Mbeya: Polisi wanamshikilia Suzy Keneth(19) kwa mauaji ya Mwanafunzi James Magesa (21)

Vijana wadogo badala ya kusoma , wanakimbilia mapenzi.. utadhani papuchi zinaoza..
Mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza chuo kikuu Cha sayansi na technologia Mbeya (MUST) ndg Linus magesa (21) Ameuwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha Kali kifuani na mtu anayesadikika kua Ni mpenzi wake Anayetambulika kwa jina la Suzy (19) chanzo kikisadika kua Ni wivu wa mapenzi, Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi.

MAPENZI !MAPENZI TENA!!

======

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SUZY KENNETH KASITEJETA [19] Mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya LINUS JAMES MAGESA [21] Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya [MUST] Kitengo cha Biomedical mwaka wa kwanza na Mkazi wa Ikuti kwa kumchoma kitu chenye ncha kali kifuani.

Ni kwamba mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 22:00 Usiku huko eneo la Ikuti lililopo Kata na Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya SUZY KENNETH KASITEJETA [19] na LINUS JAMES MAGESA [21] ambao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi waligombana na kupelekea LINUS JAMES MAGESA kujeruhiwa sehemu za kifuani kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali na SUZY KENNETH KASITEJETA hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu.

Leo tarehe 18.07.2020 majira ya saa 00:05 Usiku LINUS JAMES MAGESA [21] alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa wapenzi hao walikuwa wakigombana mara kwa mara. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

WITO:

Ninatoa wito kwa jamii kutofumbia macho ugomvi unatokea mbele yao kwa kudhani ni kitu cha kawaida na kukaa kimya, ni wito wa Jeshi la Polisi kwa jamii kutoa taarifa mapema kwa Watendaji wa Kata au Wenyeviti wa Mitaa ambao ni walinzi wa amani katika maeneo yao ili waweze kuchukua hatua za awali kupitia baraza la usuluhishi la Kata au Mtaa.

KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia DICKSON KABUJE [32] Mkazi wa Ikumbi akiwa na mali mbalimbali za wizi.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 14:00 Mchana huko Kijiji cha Ikumbi, Kata ya Utengule – Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya na katika upekuzi alikutwa akiwa na mali za wizi ambazo:-

Spika kubwa 02,

Redio Sub-Woofer 01 na Spika zake,

Stablizer 01, m

Mtungi mkubwa wa gesi Mihani 01,

Deki 02 za Singsung,

Godoro 01 Super Banco.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
View attachment 1510607
View attachment 1510630
 
Yaan vijana wa vyuo miaka hii Mapenzi yamekuwa too much compare na miaka ya nyuma... Pita jioni hadi usiku usiku mitaa kuanzia mlimani city kuja hizo hostel za mheshimiwa hadi ubungo mataa it's time for couple kila hatua couple...
Umri unachangia wanachuo wa sasa wengi umri mdogo, hawana ukomavu.
Tofauti na zamani.
 
mapenzi ya wivu mkali yanapatikana umri huo maana wahusika hua ni wachanga wa haya mambo
 
Mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza chuo kikuu Cha sayansi na technologia Mbeya (MUST) ndg Linus Magesa (21) ameuwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha Kali kifuani na mtu anayesadikika kua ni mpenzi wake anayetambulika kwa jina la Suzy (19). Chanzo kikisadika kua Ni wivu wa mapenzi, Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi.

MAPENZI !MAPENZI TENA!!

======

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SUZY KENNETH KASITEJETA [19] Mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya LINUS JAMES MAGESA [21] Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya [MUST] Kitengo cha Biomedical mwaka wa kwanza na Mkazi wa Ikuti kwa kumchoma kitu chenye ncha kali kifuani.

Ni kwamba mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 22:00 Usiku huko eneo la Ikuti lililopo Kata na Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya SUZY KENNETH KASITEJETA [19] na LINUS JAMES MAGESA [21] ambao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi waligombana na kupelekea LINUS JAMES MAGESA kujeruhiwa sehemu za kifuani kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali na SUZY KENNETH KASITEJETA hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu.

Leo tarehe 18.07.2020 majira ya saa 00:05 Usiku LINUS JAMES MAGESA [21] alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa wapenzi hao walikuwa wakigombana mara kwa mara. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

WITO:

Ninatoa wito kwa jamii kutofumbia macho ugomvi unatokea mbele yao kwa kudhani ni kitu cha kawaida na kukaa kimya, ni wito wa Jeshi la Polisi kwa jamii kutoa taarifa mapema kwa Watendaji wa Kata au Wenyeviti wa Mitaa ambao ni walinzi wa amani katika maeneo yao ili waweze kuchukua hatua za awali kupitia baraza la usuluhishi la Kata au Mtaa.

KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia DICKSON KABUJE [32] Mkazi wa Ikumbi akiwa na mali mbalimbali za wizi.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 14:00 Mchana huko Kijiji cha Ikumbi, Kata ya Utengule – Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya na katika upekuzi alikutwa akiwa na mali za wizi ambazo:-

Spika kubwa 02,

Redio Sub-Woofer 01 na Spika zake,

Stablizer 01, m

Mtungi mkubwa wa gesi Mihani 01,

Deki 02 za Singsung,

Godoro 01 Super Banco.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Hao hawakuwa wapenzi bali wachezea viungo vya uzazi!
 
Mademu wanaopenda kiasi hicho kumbe bado wapo........ Hawa ndio mademu, demu anaye hakikisha ni hadi kifo kiwatenganishe....
Napenda wanawake wenye wivu hivi.
Ila huyu alichokosa ni zile lifeskills tulizofundishwa sekondari.Hasa hasa ile decision making.
Na hicho ndo kinachomgharimu sasa.
 
Mapenzi mapenzi yanahitaji akili na uvumilivu kweli.

Nakumbuka siku namaliza mtihani wa kidato cha 6 nilirudi ghetto huku na furaha tele. Nafika tu mtaa niliopanga ghetto langu namtafuta manzi wangu tupige picha ya ukumbusho akataa kabisa hali inabadilika natokwa na jasho na mwili unalowa.

Nilikua nampenda saana yeye aliishia kidato cha 4. Kesho yake namfata kwao kujua kulikoni namfumania na njemba, akili ziliniruka kama mweu nilitembeza kipigoo hatari nilikua nasikia tu majirani wanasema nitauaa. Kila nikiwaza tukio lile ningeishia polisi na kuniharibia future zangu shukrani zimuendee dada wa bint ambaye alizuia wasiende polisi.

Nikiwa chuo tena yakanipata nilikua na mahusiano na bint mwanachuo nikajikuta nampa ujauzito kumbe nyumbani alikua na mahusiano na jamaa mimi nilidanganywa. Yule jamaa alipogundua alikua mbogo aswaa pona yangu ni umbali maana matusi, vitisho tele.fikiri kama tungekua karibu. Wakafanya mchakato wakautoa ule ujauzito najua jamaa aliumia sana.

Nilimaliza salama na bahati nikapata ajira, nafurahia maisha ya single. Wao hadi leo hawajaolewa.

Pumzika kwa Amani kamanda!!
Hao mabinti wote hawajaolewa hadi sasa?
 
Ulipata daraja gani form six mheshimiwa?
 
Back
Top Bottom