku hizi ni balaa kabisa, mabinti wanachinja mama zao, vijana wanachinja baba zao wa kuwazaa kabisa, Kuna kitu hakiko sawa kabisa kwenye jamii. Unawezaje kuchinja mama au baba yako aliyekulea mpaka hapo ulipo.
 
Mimi naona ungeuliza swali hivi kuna nini kati ya vijana na hii serikali vijana kukosa ajira wamekua mbogo wana frustration za kutosha
Kukosa ajira sio justification ya mauaji maana hata huyu muuaji mbona ni mfanyakazi,.
 
Mimi naona ungeuliza swali hivi kuna nini kati ya vijana na hii serikali vijana kukosa ajira wamekua mbogo wana frustration za kutosha

sasa mzazi wako anahusikaje na hilo!!

msomi anajua kabisa serikali ndio tatizo,anaua mzazi wake.
 
Back
Top Bottom