Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Pia limesema ambao hawakuachiwa ni wale walioshindwa kukidhi masharti ya dhamana au kuwa na makosa zaidi ya moja, ikiwemo jinai.
Limesema halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekiuka sheria na taratibu za nchi kwa kuiga mataifa mengine.
Wanahabari wa Jambo TV Ramadhan Khamis na Fadhil Kirundwa pamoja na wanahabari wengine waliokuwa wakishikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya tangu Jumapili nao wameachiwa huru.
Pia soma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akamatwa uwanja wa Ndege Songwe
Akizungumza usiku huu Agosti 12, 2024 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo nchini, Awadhi Haji amesema Agosti 11 walikamatwa 375, ikiwa wanaume 261 na wanawake 114 na leo Agosti 12 wamekamata 145, wanaume 112 na wanawake 33.
"Kati ya watuhumiwa waliokamatwa kwa kosa la kukaidi kuendelea na safari kuja Mbeya, walikuwemo viongozi wakuu wa Chadema waliokamatiwa mkoani hapa eneo la Kadege, ambao ni Makamu Mwenyekiti Tundu Lisu, Katibu Mkuu, John Mnyika, Mwenyekiti wa Kanda, Joseph Mbilinyi 'Sugu', Katibu Mwenezi wa Bavicha Taifa, Twaha Mwaipaya na Makamu Bavicha, Moza Ally.
"Agosti 12 Jeshi la Polisi limewakamata wafuasi wengine 145 wakiwamo viongozi wakuu wa chama hicho Taifa, ambao ni Mwenyekiti Freeman Mbowe na Mwenyekiti Bavicha Taifa, John Pambalu katika Uwanja wa Ndege Songwe wakija kushiriki kongamano lililopigwa marufuku na kufanya jumla ya waliokamatwa kufikia 520" amesema Kamanda Haji.
Pia soma: Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Kamanda huyo amesema kuwa watuhumiwa wote walihojiwa kisha kurejeshwa maeneo walipotoka kwa kusindikizwa na Polisi, huku waliokamatwa kutoka Mkoa wa Mbeya wakipewa dhamana.
Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Mbeya na maeneo yote nchini penye viashiria vya uvunjifu wa amani na linaendelea kufuatilia mipango ya kufanya uvunjifu wa amani na atakayebainika atachukuliwa hatua bila kujali nafasi wala cheo chake.
Pia soma: Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Jeshi la Polisi linawataka viongozi wote wa vyama vya siasa na wafuasi wake kufuata sheria na taratibu za nchi na litachukua hatua kali za kisheria kwa mtu au kikundi kitakachojihusisha na vya uvunjifu wa amani," amesema Kamanda huyo.
Mwananchi
Pia soma=> Mbeya: Vijana wa CHADEMA waliokuwa wanashikiliwa waanza kuachiwa bila masharti yoyote