Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi

Sijaona tatizo la huu wimbo. Sijaona uchochezi wowote hapo...

Kila kilichowasilishwa kupitia sanaa ya uimbaji ndani ya wimbo huu ni kweli na yapo na Kila mtu ni shuhuda wakiwemo haohao polisi..

Kwa mfano;

√ Je, si kweli kuwa wamasai huko Ngorongoro Loliondo wanalazimishwa kuhamia Handeni - Tanga kwa nguvu na wengi wanaokataa wanapigwa, kuteswa, kutungwa na kuuwawa?

√ Je, si kweli kuwa umeme unakatika katika hovyo na kusababisha kero kubwa kote nchini huku kazi za wananchi zinazotumia umeme kusimama na kusababisha hasara kubwa?

√ Je, si kweli kuwa Kila anayekosoa serikali kwa lugha kali ya kukemea mara zote anaitwa mchochezi?

√ Je, si kweli kuwa Mch Mbarikiwa Mwakipesile polisi wameua mtoto wake Kwa maagizo ya mkuu wa TISS na RSO wa Mbeya na hakuna hatua zilizochukuliwa Kwa wahusika wa mauaji?

√ Je, si kweli kuwa nishati ya mafuta imepanda bei kuliko kawaida na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha kwa sababu ya kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali na serikali haichukui hatua yoyote ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi?

√ Je, si kweli kuwa Tundu Lissu alipigwa risasi mchana kweupe ktk maeneo ya kuishi viongozi serikali Area D Dodoma yenye ulinzi masaa 24 na mpka sasa polisi hawataki kukamata wahalifu hawa?

##Kama haya yanayokea na huku tukiwa na serikali lakini haichukui hatua yoyote kwa nini watu wasiseme labda viongozi wa serikali wenye dhamana na mamlaka ku - regulate mambo wanatuona sisi wananchi na manyani (wanyama) wasio na thamani yoyote?

## Ni kosa kubwa sana kumkamata na kumweka ndani binti aliyeimba wimbo huu badala ya serikali kutoka na kusema, hapana serikali haiwaoni wananchi kama manyani (wanyama) kwa sababu katika hayo serikali inachukua hatua 1, 2, 3 na kuendelea..??

We demand the police to release that lady immediately without any conditions ni Jesus Christ's name..!!!

Na kwa nini polisi mlimuua mtoto wa mchungaji? Alikosa nini hataastahili kuuwawa? Huyo mchungaji anazusha mambo na kusingizia polisi siyo? Kama anazusha, hatua Gani zimechukiliwa na Tanpol kwa kusema uongo dhidi ya polisi???

Serikali hakika mmegusa pabaya!!
 
Unaunga mkono uuzwaji holela wa nchi?
 
Akili yake ni njema kabisa....

Mtawala hukoselewa kwa STAHA....

Kubwa hushauriwa.....

Huwezi kushindana na dola kupitia njia hizo....huo ni ubwege[emoji1787]
'Ubwege' ni huu wako na huyo kilaza mwenzio mnaoabudu dola.

Hivi mnajua dola ni kitu gani?
Dola siyo mali inayomilikiwa na wapumbavu.
 
Serikali mbovu, Rais Mbovu hasaa. Walitaka aimbe nini?
 
Mashairi yaliyopo kwenye wimbo wa Sifa Bujune, uitwao Mnatuona Nyani tu ni haya.

"BANDARI hatarini wananchi tukilia hatusikilizwi, hii ni kwasababu, Mnatuona Nyani tu.

Ngorongoro ndugu zetu wanaamishwa kwa nguvu, hii ni kwasababu Mnatuona Nyani tu.

Inamaana hao Wageni wanathamani kwenye nchi kuliko wenyeji, hii kwasababu, Mnatuona Nyani tu.

Masai ndugu zetu wamelia kila kilio lakini hawasikilizwi, Mnatuona Nyani tu.

Kijana mdogo kango'lewa meno na maaskari, hii ni kwasababu Mnatuona Nyani tu.

Imefika wakati Tanzania Kila anaepinga DHULMA, anaitwa mkaidi, anaharibu amani ya nchi mara mchochezi, Mnatuona Nyani tu.

Mbarikiwa Mwakipesile amelalamika mtoto ameuwa lakini mmepuuza, Mnatuona Nyani tu.

Amepiga kelele mmempa na kesi, Mnatuona Nyani tu.

Kwa mujibu wa Katiba viongozi ni wawakirishi wa wananchi lakini tunalia kero zetu hazisikilizwi hii ni kwanini? Mnatuona Nyani tu.

"Bidhaa zipo juu Maisha ni magumu kila kitu kimepanda, Mnatuona Nyani tu.

Maisha ni magumu Kodi zipo juu ni kwanini? Mnatuona Nyani tu.

Sikuhuzi umeme kukatika imekua kawaida, Mnatuona Nyani tu

Kazi zinasimama kwa umeme kukatika mbona ni hasara, Mnatuona Nyani tu.

❤️🇹🇿

Naona kwa mbali Wananchi wameanza kuamka kutoka usingizi wa pono. Ni wakati muafaka kwa watawala wetu kujitafakari. Haya mambo yao ya kuendelea kufanya vitu kwa mazoea, kuna siku yatakuja kuwatokea puani.
 
Nachelea sana kuamini kama kweli wewe ni kiongozi wa kiroho
 
Kama wazungu na waarabu wangekuwa na akili kama hii, basi maendeleo waliyonayo wangeyasikia kwenye chupa.

Unaijua "Arab spring movement" unaijua faida yake?
Unaijua faida waliyopata USA baada ya kupinga sera za wahamiaji za Trump?

Unadhani wangekuwa wanalialia tuu na kumwachia Mungu, unadhani wangefika walipo fika?

#YNWA

#YNWA
 
Sifa Boniventure Bujune wewe ni jembe. Ugombee ubunge, Urais. Anzisha kampeni tutakuchangia.
 
Mashairi yaliyopo kwenye wimbo wa Sifa Bujune, uitwao Mnatuona Nyani tu ni haya.

"BANDARI hatarini wananchi tukilia hatusikilizwi, hii ni kwasababu, Mnatuona Nyani tu.

Ngorongoro ndugu zetu wanaamishwa kwa nguvu, hii ni kwasababu Mnatuona Nyani tu.

Inamaana hao Wageni wanathamani kwenye nchi kuliko wenyeji, hii kwasababu, Mnatuona Nyani tu.

Masai ndugu zetu wamelia kila kilio lakini hawasikilizwi, Mnatuona Nyani tu.

Kijana mdogo kango'lewa meno na maaskari, hii ni kwasababu Mnatuona Nyani tu.

Imefika wakati Tanzania Kila anaepinga DHULMA, anaitwa mkaidi, anaharibu amani ya nchi mara mchochezi, Mnatuona Nyani tu.

Mbarikiwa Mwakipesile amelalamika mtoto ameuwa lakini mmepuuza, Mnatuona Nyani tu.

Amepiga kelele mmempa na kesi, Mnatuona Nyani tu.

Kwa mujibu wa Katiba viongozi ni wawakirishi wa wananchi lakini tunalia kero zetu hazisikilizwi hii ni kwanini? Mnatuona Nyani tu.

"Bidhaa zipo juu Maisha ni magumu kila kitu kimepanda, Mnatuona Nyani tu.

Maisha ni magumu Kodi zipo juu ni kwanini? Mnatuona Nyani tu.

Sikuhuzi umeme kukatika imekua kawaida, Mnatuona Nyani tu

Kazi zinasimama kwa umeme kukatika mbona ni hasara, Mnatuona Nyani tu.

#WenyeNchiWananchi
 
Safi sana, wananchi wameanza kuamka. Wanatuona nyani, WASHENZI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…