Mbeya City yaitoa Azam FC kombe la Shirikisho la CRDB

Mbeya City yaitoa Azam FC kombe la Shirikisho la CRDB

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Huu kweli ni mwaka wa ubaya ubwela.

Azam ametolewa kwa penati na Mbeya City katika mashindano ya Shirikisho la CRDB Cup. Tukumbuke kwamba Mbeya City inacheza katika ligi daraja la kwanza.

Timu hizo zilimaliza mchezo kwa kufungana 1-1 ndiyo wakaenda kupigiana penati ambapo Mbeya City ikashinda kwa mikwaju 4-2.

Next, Coastal Union inaenda kuitoa Utopolo.
 
Unataka Yanga itolewe ili upate mpenyo?
 
Huwa nasema Bakhresa angefanikiwa zaidi na timu yake ya Azam kama angeipeleka sehemu kama Mbeya au Morogoro, maeneo yenye historia nzuri ya mpira halafu akatafuta mashabiki wafia timu.
 
Azam FC imeondolewa kwenye CRDB Bank Federation Cup baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City na kwenye mikwaju ya penati Azam wametolewa kwa penati 2-4.

Mbeya City inasonga mbele hatua ya 16 bora ya CRDB Bank Federation Cup.
IMG_3340.jpeg
 
Back
Top Bottom