Mbeya: Mwandishi wa Habari afariki baada ya kujifungua

Mbeya: Mwandishi wa Habari afariki baada ya kujifungua

Huo sio uzembe wa madaktari kweli?
Mkuu unaweza usiwe uzembe ila labda ni sababu ambazo hazizuiliki, je unajua ni wangapi wamefanyiwa na wapo vizuri tuu? Hapo meta ni hospital ya rufaa kanda wapo maspecialist wengi tuu wa wanawake ingekua ni jambo lakuzuilika lingezuilika mapema tuu na ukiona mama amejifungua kafariki ujue ni issue kubwa na watu apo wamepigana kumwokoa hadi mwisho wa uwezo wao.
 
Operation siyo nzuri kabisa kuna muda nakata tamaa kuongeza watoto...nikikumbuka nafanyiwa upasuaji huku nikiwa na mashine ya kupumulia 😓 R I P cute
NadhanI tatizo kubwa linakuwa shida ni preassure.

Ila madogo sisi tuliozaliwa kwa operation tunakuwaga wacheshi afu wajanjawajanja yani,tumawahi kuona mwanga mapema tofaut na yule anayezaliwa kwa njia ya kusukumwa na kuvutwa.
 
NadhanI tatizo kubwa linakuwa shida ni preassure.

Ila madogo sisi tuliozaliwa kwa operation tunakuwaga wacheshi afu wajanjawajanja yani,tumawahi kuona mwanga mapema tofaut na yule anayezaliwa kwa njia ya kusukumwa na kuvutwa.
Ucheshi hujakosea,wanangu ni wacheshi sana.Yeah,nina shida ya pressure ya kupanda wakati wa kujifungua
 
eti UZEMBE wa daktari! ,,, halafu huna hata chembe ya ufahamu wa RISK wala COMPLICATIONS zozote za C-Section.
 
Daahh nikionaga hizi habar za maternal death huwa ubongo una stuck kabisa maana wife ni previous scar mjamzito miez 6 na ana pressure ya kushuka Kila nikiuliza naambiwa uwezekano mkubwa akafanyiwa tena upasusji basi ndio nachoka Zaid.

Mungu atamfanyia wepesi Ameen!!!
 
View attachment 2225156
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC) kimepata pigo baada ya kuondokewa na mwanachama wake wa muda mrefu, Hannerole Mrosso aliyefariki baada ya kujifungua katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kitengo cha Wazazi Meta Jijini Mbeya tarehe Mei 13, 2022.

Akitoa taarifa mume wa marehemu, Baraka Kasubiri ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii amesema mkewe alifanyiwa upasuaji na kujifungua mtoto wa kike na muda mfupi baada ya kujifungua alipoteza maisha akimuacha mtoto ambaye anaendelea vizuri.

Taratibu za mazishi zinafanywa eneo la Sokomatola Jijini Mbeya ambapo mwili umesafirishwa kwenda Namtumbo Mkoani Ruvuma kwa maziko yanayotarajiwa kufanyika tarehe leo Mei 15, 2022.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwaisango amesema marehemu alikuwa ni mwanachama ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa tasnia ya habari pia alikuwa na ushirikiano na kila mtu.

Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Uchumi kwa Wanahabari (MJEF), Kakuru Msimu amesema msiba huu umewaumiza hasa pale ambapo wanapompoteza mwenzao ambaye walitegemea kujikwamua kiuchumi.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi Wanahabari Wanawake, Esther Macha amesema wamepata pigo kwani wamempoteza mwanachama wao ambaye alikuwa na mchango mkubwa tangu kuanzishwa chama chao.

Sambo amesema marehemu ambaye pia alikuwa mwanachama chama cha kusaidiana wanahabari (Amani) amefariki wakati chama chao kikiwa kichanga na marehemu alikuwa mshiriki mwaminifu.

"Ni vigumu kuamini kuwa Hannerole ametuacha kwani upole wake na ucheshi wake ulikuwa ni faraja katika kikundi," amesema Martha.

Naye mwandishi mwandamizi Felix Mwakyembe amesema tasnia imeondokewa na mwandishi ambaye alipenda kujifunza na kujiendeleza kielimu ambapo hadi umauti alikuwa akisoma Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) Mbeya.

Mmoja wa wanafunzi wa TEKU, Shaban Nassoro Kisilwa amesema ndoto za mwenzao zimezimika ghafla kwani walitarajia kuhitimu naye mwaka huu.

Shughuli zote za msiba zinaratibiwa na Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Kenneth Mwakandyali ambapo amewataka waandishi kushirikiana katika kumsindikiza mwenzao katika safari yake ya mwisho.

Enzi za uhai wake marehemu amewahi kuhudumu kituo cha Radio cha Generation Fm na Baraka Fm akiwa masomoni.

Marehemu ameacha watoto watatu wawili wakiwa ni mapacha Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

Chanzo: Mwanahalisi
Poleni wanahabari mbeya.
 
Pole nyingi sana kwa baba watoto. Ni uchungu kuachiwa kitoto kichanga. Mungu ampe moyo mkuu huyo baba.
 
Back
Top Bottom