Mbeya: Auawa kwa kupigwa Risasi kisa kudai ushuru wa maegesho wa shilingi 7,500

Juzi nilikuwa nasafiri pale mwanza sehemu moja inaitwa busisi ....ikapita gari moja nikaiwahi kwa nyuma nikapiga bodi ili gari ili isimame , akashuka jamaa mmoja mrefu ana kipara ......akaanza kutamba pale..akauliza nani kapiga bodi! Nani kapiga bodi.......bodaboda wote waliokuwa pale kimyaaa, nikajitokeza mimi nikasema mimi ndie nimepiga bodi...jamaa akasema nitakupasua nikamuambia umpasue nani wewe mpumbavu wa magufuri...jamaa akachachamaa bodaboda ndio waliokuja kuamua.....kumbe mbwembwe zote zile jamaa anamiliki bastora😁
 
Na alivyo zumbukuku saa hizi atakuwa analia tu huko mahabusu. Tuwe na simile. Hata kama mtu kakujibu au kukuuliza bila adabu unapaswa kutulia kwanza kabla hamjajibizana mbovu. Mengine tujifunze kuudhiwa. Haung'oki ngozi. Ona sasa! Shida tupu!
Watu wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujifunza kama Lowasa.
 
Watu wa madini akili zao sio Sawa, kuua na kuuwawa ni kama mchezo hivi.
 
Jambo lipo hivi jamaa alikamatwa gari ikapigwa Chain si mnajua vihelehele via hawa jamaa then wakapeleka Gari yard kwao kule ndio jamaa akawaomba arudi kulipa baadae ndipo marehem akaenda Ku block gate na ndani ya Gari kulikuwa na mzigo wa dhahabu jamaa ndio katoka polini
 
Ukiwa na silaha unajisikia kama kupiga piga hivi silaha inakushawishi sana we uoni polisi wakiwa nazo smg kwenye lindo za bank uwa wanavyojiona..
... sijui al-Hamza aliwapatia vipi hadi kuwapora 2 mchana kweupe akiibukia baharini pale Ambassade de France! Al-Hamza chimbo lake lilikuwa huko huko Chunya; panatakiwa kumulikwa.
 
Huyu mfanya biashara lazima tu atakuwa ni Mwanaccm
.

Samahani lakini. Poleni wafiwa. Jamaa tayari katoa kafara.

Imeisha hiyo.
 
Kuna wenye bunduki wastaarabu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…