PreGE2025 Mbeya: Chifu Mwanshinga akemea mipango ya kuzuia uchaguzi 'No reforms No election' amuombea Rais Samia apate ushindi wa kishindo

PreGE2025 Mbeya: Chifu Mwanshinga akemea mipango ya kuzuia uchaguzi 'No reforms No election' amuombea Rais Samia apate ushindi wa kishindo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tujue ni maoni yake au anawakilisha wana Mbeya
Chifu kasema kweli na ni mtu mzima.
Tunamuunga mkono.
Vijana wajinga wajinga hawana lolote la kuonyesha kuleta maendeleo ila vurugu na maandamani mjini Mbeya.
Ukiwachunguza wengi wanaishi nyumba za tope.
 
Chifu wa Mkoa wa Mbeya, Rocketi Masoko Mwanshinga, amewataka wananchi wote wa mkoa huo kutumia haki yao ya kikatiba kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Chifu Mwanshinga amekemea vikali wale wote wanaotaka kuwazuia wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi, akisema Mungu atawapa usingizi na hawataweza kuzuia uchaguzi kufanyika.

Amesisitiza kuwa kila raia ana haki ya kupiga kura na kupigiwa kura bila hofu wala vizuizi vyovyote. Aidha, Chifu Mwanshinga amemuombea Rais Samia Suluhu Hassan apate ushindi wa kishindo, akisema kuwa uongozi wake umekuwa wa neema kwa Watanzania.

Amewataka wakazi wa Mbeya kuungana kwa mshikamano na kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kidemokrasia ili kuchagua viongozi watakaosukuma mbele maendeleo ya Tanzania.

View attachment 3278469
Chifu kaongea busara, hao wanaoishi nyumba za tope wanamatatizo makubwa.
 
Back
Top Bottom