TANZIA Mbeya: Mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi, Michael Kalinga akutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa

TANZIA Mbeya: Mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi, Michael Kalinga akutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa

Inasikitisha sana!
Haya mambo ndio katoka kusema Askofu Yuda Thadeus Ruwa'ichi....
Naona taratibu tunaelekea kwenye matatizo makubwa sana kama Taifa....
Mdogo mdogo tunaelekea kwenye jino kwa jino! Jicho kwa jicho!
Wanaoteka, kutesa na kuua wengine na kunyamaziwa watasababisha madhara kwa wengi!
 
Ccm wakiuliwa hatusikii haki za binadamu wakizungumza ila wakifa vyama vingine

..hakuna anayepiga kelele kwasababu watu wana imani kwamba CCM siku zote wanatendewa haki.

..haki za binadamu wako kutetea wale ambao hawana sauti, wanaonyanyaswa, na hawana watetezi.

..CCM inao makada wake katika vyombo vyote vya dola hapa nchini. Mwenyekiti wa Ccm ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Kwa mantiki hiyo mwanaCCM akipatwa na matatizo lazima atasaidiwa na vyombo vya dola.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Tawi la Machinjioni, Kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya, Michael Kalinga amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne, Desemba 3, 2024 na mwili wake kukutwa Kata ya Mkola.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa amesema wamepata taarifa za mauaji ya Kalinga na wanaendelea kuzifanyia kazi.

Katibu wa CCM Wilaya Chunga, Charles Jockel akizungumza na Mwananchi amesema amepokea taarifa hizo leo Jumanne asubuhi kutoka kwa uongozi wa CCM Kata ya Makongorosi.

"Haijulikani alikuwa anakwenda au kurudi Makongorosi maana mwili wake umekutwa eneo la kuelekea Kata ya Mkola," amesema Jockel.

Kumbe na maccm nayo yanakufa? Au ndiyo drama tu kama alivyowahi kusema mwenyekiti wao ili kubalance matukio?
 
Aiseee
Haya mambo yanazidi kupamba moto
Mungu turehemu

Wanaofanya haya, Mungu yupo.
 
Imeniuma sana kumpoteza kijana mtiifu kwa taifa lake na chama chetu .tunatoa wito kwa polisi kufanya uchanguzi wa kutosha kuhakikisha walimuua wanaopatikana na kuchukuliwa hatua stahiki

USSR
View attachment 3168062weny
Huyu sijui chochote juu yake; ndiyo sababu nasita kuchukua upande. Siamini kamwe hata siku moja kwamba waTanzania wote waliomo CCM wana stahili haya yaliyo mtokea huyu.
Lakini, kama alikuwa kama yule UVCCM wa Kagera; nisinge sita kumtakia kheri huko aendako.

Ni bahati mbaya sana kwamba viongozi wa nchi hii wame tufikisha katika hali hii ya mgawanyiko kama taifa.
 
Back
Top Bottom