Mod Tunakuomba muanzishe policy ya ku vet articles zilizo na headings za uchochezi kwa jamii. kama hii, La kuuliza ni kwa nini janga linapomtokea mtu au familia yake kuna watu humu jamvini wanakimbilia kuleta huo uzi ukiwa na political affiliations za mhusika. Ingekuwa kitendo hiki kimemtokea mwananchi wakawaida tusingelisika hapa JF.
Juzi aliuawa mtu huko mwanza aliyekuwa katibu wa ccm wa zamani, tukaletewa uzi ukiwa na heading ikisema incumbent party head, na hali hana cheo hicho. Wengine huja na uchochezi wa kidini.
Ndugu zangu napenda kuwashauri ya kuwa sisi wa africa hatuuani kwa siasa hata siku moja bali tunauana kwa mambo ya kijinga kama Udini na Ukabila, hebu tuangalie yanayotokea huko Africa ya Kati na Sudan ya kusini, Jee hiyo ua ua ama chinja chinja inamfaidia nini mwafrika. Jee Tanzania yetu inastahili fitina kama hizo ?
Huyu aliyeleta huu uzi anastahili Ban, kwa namna alivyouelekeza uzi wake, huu ni uchochezi wa hali ya juu, hao walio kwenda kwauwa viumbe visivyo na hatia, wanastahili kifungo na kupelekwa mahakamani, na kama walifanya hivyo kwa sababbu wamedhulumiwa, basi kesi yao ishughuliiwe na haki itendeke.
Hapa kwetu Hakuna chama chochote kile kinacho mtuma mwanachama wake kudhulum wananchi, viongozi wa vyama wanatakiwa kuwa na mifani mizuri na itokeapo kuna baadhi yao wanafanya madhambi basi hizo ni nia zao mbaya na haimaanishi ni chama chake ndicho chenye dhambi.