Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais ni Mali ya Umma sio yake ,kuharibu Mali ya Umma ni kosa na vibaya kimaadili.
Umewaza kipumbavu , kichawa. Ukikaa ukapata akili utagundua hamna kosa alilofanya. Rais si Mungu. Ni binadam wa kawaida kabisa. Amevunja sheria gani kwa kuchoma picha ambayo ni mali yake ameona ni takataka? Mi nimechoma sana hayo mapicha.
 
Hiyo picha ni mali yake ana haki ya kuifanya atakavyo

Bendera za Israel na Marekani kila mara zinachomwa moto ndio sembuse chura kiziwi.

Yupo mwamba mpaka nakala za Qurani kapiga moto ni mali yake huwezi kumpangia.
Thubutu yake..!!Labda achome kimya kimya,achome hadharani aone...
 
Picha ya huyo chura kiziwi inatukera sana sisi wazalendo.kijana kaonesha uzalendo sana kuchoma hiyo takataka.kila Kona ya Nchi wamebandika picha yake Hadi kuharibu muonekano wa Nchi(uchafuzi wa mazingira).
 
Umewaza kipumbavu , kichawa. Ukikaa ukapata akili utagundua hamna kosa alilofanya. Rais si Mungu. Ni binadam wa kawaida kabisa. Amevunja sheria gani kwa kuchoma picha ambayo ni mali yake ameona ni takataka? Mi nimechoma sana hayo mapicha.
Kama sio Mungu ndio inatakiwa picha yake kuchanwa? Hilo ndio kosa sasa
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Z. Homera ametoa Muda wa Saa 24 kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga, kumsaka na kumkamata Kijana ambaye jina lake halijafahamika mkazi Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Kwa Kosa la Kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maneno Makali na Kisha kuichoma moto Picha inayomuonyesha Rais Samia Suluhu Hassan.

Homera amesema Kitendo hicho kuwa si Cha kimaadili Wala Uungwana na Kiko tofauti na Utamaduni halisi wa Wananchi wa Mkoani Mbeya.Hata hivyo ametoa Masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga Kumkamata Kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na Mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza Moja kwa Moja kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine Homera amewasihi Wananchi Mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye Vitendo viovu kwa Kukashifu Viongozi Makusudi badala yake wajikite katika Utafutaji na Uchapa Kazi kwa Manufaa ya Familia zao na Tanzania kwa Ujumla.
 
Back
Top Bottom