UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Katika Mkoa wa Mbeya wenye zaidi ya watu 12,000 wenye ulemavu wa kusikia, ni kituo kimoja tu cha kutolea huduma za afya chenye mkalimani wa lugha ya alama. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Mbeya (CHAVITA).
Hata hivyo, nyuma ya hali hiyo, kuna maumivu makubwa yanayowakabili wagonjwa viziwi ambao mara nyingi hushindwa kuwasiliana kwa ufasaha na watoa huduma za afya, jambo linaloweka afya na usalama wao katika hatari.
Mwandishi wa Habari, Mwanaisha Makumbuli (kushoto) akizungumza na ambaye ana changamoto ya kutosikia.
Takwimu za Mfumo wa Elektoniki wa Usajili wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya (HFR) zinaonyesha kuwa hadi mwanzoni mwa mwaka 2026, Jiji la Mbeya lilikuwa na vituo 95 vya afya. Hata hivyo, ni kituo kimoja pekee kilichokuwa na mkalimani wa lugha ya alama, ambaye pia hakuwa katika utaratibu rasmi wa ajira.
Kuna madhara makubwa ya kutokuwepo kwa wakalimani wa lugha ya alama, ikiwemo kukosekana kwa usiri au faragha kati ya mgonjwa na mtoa huduma, pamoja na kushindwa kuelewa ushauri na nasaha anazopewa mgonjwa kutoka kwa daktari au mhudumu wa afya. Lightness Mgonagile, mama mwenye ulemavu wa kusikia, anakumbana na gharama ya ukosefu huo.
Lightness Mgonagile: "Jina langu Lightness Mgonagile. Mimi nashukuru sana. Kwa sababu kuna kipindi nilijifungua mtoto wangu wa kwanza, alikuwa sio kiziwi. Baadaye mtoto aliumwa, tukaenda hospitali. Sasa tukafika pale hospitalini hakuna mkalimani. Baadaye tulienda pamoja na mume wangu, tukafika pale hospitalini mtoto alikuwa anasikia vizuri. Lakini shida mkalimani hamna wala dokta alikuwa haelewi, hatukupewa dawa. Baadaye tukarudishwa nyumbani.
Tulipofika nyumbani tukaona mtoto anaendelea kuumwa, tukaenda kwa mama mkwe Tukuyu. Baadaye wakatuambia mtoto ana changamoto kubwa, amepata uziwi kwa sababu tumechelewa kupata huduma.
Kwa hiyo hiyo ndio shida ambayo niliipata kwa mtoto wangu wa kwanza. Ndio, kwa sababu huduma kule tulikosa, na tukikosa mkalimani mawasiliano yanakuwa shida sana. Na hiyo ndio sababu ambayo ilileta shida mpaka sisi tukashindwa kuelewana na dokta na kupata huduma nzuri, tunakuwa tunapata shida sana.
Hamna, yaani kunielewa hakuna kabisa. Lazima kidogo niende labda na mama kidogo ndio unakuta ananielewa kidogo na yeye, sio sana. Ndio ananisaidia hapa huku ananiambia, 'Hapa nina uchungu', au bibi namwambia mimi kidogo najisikia hivi ndio anamwambia nesi kule hospitalini. Lakini wenyewe mimi kama mimi nikienda hakuna huduma yoyote."
Lightness analazimika kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi mama yake mzazi ili amsaidie kuwasiliana na daktari.
Lightness Mgonagile: "Mimi mara nyingi nikifika pale, kwa mfano naumwa au kipindi ninakuwa na mimba, wakiniuliza pale unaumwa, kumjibu mama anashindwa. Wewe mwenyewe binafsi ukienda, eh, ndio hivyo hivyo au saa nyingine anawatumia meseji kuwaambia au anawaambia subirini mtu aje, naumwa, mama anamtumia meseji anakuja. Au wanasubiri wanaambia njia bado lakini inakuwa shida, kwa hiyo namwomba Mungu tujifungue kwa operesheni. Ndio, mara nyingi yaani nikiumwa tu nashindwa kweli kuelezea, basi. Hsante sana, kwenye uchungu ndio inakuwa shida zaidi."
Hali hii inakiuka wazi Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 2010, Kifungu cha 5 na cha 26 kinachotaka huduma za afya kutolewa bila ubaguzi wala kumnyima mtu haki yake. Hata katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, ambayo ndiyo pekee yenye mkalimani wa mkataba, madaktari wanakiri ugumu wa kazi.
Dr. Pascal Darama anaeleza "Lakini bado hawa wataalamu ni wachache kupelekea kwamba taasisi nyingi bado kuna hiyo changamoto ambapo wanakuwa wanakosekana. Kwa hiyo tunakuwa tunalazimika kutumia alama ya kutumia alama mbalimbali, lakini pia wengine wanaweza wanaweza wakaandika kwenye kikaratasi ana shida gani, akajieleza pale kwenye ile karatasi unaona amekuandikia, basi tumekuwa tukiwasiliana kwa njia hiyo.
“Lakini pia siku hizi kuna matumizi ya mitandao, kwa hiyo mnaweza mkaelewana mkatumia hata kwa njia ya meseji, anaandika kwenye kwenye kwenye simu anaeleza shida zake, then unaweza kutatua hiyo hiyo changamoto.
“Njia nyingine ni ni kutafuta mtu ambaye anaweza akasaidia kuweza kulink baina ya mtoa huduma na huyo mteja ambaye ana hiyo changamoto ya ukiziwi. Nikiri kwamba bado kuna changamoto katika kutoa hizi huduma, na ndio maana hata serikali inaendelea kupambana kuhakikisha kwamba wataalamu wengi wana ajiriwa kwenye hizi taasisi ili kuweza kusaidia wateja wetu wenye hizo changamoto na hayo makundi maalumu yenye hizo shida yaweze kupata huduma stahiki ambayo angesahili mtu mwingine ambaye anayo changamoto.
“Tukumbuke kuwa na hilo tatizo siyo kigezo cha yeye kwamba asipate huduma ambayo mtu mwingine ambaye hana hiyo changamoto angesahili kuipata."
Muuguzi wa hospitali hiyo, Lucas Kinyunyu, anaongeza kuwa kabla ya kupata mkalimani huyo, walitumia muda mrefu kuandikiana na wagonjwa.
Lucas Kinyunyu anaeleza: "Tunasema kiziwi yeye hasikii, sindio? Kwa hiyo kuto kusikia kwake kuna kunampa ugumu mtoa huduma kuweza kufanya mawasiliano ya moja kwa moja. Kwa hiyo inalazimu sasa either waanze kutumia either kuandika, sasa kwanza lazima ujue kwamba hasikii either kutumia njia nyingine za kuwasiliana nayo.
“Kama tulivyosema, either waanze unaandika halafu na yeye anakujibu, anaanza kujibu naye kwa kuandika, pia inachelewesha inachelewesha huduma. Kwa sababu utaandika, utampa, ataandika na yeye, kwa hiyo huo muda hata kama alikuwa na dharura bado inaweza ikaleta changamoto.
“Inakulazimu pia kutafuta mkalimani, sasa kama sehemu haina mkalimani maanake tayari huyo nani mteja anakosa huduma ambayo alikuwa anastahili, na anaweza akaona ni kama labda amepuuzwa lakini kumbe shida ni mawasiliano."
Ripoti ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) ya Septemba Mwaka 2023 kuhusu hali ya kimataifa ya usawa na ufikiaji wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu inaonyesha kuwa viziwi wanakabiliwa na changamoto mara sita zaidi kupata huduma za afya kuliko wengine.
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Mbeya, Tunsajigwe Mwalegwa anasema mateso huanza hata kabla daktari hajamwona mgonjwa.
Tunsajigwe Mwalegwa anasema "Kwanza changamoto tunazokutana nazo, ya kwanza, tunapewa kipaumbele kwamba sisi hatusikii, sisi hatuelewi, ah-ah. Tunajiangalia wenyewe, kwa mfano mimi ni mama wa watoto watatu, ninapoenda hospitalini, mtoto wangu anaumwa mwenyewe au mtoto wa mtu mwingine, lakini unakuta huduma ya mkalimani hakuna.
“Napata changamoto kuingia mapokezi, unamwandikisha jina, muda wanaita wanaita mwingine ukusikia hamna. Kwa sababu wanashangaa muda wote jina langu najua bado halijaitwa. Baadaye nakuja namuuliza dada vipi, anasema, 'Mimi mbona nakuita hamna'.”
Anasema 'Nimeita muda mrefu lakini hujatokea'. Namwambia, 'Samahani, mimi ni kiziwi'. Anasema, 'Ah, kiziwi maanake nini?' Namwambia, 'Mimi sisikii vizuri'.
Anasema, 'Ah, sawa sawa, njoo uanze kuandika upate huduma'. Hapo bado hujaingia kwa dokta, bado hujakutana na dokta. Halafu hapo anawaza unakuta dokta anaongea kidogo, sasa mimi angalau akitamka akinyanyua mimi naelewa, lakini hapo unakuta sipati kitu chochote.
“Unamwambia, 'Samahani, mimi kiziwi'. Mwingine anaweza akakuhurumia, akakuhudumia kwa maandishi, lakini akaniuliza taratibu una shida gani, mimi nakuta nashangaa, lakini mimi nilivyovumilia sauti yangu ya kukatakata tunaelewana, naanza kujieleza.
Sehemu ya pili ~ Mbeya: Baadhi ya Mifumo ya utoaji huduma kwa viziwi inakiuka Sheria za nchi na Mikataba ya Kimataifa
“Baadaye mwisho wa siku nakata tamaa, naona huduma siyo rafiki. Bila mkalimani hapa inakuwa dokta anaweza akaniandikia dawa nyingine, mimi nikapata madhara."
Huu ni kimya unaoumiza. Katika makala ijayo tutafichua kiini halisi cha kwa nini halmashauri na vituo vya kutolea tiba vinashindwa kuwa na wakalimani hawa.
Sehemu ya tatu ~ Taasisi na Serikali ziwekeze katika mafunzo ya watoa huduma kwa wenye changamoto ya kusikia
Andiko la: Mwanaisha Makumbuli
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.