Mbeya: Mahakama imeahirisha kusoma hukumu ya Mdude Nyagali hadi Juni 28, 2021

Mungu wa Mbinguni ikiwa uliweza kumtoa Petro katikati ya gereza tena chumba Cha ndani Kama maandiko yesamavyo, na ikiwa ulimponya Daniel na Simba wenye njaa Kali ukawafunga vichwa vyao, na pale alipokuomba Joshua jua lisimame na ukafanya hivyo.

Naamini hujabadilika kamwe wewe na mwanzo tena mwisho, asubuhi ya leo najitakaza kwa ajili ya Taifa langu Tanzania, najitakasa kwa ajili ya Rais wangu Samia Suluhu Hassani

Natubu kwa ajili ya jaji Mkuu wa Tanzania, natubu kwa ajili ya majaji wa mahakama kuu ya Mbeya pamoja na jaji atakaehukumu kesi ya mtumwa wako Mdude, Natubu pia kwa ajili ya Mdude.

Najua kila mwanadamu ana mapungu yake na kamwe anakuudhi na kukukosea, inuka eeh Bwana kwenye kiti Cha enzi geuza uso wako ukamwangalie mtoto wako Mdude Leo hii mahakani, simama Mungu wa Ibrahimu, Isack na Yakobo tazama wanao wote waliokusanyika mahamani wakisuburi hukumu watie nguvu wape uvumilivu na huruma pia wape, kafanye Jambo ambalo litaacha midomo ya watu ikiwa wazi ukimtetea waziwazi mtumushi wako Mdude.

Kwa jina la Yesu Kristo wanazareti Naomba nikiamini hivyo ameeni
 
Amen
 
Hukumu imeahirishwa hadi 28/06/2021
 
Amen Amen Amen Mungu atatenda kwa wakati na muda sahihi.
 
Kesi inaendelea muda huu bado nasisitiza hatutaki mambo ya Rais kupigiwa simu katikati ya kesi ikiendelea

Kama ilivyofanyika kwenye kesi ya Akwilina

Tunataka mdude aachiwe huru haraka sana sio kwa maelekezo ya mtu yeyote maana hana kesi ya kujibu
Imeahirishwa baada ya kuona mtiti wa watu nje, Shensi
 
Ongeza na Mungu aliyemwokoa TL na yale marisasi!
 
Zama zile jiwe ashatoa hukumu zamani bashite akiandika kwa kiingereza chake,huku hakimu akiona ndo fursa ya kumridhisha jiwe Ili kesho apate uteuzi wa ujaji.Wapo walioteuliwa ujaji baada ya kuwaumiza wapinzani kwa kuwafunga na kuwanyima Dhamana.
 




=========

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imeahirisha kusoma hukumu ya kesi ya kada wa Chadema, Mdude Nyangali iliyokuwa itolewe leo Jumatatu Juni 14, 2021.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Zawadi Laizer amesema ameiahirisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake na kubainisha kuwa hukumu hiyo itasomwa Juni 28, 2021.

Mdude anakabiliwa na shtaka la kusafirisha heroin gramu 23.4 mwaka 2020.

Akizungumza nje ya mahakama mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu mpaka tarehe iliyopangwa.


PIA, SOMA: Hukumu ya Mdude Nyagali ni leo 14|06|2021
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…