Mbeya: Atuhumiwa kumuua mtoto wa kambo kwa kumpiga na kitu kizito kichwani kisha amtupa kwenye shimo

Mbeya: Atuhumiwa kumuua mtoto wa kambo kwa kumpiga na kitu kizito kichwani kisha amtupa kwenye shimo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ZAWADI SASTONI NZUNJE [30] Mkazi wa Igalako Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kambo aitwaye MESHAKI FAZILI MLAWA [12] Mkazi wa Kapyo kwa kumpiga kwa kitu kizito kichwani na kukimbia kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema "Awali Aprili 02, 2023, mtuhumiwa alitoweka nyumbani kwake akiwa na mtoto huyo kwenda naye kusikojulikana ambapo Aprili 04, 2023 ilifunguliwa kesi ya wizi wa mtoto katika kituo cha Polisi Igurusi. Kutokana na tukio hilo, tulianza msako mkali na Aprili 06, 2023 tulimkamata mtuhumiwa."

Amesema "Mtuhumiwa alikamatwa akiwa amejificha au kuomba hifadhi Msikitini na akiwa amevaa mavazi ya kanzu ili aonekane ni muumini mzuri."

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hili ni mgogoro kati ya mtuhumiwa na mke wake ambao ulipelekea chuki na hasira dhidi ya mtoto huyo ndipo mtuhumiwa akapanga kumuua mtoto huyo ili kumkomoa aliyekuwa mke wake. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.
 
Sheria ichukue mkondo wake. Adhabu kali itolewe endapo ni KWELI ametenda hilo.
 
Mwanaume mjingaaa, hivi visa vingi wanafanyaga KE...., Na yeye atolewe zawadi tuu kama vp.
 
Polisi wahakikizhs anajinyonga kituoni
 
siku hizi na Wanaume wanaitwa Zawadi ? anyway tuachane na hayo.

nilikua nataka kusema hivi:

KUOA MWANAMKE MWENYE MTOTO NI SAWA NA KUNUNUA SHAMBA LENYE MIGOGORO INATAKIWA UWE UMEJIPANGA HASA MAANA UNAOA MAMA WATOTO WA MTU SO USIDHANI NI KAZI RAHISI KAMA UNA ROHO NYEPESI UNAONDOKA NA UHAI WA MTU KABISA.

we uliona wapi mechi inaanza na 1 bila ?

karibu katika chama cha KATAA NDOA TANZANIA(KNT).

Tanzania bila ndoa inawezekana…
 
Watu wazima tukiwaambia wale wanaowasitiri single mama's kwa kuwapa zawadi ya utulivu kwa mara ya pili (NDOA) kwamba wahakikishe kwanza wanaonyeshwa vyeti vya vifo na yalipo makaburi ya wale waliowazalisha wanatuona hatuna akili.

Case kama hizi mara nyingi hutokea pale inapohisiwa kuwa na kinachoendelea nyuma ya pazia kati ya mama mtoto na mzazi mwenzake.
 
Back
Top Bottom