Mahakama ya wilaya ya kyela imemtia hatiani na kumhukumu miaka 30 jela mshitakiwa aliefahamika kwa jina la claud Alex Mwinuka alimaarufu kama kibakuli(22) mkazi wa mwanganyanga kyela kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.
Akizungumza mahakamani hapo Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya kyela Paul Mabula Barnabas amesema kuwa mshtakiwa amefikishwa mahakamani hapa leo tar 6/4/2022 kwa kosa la kuruhusu mwanaume kumuingilia kinyume na maumbile ikiwa ni kinyume cha kifungu cha 154 kifungu kidogo cha kwanza C cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo,mshtakiwa akakili kosa na baada ya kukili mahakama imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela.
Itakumbukwa video za kijana huyo zilisambaa katika mitandao ya kijamii siku chache zilizopita ikiwa amevaa mavazi ya kike usiku wa manane pindi alipokamatwa na vikundi vya ulinzi shirikishi maarufu kama sungusungu.
View attachment 2578736