Mbeya: Viongozi walioshinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa warudisha fadhila kwa wananchi

Mbeya: Viongozi walioshinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa warudisha fadhila kwa wananchi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Viongozi wa mtaa wa Masewe na Ilemi kutoka mkoani Mbeya,Patrick Mwashuma na Lupakisyo Mwasasu, wamefanya hafla ya kuwashukuru wananchi wa kata hizo kwa kuwapigia kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, uliofanyika Novovemba 27.2024.

Katika hafla hiyo iliyofanyika leo kwenye viwanja vya James kata ya Ilemi, viongozi hao wameahidi kuwahudumia wananchi kwa moyo wao wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Sifa Abdul, amesema wameamua kuandaa hafla hiyo ili kuongeza hamasa na kudumisha umoja na ushirikiano ndani ya kata hayo.

Aidha Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo, wamewapongeza viongozi hao kwa kuja kuwashukru, huku wakiahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika shughuli za Maendeleo .

Mbeya .png
 
Back
Top Bottom