Unafahamu kusoma na kuelewa vizuri? Wapi kwenye hiyo sheria wamesema unahitaji kibali cha Polisi?
Kama huelewi vizuri Kiingereza ni kwamba, kifungu hicho kinasema kuwa kwa mtu anayekusudia kuandaa kusanyiko la hadhara, atatoa taarifa polisi.
Kama mimi naenda sehemu, nikafika hapo nikawakuta watu wamejazana kunisalimia au njiani wakanisimamisha kunisalimia au kunishangilia, mimi ndiyo nimeandaa hilo kusanyiko? Anayetakiwa kutoa taarifa ni aliyeandaa kusanyiko la hadhara. Na usiishie hapo tu bali unatakiwa ufahamu pia kwa tafsiri ya kisheria, nini maana ya kusanyiko la hadhara kwa kadiri sheria ilivyokusudia.
Ukienda sokoni kila siku utawakuta watu wamekusanyika, ukienda makanisani watu wamekusanyika, ukienda kwenye misiba watu wamekusanyika, ukienda stand watu wamekusanyika, ndani ya ndege au basi watu wamekusanyika - je, hao wote wanatakiwa kutoa taarifa polisi?
Tusiitumie sheria kama watu wenye uwendawazimu bali kwa kuzingatia kusudio la sheria pia.
Sent using
Jamii Forums mobile app