Mbeya: Polisi inawashikilia watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti wa UVCCM tawi la Machinjioni kata ya Bwawani Makongolosi

Mbeya: Polisi inawashikilia watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti wa UVCCM tawi la Machinjioni kata ya Bwawani Makongolosi

Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) tawi la Machinjioni kata ya Bwawani Makongolosi wilayani Chunya Michael Andarson Kalinga (36) mkazi wa wilayani humo.

Inaelezwa kuwa watu hao ambao hawajatajwa majina walimpiga marehemu na kitu butu kichwani.Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert Siwa amesema mnamo Desemba 2, 2024 majira ya saa tano usiku huko katika eneo la Mianzini Mikoroshini, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, mtu aitwaye Michael Andarson Kalinga (36) alikutwa amefariki dunia na mwili wake umetelekezwa porini umbali wa mita 250 kutoka barabara ya Makongolosi - Lupatingatinga baada ya kupigwa na kitu butu kichwani sehemu ya utosini.

Pia, Soma: Mbeya: Mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi, Michael Kalinga akutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa

Kaimu Kamanda Siwa amesema kuwa baada ya hapo watuhumiwa hao walimpora marehemu pikipiki yake yenye namba za usajili MC.464 ELL.Aidha, amesema Jeshi la Polisi lilianza msako mara moja ambapo Desemba 3, 2024 huko katika Mji mdogo wa Mlowo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakihusika na tukio hilo wakiwa na pikipiki waliyopora kutoka kwa Michael Andarson Kalinga.

Polisi imesema upelelezi wa shauri hilo unaendelea ili hatua nyingine za kisheria zifuate na limetoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaoendelea kujihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja tabia hiyo.
 
yawezakana aliyekamatwa aliuziwa pikipiki kimasihara anaenda kufia jela.

kifungo cha maisha kinamuhusu
 
Ben sanane
Anzory gwanda
Alphonso mawazo
Deo soka
Akwilin akwilin
Mgombea wa chadema manyoni aliyepigwa risasi kiunoni
WAKO WAPI? HUYU JANA TU WAUAJI WAMESHAKAMATWA?
Angalizo isije ikawa kama ya dr. Mvungi kwamba alikatwakatwa na .mapanga yaliyovingirishwa bendera ya CHADEMA!
Isijeikawakama DR ULIMBOKA KWAMBA ALISHAMBULIWA NA CHIZI MKENYA?
ISIJE IKAWA YA AKWILIN KWAMBA RISASI ILIPINDA NA KUKATA KONA
ISIJE IKAWA FUTUHIII
 
Ben sanane
Anzory gwanda
Alphonso mawazo
Deo soka
Akwilin akwilin
Mgombea wa chadema manyoni aliyepigwa risasi kiunoni
WAKO WAPI? HUYU JANA TU WAUAJI WAMESHAKAMATWA?
Angalizo isije ikawa kama ya dr. Mvungi kwamba alikatwakatwa na .mapanga yaliyovingirishwa bendera ya CHADEMA!
Isijeikawakama DR ULIMBOKA KWAMBA ALISHAMBULIWA NA CHIZI MKENYA?
ISIJE IKAWA YA AKWILIN KWAMBA RISASI ILIPINDA NA KUKATA KONA
ISIJE IKAWA FUTUHIII
Huyo ni ndugu yao ktk imani..thats why..
 
Wangekuwa wamemuua kiongozi wa CHADEMA wasingepatikana kamwe
 
Kuna ubaguzi kwenye vyombo vya dola. Mbona watuhumiwa wamepatikana haraka.
 
Chadema hawataki kutoa ushirikiano CCM wanatoa ushirikiano
Familia ya mzee Kibao wamejitahidi kufuatilia ila ni hakuna tu..
 
Back
Top Bottom