Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, Jeshi la Polisi linawataka wananchi, wagombea na wafuasi wa vyama vya siasa kutii sheria bila shuruti ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na jitihada za kuzuia na kudhibiti makosa mbalimbali ya barabarani ikiwemo utoaji wa elimu kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara, ukaguzi wa vyombo vya moto pamoja na ukamataji wa makosa ya usalama barabarani.
Kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2024 jumla ya makosa 6921 ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani yalikamatwa kati yake magari yalikuwa 5618 na Bajaji/Pikipiki zilikuwa 1303.
Vile vile, katika kipindi hicho jumla ya magari 5618 yalikaguliwa ambapo magari 104 yaligundulika kuwa na changamoto mbalimbali za kiufundi na kuwataka wamiliki na madereva kurekebisha kasoro hizo ndipo yaingie barabarani.
Sambamba na hayo, katika harakati za kuzuia na kudhibiti matukio ya ajali za barabarani mkoani Mbeya, kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2024 jumla ya madereva 03 walifungiwa leseni zao za udereva kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani ikiwemo kuendesha gari kwa mwendo kasi, kuyapita magari mengine katika maeneo hatarishi na kusababisha ajali.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa madereva kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali kwani kitendo chochote cha ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani hakitavumilika, hatua za kisheria ikiwemo kuwafungiwa leseni madereva na kuwafikisha mahakamani kwa uzembe na kutokutii sheria zitachukuliwa.
Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.