Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Leo Juni 28, 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuachia huru Mdude Nyagali baada ya kutomkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kusafirisha madawa ya kulevya.

Mpaluka Mdude Nyagali alikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 23.4 mwaka 2020.

Mdude ni Mwanaharakati na Mwanachama wa CHADEMA ambaye alitumia muda mwingi kuikosoa Serikali ya Awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati John Magufuli. Mdude anajitambulisha kama mpiganiaji uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuwepo mdahalo wa kisiasa.

Pia soma
- Mbeya: Mpaluka Nyagali Mdude akamatwa na Heroine, apandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya Uhujumu Uchumi



Nyagali.jpg

1624874090695.png
 
Natoa wito huu kwa Serikali ya awamu ya 6, kwamba wote walioshiriki kumtesa Mdude ambao bila shaka wanafahamika , wakamatwe haraka sana na kushitakiwa Mahakamani

Ni muhimu sana kwa Chalamila na kundi lake akiwemo RPC wa Songwe na RPC wa Mbeya , DPP aliyeng'olewa Biswalo Mganga (mnyororo ni mrefu) wakamatwe na kushitakiwa ili kuimarisha utawala wa sheria nchini Tanzania, ni muhimu watu hawa kukamatwa ili kuepusha wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa lengo la kulipa kisasi.
 
Natoa wito huu kwa Serikali ya awamu ya 6 , kwamba wote walioshiriki kumtesa Mdude ambao bila shaka wanafahamika , wakamatwe haraka sana na kushitakiwa Mahakamani
UTASUBIRI SANA muh8ini yule kishashika adabu mwambie aende akashitaki sasa kama atakukubalia sasahivi kila mtu hata mtoto atamuamkia mpuuzi yule
 
Back
Top Bottom