Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Sijaona tatizo la huu wimbo. Sijaona uchochezi wowote hapo...
Mwimbaji huyo Sifa Boniventure Bujune (25) ni Mkazi wa Isyesye anatuhumiwa kuimba wimbo unaojulikana kwa jina la “Tanzania Inaelekea Wapi?” wenye maudhui ya uchochezi na kisha kuurusha katika Mitandao ya Kijamii pamoja na YouTube...
Kila kilichowasilishwa kupitia sanaa ya uimbaji ndani ya wimbo huu ni kweli na yapo na Kila mtu ni shuhuda wakiwemo haohao polisi..
Kwa mfano;
√ Je, si kweli kuwa wamasai huko Ngorongoro Loliondo wanalazimishwa kuhamia Handeni - Tanga kwa nguvu na wengi wanaokataa wanapigwa, kuteswa, kutungwa na kuuwawa?
√ Je, si kweli kuwa umeme unakatika katika hovyo na kusababisha kero kubwa kote nchini huku kazi za wananchi zinazotumia umeme kusimama na kusababisha hasara kubwa?
√ Je, si kweli kuwa Kila anayekosoa serikali kwa lugha kali ya kukemea mara zote anaitwa mchochezi?
√ Je, si kweli kuwa Mch Mbarikiwa Mwakipesile polisi wameua mtoto wake Kwa maagizo ya mkuu wa TISS na RSO wa Mbeya na hakuna hatua zilizochukuliwa Kwa wahusika wa mauaji?
√ Je, si kweli kuwa nishati ya mafuta imepanda bei kuliko kawaida na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha kwa sababu ya kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali na serikali haichukui hatua yoyote ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi?
√ Je, si kweli kuwa Tundu Lissu alipigwa risasi mchana kweupe ktk maeneo ya kuishi viongozi serikali Area D Dodoma yenye ulinzi masaa 24 na mpka sasa polisi hawataki kukamata wahalifu hawa?
##Kama haya yanayokea na huku tukiwa na serikali lakini haichukui hatua yoyote kwa nini watu wasiseme labda viongozi wa serikali wenye dhamana na mamlaka ku - regulate mambo wanatuona sisi wananchi na manyani (wanyama) wasio na thamani yoyote?
## Ni kosa kubwa sana kumkamata na kumweka ndani binti aliyeimba wimbo huu badala ya serikali kutoka na kusema, hapana serikali haiwaoni wananchi kama manyani (wanyama) kwa sababu katika hayo serikali inachukua hatua 1, 2, 3 na kuendelea..??
We demand the police to release that lady immediately without any conditions ni Jesus Christ's name..!!!
Na kwa nini polisi mlimuua mtoto wa mchungaji? Alikosa nini hataastahili kuuwawa? Huyo mchungaji anazusha mambo na kusingizia polisi siyo? Kama anazusha, hatua Gani zimechukiliwa na Tanpol kwa kusema uongo dhidi ya polisi???
Serikali hakika mmegusa pabaya!!