Mbeya: Hukumu kesi ya kupinga mkataba kuhitimisha mjadala wa DP World

Mbeya: Hukumu kesi ya kupinga mkataba kuhitimisha mjadala wa DP World

Ikiwa makundi mawili yenye mitazamo na hoja zinazokindhana kuhusu sakata Mkataba wa uwekezaji wa Bandari',Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya inatarajiwa kutoa uamuzi leo Agosti 7, 2023 ikiwa ni baada ya kukamilisha usikilizwaji wa hoja za pande zote katika kesi ya kupinga mkataba wa makubaliano ya uboreshaji na usimamizi wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA),

Usikilizwaji wa kesi hiyo ulihitimishwa kwa mawakili wa upande wa walalamikaji ambao walikamilisha kwa kuwasilisha hoja za ziada kujibu hoja za mawakili wa Serikali.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023, ambayo imefunguliwa na wanasheria wanne kataka Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya wakipinga makubaliano hayo kwa madai kuwa ni batili kwa kuwa yana ibara zenye masharti yanayokiuka sheria za nchi na Katiba.

Baada ya walalamikaji kufungua kesi, Serikali iliwasilisha pingamizi la awali ikitaka Mahakama hiyo isiisikilize kesi hiyo, huku ikibainisha hoja nne za kutaka Mahakama hiyo iitupilie mbali kesi hiyo bila kuwasikiliza wadai hao.

Baadhi ya wadau wanangojea uamuzi wa Mahakama katika swala hilo ambalo limekuwa gumzo kubwa katika jamii, hususani kwenye mitandao ya kijamii, amabapo imeshuhudiwa Chama cha Mapinduzi kupitia Katibu Mkuu, Daniel Chongolo na timu yake akiwepo Stiven Wasira wakieleza mambo kadha wa kadha kuhusu mkataba huo, katika mikutano hiyo wamekuwa wakihamasisha wananchi kuunga mkono mchakato huo.

Vilevile upande wa Chadema walizindua oparesheni "Okoa Bandari Zetu" Mkoani Kagera ambapo nao wamekuwa wakikosoa mkataba huo wakidai una mapungufu makubwa hali ambayo imekuwa ikiwafanya kuwahamasisha wananchi kutokubaliana na mkataba huo, pia wanaharakati wengine nao wameendelea kuwa na mitazamo kindhani juu ya suala hilo hali ambayo inakuza zaidi mjadala huo.

Mkindhano huo wa hoja unaweza kuwa unaongeza umakini zaidi na shauku kwa wadau pamoja na wananchi kufuatilia kwa ukaribu zaidi uamuzi wa Mahakama ambao unatarajiwa leo
 
Leo, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya inatarajiwa kutoa Uamuzi/Hukumu yake juu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wanaharakati wanaohoji uhalali wa Mkataba wa Ukodishwaji wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World.

Kuanzia Makao Makuu ya CCM Dodoma na Ofisi zake zote mikoani, CCM imeelekeza macho na masikio yake Mbeya. Amini nawaambia, kadiri ya mipango isiyo na viwango iliyopangwa na chama hiki tawala, Hukumu ya kesi ya Mbeya imebaki kama tumaini la mwisho kuhusiana na mkataba wa DP World.

CCM imepanga (huku ikiamini kuwa kesi hiyo itashindwa) kutumia Hukumu hiyo ya Mbeya kuwanyamazisha watanzania na kuishauri Serikali kuendelea na utekelezaji wa mkataba huo tata wa DP World. Nyaraka za madokezo ya kichama nilizoziona zinaonesha kuwa CCM inaisubiri kwa hamu hukumu ya leo.

Mipango hiyo ya CCM inaonesha kuwa Hukumu ya Mbeya itatumika kama fimbo na kizibo cha kuwachapa na kuwaziba wakosoaji wa mkataba huo wa DP World. Kwa maana nyingine, CCM inaamini kuwa suala la DP World linahitimishwa leo kupitia Hukumu ya Makahama Kuu ya Mbeya.

Nakitahadharisha na kukiambia chama changu, Hukumu ya Mbeya haitahitimisha jambo hili kwa wanaharakati kushinda au kushindwa kwenye kesi hiyo. Mwisho wa ukosoaji wa mkataba wa DP World ni kwa Serikali kuachana na mkataba huo tata kwakuwa watanzania wameukataa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
CCM imepanga (huku ikiamini kuwa kesi hiyo itashindwa) kutumia Hukumu hiyo ya Mbeya kuwanyamazisha watanzania na kuishauri Serikali kuendelea na utekelezaji wa mkataba huo tata wa DP World. Nyaraka za madokezo ya kichama nilizoziona zinaonesha kuwa CCM inaisubiri kwa hamu hukumu ya leo.[emoji848][emoji3064][emoji848][emoji3064]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya inatarajiwa kutoa Uamuzi/Hukumu yake juu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wanaharakati wanaohoji uhalali wa Mkataba wa Ukodishwaji wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai kupitia kampuni ya DP World.

Kuanzia Makao Makuu ya CCM Dodoma na Ofisi zake zote mikoani, CCM imeelekeza macho na masikio yake Mbeya. Amini nawaambia, kadiri ya mipango isiyo na viwango iliyopangwa na chama hiki tawala, Hukumu ya kesi ya Mbeya imebaki kama tumaini la mwisho kuhusiana na mkataba wa DP World.

CCM imepanga (huku ikiamini kuwa kesi hiyo itashindwa) kutumia Hukumu hiyo ya Mbeya kuwanyamazisha watanzania na kuishauri Serikali kuendelea na utekelezaji wa mkataba huo tata wa DP World. Nyaraka za madokezo ya kichama nilizoziona zinaonesha kuwa CCM inaisubiri kwa hamu hukumu ya leo.

Mipango hiyo ya CCM inaonesha kuwa Hukumu ya Mbeya itatumika kama fimbo na kizibo cha kuwachapa na kuwaziba wakosoaji wa mkataba huo wa DP World. Kwa maana nyingine, CCM inaamini kuwa suala la DP World linahitimishwa leo kupitia Hukumu ya Makahama Kuu ya Mbeya.

Nakitahadharisha na kukiambia chama changu, Hukumu ya Mbeya haitahitimisha jambo hili kwa wanaharakati kushinda au kushindwa kwenye kesi hiyo. Mwisho wa ukosoaji wa mkataba wa DP World ni kwa Serikali kuachana na mkataba huo tata kwakuwa watanzania wameukataa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
CCM hawajawahi kushindwa kesi kama hizi. Wote tunajua matokeo na Mwambukusi walishajua hayo kabla ya kesi. Ila hiyo hukumu litazidi kuthibitisha kile alichokisema Rostam kuhusu mahakama zetu.
 
Siku ya Historia! Kama Muhinili utakubali kujiabiasha au lah
Issue ya bandari ni kubwa, tusichukulie kawaida.

CCCM yenyewe yaweza kukubali kushindwa kupitia mahakama Ili kuficha Aibu ya kiongozi wake kusaini mkataba wa kimangungo.
 
Screenshot_2023-08-07-09-56-26-1.jpg

Taarifa hii ikufikie popote ulipo kwamba , leo 7/8/2023 yaweza kuwa siku muhimu sana miongoni mwa masiku yote ya mwaka huu Nchi Tanzania , Hii ni kwa sababu kuna jambo muhimu sana laweza kutokea kwenye Mahakama kuu Kanda ya Mbeya .

Jopo la Majaji wakiongozwa na Mh Dunstan Nduguru watatoa maamuzi kuhusu kesi ya Mkataba Mbovu wa Bandari iliyopelekwa mahakamani hapo na Wazalendo wakiongozwa na Wakili Msomi Mwabukusi .

Usiondoke JF
 
Back
Top Bottom