Mbeya: Raia 37 wa Ethiopia washikiliwa kwa kuingia nchini bila kibali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 37 wanaume raia wa nchini Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.

Watuhumiwa walikamatwa Januari 16, 2026 saa 10 jioni katika Kijiji cha Kasumulu, Wilayani Kyela, Mkoa wa Mbeya na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na Maafisa Uhamiaji wakiwa katika oparesheni ya pamoja ya kuzuia na kudhibiti uhalifu.

Wahamiaji hao walisafiri na kuingia nchini kwa kificho kwa kutumia njia zisizo rasmi kisha kufichwa kwenye nyumba moja mali ya mtu aliyefahamika kwa jina moja la Kasanga iliyopo mashambani mbali na makazi ya watu.

Taratibu nyingine za kisheria zinaendelea kukamilishwa kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya.
PC HASSAN.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga.
​
WAWILI WATIWA MBARONI KWA KUTENGENEZA BIDHAA BANDIA.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Watumishi wa Kampuni ya Brewmaster Limited linawashikilia watuhumiwa wawili, Muddy Damata maarufu Abdalah, Miaka 26, Mkazi wa Soweto Jijini Mbeya na Juma Said maarufu Juma, Miaka 49, Mkazi wa Isangawana Wilayani Chunya kwa tuhuma za kutengeneza pombe bandia.

Watuhumiwa walikamatwa Januari 18, 2026 saa 7 usiku katika Kitongoji cha Mpakani, Kijiji cha Isangawana, Wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya wakiwa na bidhaa bandia na zisizo na kiwango ambazo ni pombe kali aina ya Panmaster katoni 49, Konyagi kubwa boksi 8, Konyagi za kati boksi 8 na Konyagi ndogo boksi 18.

Watuhumiwa walikamatwa na pombe hizo bandia “fake” wakiwa tayari wakijiandaa kusambaza kwa wateja.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa baadhi ya wananchi ambao bado wanaendekeza tabia ya kujipatia mali na fedha kinyume cha sheria kuacha mara moja kwani madhara yake ni makubwa kwao na kwa jamii kama ilivyotokea kwenye tukio hili la mauaji ya Juveni Baraka Mwambugi.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wageni kufuata sheria na taratibu za kuingia nchini ili kuepuka usumbufu na kuchukuliwa hatua za kisheria. Pia, linatoa wito kwa baadhi ya watu wanaotengeneza pombe bandia na zisizo na kiwango kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria lakini pia zinasababisha madhara kwa wanaozitumia. Aidha, kwa wanauza vileo wahakikishe wananunua bidhaa zao kutoka kwa wasambazaji halali na wanaofahamika kupitia kampuni au wakala wanaofanya biashara kama hizo.
 
View attachment 3532623

Ni ajabu maustadh wanatengeneza pombe feki! Hii ni dhambi double.
 
Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 37 wanaume raia wa nchini Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Huww sisikii wahamiaji haramu wanawake
 
Back
Top Bottom