Mbeya: Mwekezaji ajinyonga baada ya ng'ombe wake 50 kukamatwa na Maliasili, RC Chalamila acharuka asihusishwe

Mbeya: Mwekezaji ajinyonga baada ya ng'ombe wake 50 kukamatwa na Maliasili, RC Chalamila acharuka asihusishwe

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwekezaji mzawa katika sekta ya mifugo huko Ihefu mkoani Mbeya amekutwa amejinyonga kwenye mti porini baada ya ng'ombe wake 50 kukamatwa na askari wa Idara ya Maliasili.

Baba wa marehemu amesema mwanae amejinyonga kwa kuhofia ufukara na umaskini baada ya kunyang'anywa ng'ombe wake wote ambao wamehifadhiwa ofisi ya wilaya.

Naye mkuu wa mkoa wa Mbeya mh Chalamila amekiri kupata taarifa za tukio hilo na ametaka Serikali isihusishwe kwa namna yoyote ile na uamuzi wa mwekezaji huo kujinyonga kwani huo ni uamuzi wake binafsi hakuna aliyemshinikiza.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Pole yake sana

Kuna kauzi kalitrend asubuhi kuwa serikali ianze kutoza kodi kwa kila ng'ombe

Niliona mazingira sio rafiki saa hii kuna mfugaji kasepa kawaachia ng'ombe

Kiukweli mazingira sio rafiki kivile kwa wafugaji
 
Serikali isihusishwe na kifo cha mwananchi wake?

Je, huyo jamaa angepata utajiri na kuuza mifugo mpaka nje na kuletea kodi taifa tusingeiongelea serikali ya awamu ya 5?

When you take credit for all good things, don't forget to take responsibility when they go wrong.
 
Chalamila amepanic!
 
Back
Top Bottom