Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) tawi la Machinjioni kata ya Bwawani Makongolosi wilayani Chunya Michael Andarson Kalinga (36) mkazi wa wilayani humo.
Inaelezwa kuwa watu hao ambao hawajatajwa majina walimpiga marehemu na kitu butu kichwani.Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert Siwa amesema mnamo Desemba 2, 2024 majira ya saa tano usiku huko katika eneo la Mianzini Mikoroshini, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, mtu aitwaye Michael Andarson Kalinga (36) alikutwa amefariki dunia na mwili wake umetelekezwa porini umbali wa mita 250 kutoka barabara ya Makongolosi - Lupatingatinga baada ya kupigwa na kitu butu kichwani sehemu ya utosini.
Pia, Soma: Mbeya: Mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi, Michael Kalinga akutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa
Kaimu Kamanda Siwa amesema kuwa baada ya hapo watuhumiwa hao walimpora marehemu pikipiki yake yenye namba za usajili MC.464 ELL.Aidha, amesema Jeshi la Polisi lilianza msako mara moja ambapo Desemba 3, 2024 huko katika Mji mdogo wa Mlowo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakihusika na tukio hilo wakiwa na pikipiki waliyopora kutoka kwa Michael Andarson Kalinga.
Polisi imesema upelelezi wa shauri hilo unaendelea ili hatua nyingine za kisheria zifuate na limetoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaoendelea kujihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja tabia hiyo.