Mbeya: Hakimu wa Mahakama ya Wilaya auawa kwa kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira kali

Naona imani za kishirikina ndio chanzo cha tatizo.
 
Kuna vijiji hawana macheko na hawatak madharau,sijui hata waliwezaje kujikusanya fasta hvyo na kufanya jambo.

Ila hicho kijiji watateseka mpaka wajute kuna nyumba zitabaki na wanawake tu
 
Juu ya kanisa katoliki au CCM kuchukua maamuzi ya kuua au ugomvi wa kuumizana ,nakataa kabisa. Kama ni wewe umepanga kufanya fujo kulisingizia kanisa au CCM na kuja kusema niliwaambia ,acha wazo hilo.
Umeona eenhh?!.Barikiwa sana mkuu.
 
Duh hii imetokea Kijiji cha Kibole, Kata ya Itete.. Halmshauri ya Wilaya ya Busokelo.

Nilimpigia Afisa Mtendaji wa Kijiji icho cha Kibole na kumpa pole kwa kilichotokea.

Kwakweli inashangaza sana Hakimu kutoheshimu maamuzi ya Mahakama.
 
Kutokana na simulizi ya tukio hao wananchi walikuwa kwenye self defence kwa sababu marehemu alishaanza kuwadhuru kwa silaha ya moto.

Reasonably silaha walizotumia wananchi ni kiwango cha chini dhidi ya marehemu.

Hakimu amepoteza maisha kwa ardhi inayoenda kummeza milele yote
 
Duh hii imetokea Kijiji cha Kibole, Kata ya Itete.. Halmshauri ya Wilaya ya Busokelo.

Nilimpigia Afisa Mtendaji wa Kijiji icho cha Kibole na kumpa pole kwa kilichotokea.

Kwakweli inashangaza sana Hakimu kutoheshimu maamuzi ya Mahakama.
Hapo ndipo utafakari usahihi wa hukumu wanazotoa mahakimu wetu dhidi ya wananchi wanaobambikiziwa hujumu uchumi
 
Ikiwa tayari hakimu alishawavunja wawili miguu huoni kama wananchi walikuwa wanajitetea na wameua bila kukusudia?
 
Hii nchi ina ardhi kubwa kwa nini ugombane na watu na mwishowe kuuwawa kizembe? Mimi natokea Kilimanjaro ambako ardhi ya familia nzima ni ekari 15 tuu na tuko zaidi ya 30. Nimeenda zangu Morogoro nimepata ardhi nzuri kwa kilimo, ufugaji na hata makazi, tena kwa bei ya kutupa kabisa na wenyeji wangu ni watu wakarimu sana. Yaani hata ukitaka ekari 100 unapata bila zengwe unaenda ofisi ya Kijiji mnaandikishiana, unalipa ushuru wa kijiji unapewa risiti maisha yanaenda.
 
Hawa wananchi, ukiondoa tukio la kumtoa roho Mhe hakimu, wsnajitambua kwa kitendo cha kufungua kesi huku wakijua jamaa ni hakimu na pengine angetumia nafasi yake kushawishi kesi ipindishwe. Pia nimpongeze hakimu aliyesimamia hiyo kesi kwa kusimamia haki bila kumpendelea hakimu mwenzake kama tunavyoona kwenye baadhi ya matukio ya Polisi,ambao wanapenda sana kulindana na kuonea watu.
 
Mkuu ni wapi huko na wanauzaje??
 
Yale yale ya Mabima na wananchi wenye hasira kali huko Mwanza.... vibastola vinawapa watu jeuri wakidhani wanaweza kutisha kila mtu. Haya sasa akazikwe na kabastola kake!
 

Mahakimu na majaji wafe tu maninaaa zao wanatumiaga sheria kama fimbo sana! Watu wengi wamefungwa kijinga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…