Mbeya: Wanandoa Mbaroni Baada ya Kumshushia Kipigo Hadi Kifo Mtoto Wao wa Miaka Minne

Mbeya: Wanandoa Mbaroni Baada ya Kumshushia Kipigo Hadi Kifo Mtoto Wao wa Miaka Minne

Ilikuwa jumatano hospital ya rufaa Mbeya kushughulikia mwili wa anko wangu mtoto wa sister,niliuona huu mwili wa huyu mtoto manake alilazwa fridge ya juu baada ya fridge ya uncle wangu! Aysee mtoto kama amelala vile,amesukwa vizuri tunywele twake,dooh! Hao wazazi ni mashetani hakika
 
Ni matokeo ya mwanaume kupewa taarifa mbaya za mara kwa mara juu ya mtoto wake.
Na baba anajali zaidi furaha ya mwanamke kwa kutoa kipigo kwa mtoto.

Pole mtoto mzuri usiye na hatia!
Damu yako itawatafuta mpaka nao wanaondoka juu ya uso wa dunia.
Hao ni wanandoa au wanaishi kihawara TU?
 
Ufala huu... Nakumbuka kuna dogo wa miaka mitano jirani na nilipopanga alijiendeshea kitandani ucku akiwa kalala... Wazazi walipoamka asubuhi na jazba wakaanza kumpa kichapo cha mbwa koko!

Ikabidi niende kuingilia ugomvi na kuwazuia wasiendelee kumpga. Uzuri nilikuwa nawamudu, Nikawaambia km shida ni kufua kinyesi chake km walivyokuwa wanalalama mi nitafua ila wamwache dogo.

Ikabidi nimuulze dogo ilikuwaje akaharisha kitandani? Akanambia usiku tumbo lilikuwa linamuuma, alipomwamsha mama yake ampeleke chooni akakataa. Akamwambia km huwezi kuamka kunya hapohapo kitandani... Dogo kutokana na kushindwa kuichambua ile kauli ukilinganisha na umri wake pamoja na break kufeli akakuta tayari ashaharibu hali ya hewa kitandani

Sisi wazazi muda mwingine ndo visababishi vya watoto kufanya mambo ya ajabu!
Nakumbuka binti yangu wa kwanza akiwa na miaka 6 alijisaidia kitandani usiku, wakati anajishtukia na kujiangalia imekuwaje na mimi nikashtuka na kuskia harufu.
Bila shida nikamuinua kumpleka chooni nikamsafisha, na shuka nikabadili nikasafisha.
Imagine mtt anashangaa na amekazana kuniomba samahani. Kwangu haikuwa shida niliona ni changamoto ya ulezi tu. Na ilikuwa nipo mwenyewe baba kasafiri.

Mimi hata kumpiga mtt basi awe amekosa adabu mno.
 
Hongera sana kwa hilo... Unajua watoto wengi wanapitia unyanyasaji na ukatili kwa kuwa wazazi wanashindwa kureason kuwa alichokifanya na umri wake sio makusudi bali ni bahati mbaya.
 
Back
Top Bottom