Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

mkuu una uhakika kuwa Mbalizi ipo jiji la Mbeya?

Huwezi tenganisha Mbalizi na Mbeya hata kama zipo halmashauri tofauti. Mbeya inahudumiwa na uwanja wa ndege uliopo nje ya mainspaa.
 
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla in typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.


Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)


Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

Inaizidi mwanza
 
Mkuu umeielezea Mbeya kwa chuki zako binafsi za kutoipenda Mbeya.
Unaelezea kama vile Mbeya haina makazi bora.
Umewahi kufika forest mpya, forest ya zamani, Iwambi mpya, Isyesye mpya, Ituha, Block T, Itezi .....
Pia nieleze jiji lililopo Tanzania ambalo halina maeneo ya hivyo.
Acha chuki mkuu, Mbeya ni jiji zuri na itabaki kuwa hivyo.
 
Mi nimezaliwa huko ila siwezi kuishi huko kamwe mtanisamehe bakamu gwangu nkulonda i peace.
 
Mkuu umeielezea Mbeya kwa chuki zako binafsi za kutoipenda Mbeya.
Unaelezea kama vile Mbeya haina makazi bora.
Umewahi kufika forest mpya, forest ya zamani, Iwambi mpya, Isyesye mpya, Ituha, Block T, Itezi .....
Pia nieleze jiji lililopo Tanzania ambalo halina maeneo ya hivyo.
Acha chuki mkuu, Mbeya ni jiji zuri na itabaki kuwa hivyo.
Achana na wapuuzi hao,Mimi Huwa nawapa za uso tuu..

Pili Hawa wanapenda Mbeya ndio maana Wana washwa nayo.
 
Hakuna utaratibu wa maisha unaosema mji uwe na vumbi, mchafu, hauna ustaarabu, na miundombinu duni. Mimi kama mlipakodi Nina haki ya kuyasema haya ikiwa yananikera.
Utajua mwenyewe
Ndo jiji sasa na tunapapenda pazuri afu inaonekana upajui vizuri au una matatizo yakulinganisha sana
 
Utajua mwenyewe
Ndo jiji sasa na tunapapenda pazuri afu inaonekana upajui vizuri au una matatizo yakulinganisha sana
Na Kwa taarifa Yao hii kuwashwa washwa na Mbeya inathibitisha ukweli kwamba hakuna Mkoa mzuri kuliko sweet Mbeya Tanzania nzima
 
Mipangilio ya miji yetu mingi inareflect thinking capacity tuliyonayo wala sio vinginevyo. Na hii ni kwa Africa nzima I think wala sio kwa bahati mbaya.
Bora wewe umeona ni Afrika nzima wana ishambulia Mbeya tu yaani
 
Back
Top Bottom