Inaumiza sana, wazazi wamezaa, wamelea imefikia mtoto kuwa huru kujisimamia anauawa, anaua na kuishia jela.
Wazazi na walezi tuendelee kufanya kazi ya kuongea na watoto wetu, tuwape elimu ya kujitambua haswa kwenye mambo ya mahusiano kwenye makuzi yao na zaidi kipindi wanapoanza kwenda vyuoni maana huko ndio wanakojiachia wakijiona wamekua huru na kuharibu.
Kuna mengi tunatakiwa kuwafundisha vijana wetu lakini hayafanyiki, tumeacha desturi, imani zetu nazo hatufuatilii, tupotupo tuu uzungu hatuwezi na asili hatuzitaki. Mungu utusaidie kwenye malezi