ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa masaa 24 kutiwa mbaroni Kwa Kijana mmja huko Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.
My Take
Naunga mkono hoja, upumbavu wa tabia za kihuni za kuiga ukomeshwe na usiruhusiwe hapa Tanzania.
Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.
Tanzania haiwezi na haitakuja kuwa Taifa la wahuni.Safi sana Polisi Kwa kumtia nguvuni,alijikuta Gen Z sana.
Ni vyema ikaeleweka kwamba Watanzania tuelewe nafasi ya Rais kama Kiongozi wa nchi na tumheshimu Rais Samia Suluhu Hasani
====
Mkuu wa mkoa wa mbeya cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini kuzaga kumsaka na kumkamata kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia kwa maneno makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais.
RC Homera amelaani vikali kitendo hicho kuwa si cha maadili wala uungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wananchi mkoani Mbeya.
Hata hivyo ametoa masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga kumkamata kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza moja kwa moja kwa Rais Samia.
Mwisho RC Homera amewasihi wananchi mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye vitendo viovu kwa kukashifu viongozi makusudi badala yake wajikite katika utafutaji na uchapa kazi kwa manufaa ya familia zao na Tanzania kwa ujumla.
Video ya Kijana akichoma moto picha ya Rais Samia.
Pia soma==>> Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela