Mbeya: Auawa kwa kupigwa Risasi kisa kudai ushuru wa maegesho wa shilingi 7,500

Mbeya: Auawa kwa kupigwa Risasi kisa kudai ushuru wa maegesho wa shilingi 7,500

baada ya kumshinikiza alipe deni la Sh.7500 ya uegeshaji gari lake (Toyota Hilax)

wenye magari Tunaomba mtuambie taratibu za kulipa hii pesa ya maegesho ya Gari.
Tatizo kubwa lipo hapa kumshinikiza kulipa deni
Je ilo deni huwa linalipwa Wakati gani, na huwa linalipwa Cash, akiwa nyumban kwake anaweza kufanya Malipo ya deni kwenye Simu.
 
Mtu mmja aliyejulikana kwa jina la William Mgaya ambaye ni wakala wa kukusanya ushuru wa magari ameuawa kwa kupigwa risasi na mfanyabiashara wa madini kutoka Chunya.

Polisi wa Mbeya wanamshikilia mtuhumiwa kwa hatua zaidi za kisheria.

My Take
Serikali kuweni makini na kuwapa watu silaha, siyo kila mwenye vijisenti anafaa kupewa silaha.

----
Polisi mkoani Mbeya inamshikilia Ezekia Luhwesha (31) mchimbaji na mnunuzi wa madini mkazi wa Matundasi Chunya,kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi wakala wa maegesho ya magari William Mgaya (58) baada ya kumshinikiza alipe deni la Sh.7500 ya uegeshaji gari lake (Toyota Hilax)

Kama huna uwezo wa kuhudumia gari usilinunue.

Matajiri uchwara wamekuwa wanaingia kwenye mgogoro na ma agent wa serikali hasa traffic na Hawa wakusanya ushuru.

Mtu unamiliki gari la MILIONI 30, unashindwa kulipa faini au ushuru wa 10,000?
 
Kuna jamaa angu mbeya palepaale aliwai kupewa bastola Aina ya grock 17 kwa akili za Yule bwana ilinibidi kuama tu mji mnk akili za jamaa Yule nazifahamu vzr San na Mara nyingi tunakuwa nae kwenye upauwaji (ulevi ) haijapita Muda akanyanganywa kwa kosa la kutoa toa hadharani silaa hyo

Yule jamaa Ni maarufu snaa hapo mbeya mjini Ni muuzaji wa mabati ya dragon white snaaa HV
 
Kaa hivyo hivyo, akienda jela katika awamu hii niite mbwa nimekaa hapa
Kesi itaahirishwa kwa kutokamilika upelelezi wakati mpelelezi anamakizia nyumba yake, Kisha faili litapotea huku makatani nao wakipandisha nyumba zao. Baada ya mwaka, mwamba atapigwa faini ya laki Saba kwa uzembe. Mnakumbuka kesi vicent vs jamahiriyah kule Senegal.
 
Kama huna uwezo wa kuhudumia gari usilinunue.

Matajiri uchwara wamekuwa wanaingia kwenye mgogoro na ma agent wa serikali hasa traffic na Hawa wakusanya ushuru.

Mtu unamiliki gari la MILIONI 30, unashindwa kulipa faini au ushuru wa 10,000?
Mbeya Kuna unable wa kishamba Sana.
MTU akipanda daraja kutoka vilabu vya mchujo na msabe makunguru na kuanza kunywa konyagi anajiona amefika Sana.
 
Labda na umri wa kumilikisha watu silaha uangaliwe upya ila Ditopile alikuwa mtu mzima tu.
 
wenye magari Tunaomba mtuambie taratibu za kulipa hii pesa ya maegesho ya Gari.
Tatizo kubwa lipo hapa kumshinikiza kulipa deni
Je ilo deni huwa linalipwa Wakati gani, na huwa linalipwa Cash, akiwa nyumban kwake anaweza kufanya Malipo ya deni kwenye Simu.
Tatizo la hii system mpya ya parking unajikuta unaambiwa unadaiwa na machine,na hujui Nani alikumulika! Wangefanya hizi machine zao kila zinapokumulika,na wwe wakati huo huo upate msg kwa simu yako kua umemulikwa na parking system,hata Kama kuna Mtu umemuazima gari unakua unajua Kama ndiyo kaingiza deni la parking kwa gari yako! Lakini hii ya kumulikwa kimyakimya bado italeta mtafaruku sana Kati ya wenye Magari na watu wa parking!!
 
Unafikiri kesi ya mauaji unaimaliza kirahisi, hapo lazima atatumia sana
Hela ndiyo atoke atauza Mali zake pia
Hapo labda ajaribu kuigeuza manslaughter akimaliza hapo ndiyo
Afanya mpango wa kuchomoka

All in all huyo jamaa ni ndezi tu

Ova
Walio toa maelezo washaifanya kuwa manslaughter. Wameweka maneno ' kulikua na majibizano' atatokea shahidi mmoja mwenye njaa na aliyeahidiwa kitu na kusema, marehemu alikua anamkashifu mwamba na kumkejeli.
 
Back
Top Bottom