Mbeya: Mwalimu aliyesambaza picha za Wanafunzi wamekaa chini, aingia matatani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mwalimu wa mazoezi wa Shule ya Sekondari Sinde - Jijini Mbeya, Evaristo Chona anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya kudaiwa kusambaza picha za Wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwa madai ya kukosa madawati, jambo lililoifanya Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbeya kufika shuleni hapo.
FoYWaODWYAAFeGv.jpg

FoYXYjPXsAA5DRU.jpg

Mwalimu wa mazoezi wa Shule ya Sekondari Sinde - Jijini Mbeya, Evaristo Chona anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya kudaiwa kusambaza picha za Wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwa madai ya kukosa madawati, jambo lililoifanya Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbeya kufika shuleni hapo.

Kumekucha! Chawa wamekereka kwa maana Mama yuko kazini.
 
Watu weusi ni jamii iliyo kwisha laaniwa? mbona vitu vidogo namna hii ccm wanashindwa kuvifanya? So sad
Sio kuvifanya tu uliza gharama wanazotumia kumdhibiti mtoa taarifa kwa umma utadhani hii nchi tumepanga! Wangezitumia kurectify the situation Mara moja!

Kibaya atakuja DC Asema hajatumia njia sahihi kufikisha taarifa angeziambia mamlaka husika zichukue hatua! Utajiuliza kweli DC, DED, DEO, MP, RC, DAS viongozi wa chama woote hapo Mana naamini wote Ni CCM hawajui kwamba Kuna shule x Haina madawati na wanafunzi wanakaa chini? Ukweli Ni kwamba wanajua ili wanajizima data.

Dogo ataumizwa Sana kwakweli kwa kuusema ukweli ili jamii ijue kwamba CCM na serikali yake Ni mabingwa wa statisticious corruption! Wanalaghai wananchi na takwimu ambazo wananchi hawawezi kuzithibitisha!
 
Mwalimu wa mazoezi wa Shule ya Sekondari Sinde - Jijini Mbeya, Evaristo Chona anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya kudaiwa kusambaza picha za Wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwa madai ya kukosa madawati, jambo lililoifanya Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbeya kufika shuleni hapo.
Hawa kamati ya ulinzi na Usalama ni wazembe sana, badala ya kufuatilia pesa ya michango ya madawati imeenda wapi, unahangaika na anayetupa taarifa ili tutoe misaada, hata madirisha hayaridhishi, hivi pesa ya Memkwa/Memki ilijenga hivyo kweli? Nyie viongozi hamjitanmbui, kazi majungu tu. MJITAFAKARI MCHUKUE HATUA
 
Ukweli unauma...

Hapo wameyaweka haraka haraka ili tu kuonekana yapo, ila picha ndiyo msema kweli...
 
Mwalimu wa mazoezi wa Shule ya Sekondari Sinde - Jijini Mbeya, Evaristo Chona anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya kudaiwa kusambaza picha za Wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwa madai ya kukosa madawati, jambo lililoifanya Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbeya kufika shuleni hapo.
Mlisema amekufa Magufuli haya hayakuwepo tena kwa sababu yeye ndiye alikuwa anatoa amri ya kukamata watoa taarifa

USSR
 
Hawa kamati ya ulinzi na Usalama ni wazembe sana, badala ya kufuatilia pesa ya michango ya madawati imeenda wapi, unahangaika na anayetupa taarifa ili tutoe misaada, hata madirisha hayaridhishi, hivi pesa ya Memkwa/Memki ilijenga hivyo kweli? Nyie viongozi hamjitanmbui, kazi majungu tu. MJITAFAKARI MCHUKUE HATUA
Kamati wamekuwa wa kwanza kulifanya siasa jambo hili,
Kisa tu eti WAMEKUTA PICHA ZA KOMBATI YA CHAMA CHA CDM
Very shame!!
 
Back
Top Bottom