Mbeya: Mhandisi aswekwa ndani kwa kutafuna Bilioni tatu za mradi wa maji. Adai kujenga Kibanda cha mabati cha 'site' kwa Milioni 100

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameamuru Jeshi la Polisi kumkamata na kumuweka mahabusu Mhandisi Alistides Kanyomo wa kampuni ya Mbesso Construction kutoka Jijini Dar es Salaam

Kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Ujenzi wa mradi wa Maji Katika Bonde la Mwakaleli wilayani Rungwe na kusababisha wananchi katika vijiji 18 vya Halmashauri za Busokelo na Rungwe kukosa Maji kwa kipindi cha miaka 11.

Prof.Makame amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea kibanda cha ofisi ya muda ya kampuni hiyo ambacho kimejengwa kwa mabati na kudaiwa kuwa Ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 100

Your browser is not able to display this video.

 
Wataifishe mitambo yake kufidia huo uhujumu uchumi/ubadhirifu alioufanya
 
Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameamuru Jeshi la Polisi kumkamata na kumuweka mahabusu Mhandisi Alistides Kanyomo wa kampuni ya Mbesso Construction kutoka Jijini Dar es Salaam
Kumbe mafisadi hawajaisha?!
 
Tumesema mara nyingi.

Hivi watendaji na wasimamizi ws wizara wako wapi?

Inabidi Mbarawa aje ndo madudu yajulikane?

Si usanii huu?
 
Hii dingi mhandisi hadi yenyewe ilikuwa inaona aibu kutamka gharama za banda πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huyo jamaa afungwe miaka 30 na kila siku wanakijiji kumi wanakuja kumchapa bakora 2 kila mmoja kipindi chote cha kifungo chake.
 
Nakulilia Tanzania, unajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye choyo.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…