Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Hivi kuna ulazima gani wa Tulia kwenda na media kila sehemu anapoenda kutoa misaada?
Kwenye hii video anasema anaita vyombo vya habari kila anapotoa misaada ili awape motisha mwingine.
Hivi kweli kuna mtanzania wa kawaida unayemjua ambaye ataenda kutoa misaada kwa sababu ya motivation kutoka kwa Tulia?
======================================================
Spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson, ametoa zaidi ya tani mbili za chakula na mboga kwa watu wenye uhitaji zaidi jijini Mbeya kwaajili sikukuu za mwisho na mwanzo wa mwaka.
Akikabidhi chakula kwa watu hao Dkt Tulia amesema wanatarajia kutoa chakula kwa wahitaji takribani 3000 kwenye kata zote 36 za jiji la Mbeya kwa lengo la kutoa tabasam kwa watu hao ili nao washeherekee sikukuu wakiwa na furaha kama watu wengine.
Nao baadhi ya watu wenye uhitaji zaidi kwenye kata za jiji la Mbeya waliopatiwa chakula hicho wameeleza hisia zao ikiwa ni pamoja na kumshukuru mbunge wao kwa kuwajali kipindi hiki cha sikukuu.