JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Katika hali isiyo ya kawaida Mzee Isaac Mwasilu amesema Bora arudi nyumbani na kwenda kufa kama itashindikana kusaidiwa kupatikana kwa mtoto wake aliyepotea tangu tarehe 11/11 mwaka 2021, kwa madai kwamba alichukuliwa kama Mateka na askari wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya aliyedai atampoteza mnamo tarehe 10/11/2021.
Akiomba msaada Mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema amehangaika juu ya kupatikana kwa mwanae kwa viongozi mbalimbali Mkoani Mbeya, lakini hakuna msaada aliopata na hadi Sasa hajulini kua mwanaye yupo hai au alifariki Dunia.
Baada ya kumsikikiza Mzee huyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wasaidizi wake kutoka ofisi yake kushughulikia suala hilo Ili kupatiwa ufumbuzi.