Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Zoezi la kujiandikisha limeishia Sasa ni mwendo wa kuhakiki taarifa zako kama ziko sawa.
Leo ndugu zangu nimekuja na jambo hili kutoka Kwa hawa watumishi wa Dampo kuu Jiji la Mbeya lililopo kata ya Nsalaga.
Hawa watumishi wamekuwa siyo waadirifu kabisa katika majukumu Yao,wanakoelekea watakuja kutuua.
Hivi karibuni imezuka tabia moja mbaya sana kutoka Kwa hawa watumishi wa Dampo.
Mamlaka mbalimbali hapa jijini pindi wakamatapo vitu ama bidhaa ambazo either zimepigwa marufuku kuingizwa nchini ama muda wake wa matumizi umeisha basi huwa wanaenda kuzitupa Kwenye Dampo hilo.
Sasa baada ya bidhaa hizo kutupwa hapo,ndipo watumishi wa Dampo hilo wanazichukua na kuzirudisha mtaani tena wanaziuza Kwa Bei nafuu kabisa.
Miezi ya hivi karibuni ilikamatwa shehena ya Samaki aina ya Sato ambao walikuwa wameharibika, mamlaka husika wakachukua jukumu la kuwatupa ,lakini baada ya masaa machache Samaki hao wakatapakaa mitaani wakiuzwa Kwa wananchi.
Njemba hizo hazijaishia Kwenye Samaki tu bali hali imekuwa mbaya zaidi sababu wameanza pia kuzoa vipodozi pamoja na pombe Kali ambazo hutupwa Dampo hapo na kuanza kuuza mitaani.
Tunawaomba viongozi wa Jiji hasa kitengo ambacho kinasimamia Dampo hilo kuhakikisha bidhaa zote zinazotupwa hapo ziwe zinachomwa moto chini ya uangalizi Mkubwa.
Hatakama maisha magumu ndiyo mtulishe Samaki wa Dampo kweli,enyi watumishi kuweni waadirifu basi mtatuua .